settings icon
share icon
Swali

Je! Ahadi za Mungu ni gani?

Jibu


Kuna ahadi nyingi za Mungu katika Maandiko. Katika kila ahadi, Mungu anaahidi kwamba jambo fulani litafanyika (au halitafanyika) au litapeanwa au kutimia. Hizi sio ahadi duni, ahadi za kawaida kama vile tunavyofanya mara nyingi; ahadi hizi za Mungu ni ahadi thabiti, ahadi zisizo na shaka zilizotolewa na Mungu mwenyewe. Kwa sababu Mungu ni mwaminifu, wapokeaji wa ahadi za kimungu wanaweza kuwa na uhakikisho kamili kwamba kile Mungu ameahidi kwa hakika kitatimizwa (Hesabu 23:19).

Hapa kuna ahadi chache ambazo Mungu ameahidi:

Ahadi za Mungu katika Agano la Kale.
Mungu aliahidi kumbariki Ibrahimu na, kupitia uzao wake, ulimwengu wote (Mwanzo 12: 2–3). Ahadi hii, inayoitwa Agano la Ibrahimu, ililenga kwa Masiya anayekuja ambaye Ibrahimu alimtazamia (Yohana 8:56).

Mungu aliwaahidi Israeli kuwa atakuwa Mungu wao na kuwafanya watu Wake (Walawi 26: 12-13). Historia ya Agano la Kale imejaa mifano ya Mungu akitimiza ahadi hizi.

Mungu aliahidi kwamba ikiwa tutamtafuta tutampata (Kumbukumbu 4:29). Mungu hafanyi kuwa vigumu kumpata. "Bwana Mungu wetu yuu karibu nasi wakati wowote tunapomwomba" (Kumbukumbu 4: 7).

Mungu aliahidi ulinzi kwa watoto wake (Zaburi 121). Alikuwa mlinzi makinifu juu ya Israeli yote.

Mungu aliahidi kwamba upendo wake hautakoma (1 Mambo ya Nyakati 16:34). Yeye ni mwaminifu katika kila njia.

Mungu aliyaahidi Israeli kwamba dhambi zao zinaweza kusamehewa, ufanisi wao utarejeshwa, na taifa lao kuponywa (2 Mambo ya Nyakati 7:14). Toba ilifungua njia ya ushirika na baraka.

Mungu, chini ya masharti ya Agano la Musa, aliahidi ustawi kwa Israeli ikiwa watatii na uharibifu ikiwa wataasi (Kumbukumbu 30: 15-18). Kwa bahati mbaya, Israeli mwishowe ilichagua kutotii, na taifa likaangamizwa na Ashuri na Babeli.

Mungu aliahidi baraka kwa wote hufurahia kulitafakari Neno Lake (Zaburi 1: 1–3). Imani rahisi ina thawabu zake.

Ahadi za Mungu katika Agano Jipya.
Mungu aliahidi wokovu kwa wale wote wanaomwamini Mwanawe (Warumi 1: 16–17). Hakuna baraka nyingine kubwa kuliko karama ya bure ya wokovu wa Mungu.

Mungu aliahidi kwamba mambo yote yatatendeka kwa mema kwa watoto Wake (Warumi 8:28). Hii ndio taswira pana inayotuzuia kufadhaika na hali za sasa.

Mungu aliahidi faraja katika majaribu yetu (2 Wakorintho 1: 3-4). Yeye ana mpango, na siku moja tutaweza kushiriki faraja tunayopokea.

Mungu aliahidi maisha mapya katika Kristo (2 Wakorintho 5:17). Wokovu ni mwanzo wa uwepo mpya.

Mungu aliahidi kila karama za kiroho katika Kristo (Waefeso 1: 3). Huku, katika Agano la Kale, Israeli ilikuwa na ahadi ya baraka za kimwili, kanisa hii leo limeahidiwa baraka za kiroho "katika ulimwengu wa mbingu." Urithi wetu umehifadhiwa kwa ajili yetu (1 Petro 1: 4).

Mungu aliahidi kukamaliza kazi aliyoianzisha ndani yetu (Wafilipi 1: 6). Mungu hafanyi chochote kwa kiwango nusu. Alianza kazi ndani yetu, na ataakikisha kuikamilisha.

Mungu aliahidi amani tunapoomba (Wafilipi 4: 6-7). Amani yake ni ulinzi. "itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."

Mungu aliahidi kutimiza mahitaji yetu (Mathayo 6:33; Wafilipi 4:19). Hii haimaanishi kwamba tunapata kila kitu tunachotaka, bali mahitaji yetu yatatunzwa. Sisi ni wa thamani zaidi kuliko ndege wa agnani, na Baba yetu wa Mbinguni huwalisha ndege (Mathayo 6:26).

Ahadi za Yesu katika Injili.
Yesu aliahidi pumziko (Mathayo 11: 28-30). Kupitia Kalvari mizigo imeinuliwa.

Yesu aliahidi maisha tele kwa wale wanaomfuata (Yohana 10:10). Kumfuata Yesu hutuletea utimilifu zaidi wa kiroho kuliko vile tungetarajia.

Yesu aliahidi uzima wa milele kwa wale wanaomwamini (Yohana 4:14). Mchungaji Mwema pia aliahidi kutulinda salama: "Hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu" (Yohana 10:28).

Yesu aliwaahidi wanafunzi wake nguvu kutoka mbinguni (Matendo 1: 8). Kwa nguvu hii, "waliubadilisha ulimwengu" (Matendo 17: 6).

Yesu aliahidi kwamba atarudi kutukujia (Yohana 14: 2–3). Kuanzia hapo na kuendelea, tutakuwa pamoja Naye daima.

Kunazo ahadi zingine nyingi za Mungu ambazo zinaweza kuorodheshwa. Ahadi hizo zote hupata utimilifu wao kamili katika Yesu Kristo, "mng'ao wa utukufu wa Mungu" (Waebrania 1: 3). "Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Kristo ni "Ndiyo." Kwa sababu hii ni kwake yeye tunasema "Amen" kwa utukufu wa Mungu" (2 Wakorintho 1:20).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ahadi za Mungu ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries