settings icon
share icon
Swali

Je! Kunayo uhalali wa alama za siri za Biblia?

Jibu


Alama siri za kanuni ya Biblia zimefichika vile baadhi wanakisia ziko katika jumbe halisi ya Maandiko. Watu wengi hudai kuwa wemegundua kanuni za Biblia wakitumia mfumo wa hisebati. Baadhi yakanuni zinapatika kwa kuhesabu barua au kwa kukadiria dhamani kwa kila herufi katika maandiko (inayoitwa kadirio la dhamani katika Biblia). Kanuni ambazo ni ngumu kufahamu zinapatikana kwa usaidizi wa tarakilishi. Kwa mfano, wengine wanaangalia Isaya 53:5 ("Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu; adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona") na kutumia kila herufi ya kumi na mbili ya Kiebrania kuimla kifungu "Yesu ndilo jina langu."

Kwa hiyo kunaonekana kuwa na kanuni za nambari za Biblia ambazo zinafunua habari maalum, yenye maana. Hatuwezi kukataa kabisa uwezekano kwamba Mungu ujumbe "fiche" katika neno Lake. Mungu ana uwezo wa kupanga Neno Lake lililo na pumzia yake kwa njia iliyo ngumu. Walakini, Mungu anataka tulifahamu Neno Lake (2 Timotheo 3:16-17), hivyo lazima tuulize ni kwa nini "angefunika" Habari muhimu ambayo watu hawangeweza kuifafanua katika maelfu ya miaka.

Kunayo shida na dhana ya kanuni ya nambari za Biblia. Ya kwanza, Biblia haitupi dukuduku huu ya kuwepo kwa mambari za Biblia (Mithali 25:2), kwa hivyo nambari zote za Biblia ni kwa mjibu wa utunzi wa mwanadamu kwa maandiko. Nyakati zote ambazo Yesu anavinukuu vifungu vya Biblia, hakuna hata wakati mmoja alitumia kanuni ya "nambari za Biblia" ili kuleta maana. Mtume Paulo, wakati wote anarejelea vifungu kutoka Agano la Kale, hakuna hata wakati mmoja alitumia kanuni ya "nambari za Biblia" ilie kupeana maana ya ndani. Inaweza kusemwa vile vile kwa waandishi wote wa Biblia.

Pia, kanuni za nambari za Biblia sio ya muhimu. Chenye tunastahili kufahamu kutekeleza ki wazi na kinatokana katika kwa Neno la Mungu "moja kwa moja." Wokovu wetu unakuja kwa kumwita Kristo kutuokoa kutoka dhambini mwetu. Kumwita Kristo kunatokea wakati tunaiweka imani yetu Kwake. Imani huja kwa kusikia neno la Mungu. Kusikia hutokea wakati watu wanatoka nje na kuhuibiri injili kwa wengine (Warumi 10:9-17). baada ya wokovu, tunakua katika Kristo tunapolishwa kwa Neno la Mungu (Zaburi 119:9-11, 105; 2 Timotheo 3:16-17; 1 Petro 2:2). Vifungu hivi vyote vinarejelea kuichukulia andiko vile lilivyo na kuitekeleza kanuni yake. Wokovu na utakazo havitegei katika kutafuta nambari za Biblia.

Pia, kutambua nambari za Biblia mara nyingi huwa ni holela. Mchakato wa kugundua na kutafsiri hutegemea pakubwa mtazamo wa mtafiti. Hii hasa huwa kweli wakati nambari za Biblia zinatazamiwa kuwa za kinabii.

Je! Biblia ni kitabu changamani? Naam. Je! Ni changamani zaidi ya vile tunajua? Naam. Je! Kuna uwezekano kuwa Mungu alieka ujumbe fiche katika andiko la Maandiko? Naam, kuna uwezekano kuwa nambari za Kibiblia zipo. Lakini, kuisoma Biblia kwa njia ya kawaida, Biblia inajizungumzia yenyewe. Chenye tunahitaji kutoka kwa Biblia ni kupata kutoka somo la moja kwa moja la andiko lake (2 Timotheo 2:15; 3:16-17). Hamna haja kutumia wakati mwingi kwa jambo la kuhesabu herufi, kutafiti mfuatano, na mpangilio wa andiko katika sehemu tofauti ili tuafikie mtindo ulio na maswali na utahitaji kutafsiriwa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kunayo uhalali wa alama za siri za Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries