settings icon
share icon
Swali

Kuna jambo kama vile aliye kuwa Mkristo wakati mmoja na sasa si Mkristo?

Jibu


Hili ni swali ambalo hakuna jibu dhahiri na wazi la kibiblia. Waraka wa Kwanza Yohana 2:19 inasema, "Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu." Andiko hili linafanya wazi sana — hakuna kitu kama vile Mkristo wa zamani. Ikiwa mtu ni Mkristo kweli, hawezi kamwe kuondoka katika imani: "Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi." Ikiwa mtu aliyewai kuwa Mkristo na anakataa imani, yeye hakuwa Mkristo kweli. " Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu — kwenda zao kunaonyesha kwamba hakuna mmoja wao aliyekuwa wetu." Hapana, kwa kweli hakuna kitu kama vile Mkristo wa zamani.

Ni muhimu kutofautisha kati ya Mkristo wa kweli na "kwa jina tu" Mkristo. Mkristo wa kweli ni mtu ambaye amemtegemea kabisa Yesu Kristo peke yake kwa ajili ya wokovu. Mkristo wa kweli ni mtu anayeelewa kile Biblia inasema juu ya dhambi, adhabu ya dhambi, Yesu ni nani, ni nini Yesu alifanya kwa ajili yetu, na jinsi hutoa msamaha wa dhambi. Mkristo wa kweli ni mtu alimyepokea Yesu Kristo kama Mwokozi wa kibinafsi, amefanywa kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17), na anabadilishwa na kuwa sura ya Kristo. Mkristo huyu wa kweli ni mtu anayewekwa Mkristo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Waefeso 4:13, 30; 2 Wakorintho 1:22). Mkristo huyu wa kweli hawezi kamwe kuwa Mkristo wa zamani. Hakuna mtu ambaye ameweza kumwamini Kristo kikamilifu kama Mwokozi anaweza kumukana. Hakuna mtu anayefahamu kweli ya uovu wa dhambi, hofu ya matokeo ya dhambi, upendo wa Kristo, na neema na huruma ya Mungu, anaweza kugeuka kutoka imani ya Kikristo.

Kunao wengi katika ulimwengu huu ambao wanadai kuwa Wakristo, lakini sio. Kuwa Mkristo haimaanishi kuwa katika taifa fulani au kuwa na rangi fulani ya ngozi. Kuwa Mkristo haimaanishi kutambua kwamba Yesu alikuwa mwalimu mkuu, au hata kutafuta kufuata mafundisho Yake. Kuwa Mkristo inamaanisha kuwa mwakilishi wa Kristo na mfuasi / mtumishi wa Kristo. Kuna watu ambao wamekuwa na uhusiano fulani na kanisa la "Kikristo" na baadaye walikataa uhusiano huo. Kuna watu ambao "wamemwonja" na "kuona uzuri wa" Yesu Kristo, bila kumpokea kabisa kama Mwokozi. Hata hivyo, hakuna kitu kama Mkristo wa kweli wa zamani. Mkristo wa kweli hawezi kamwe, na hawezi kamwe, kukataa imani. Mtu yeyote ambaye alidai kuwa Mkristo, lakini baadaye anakataa imani ya Kikristo, hakuwa kamwe Mkristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuna jambo kama vile aliye kuwa Mkristo wakati mmoja na sasa si Mkristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries