Swali
Amri kumi ndio gani?
Jibu
Amri kumi ni sheria kumi katika Bibilia ambazo Mungu aliwapa taifa la Israeli muda mfupi baada ya kutoka Misri. Amri kumi hasa ni ufupisho wa amri 613 ambazo ziko katika sheria ya Agano La Kale. Amri za kwanza nne zahusika na uhusiano na Mungu. Zingine sita za mwisho zahusika na uhusiano na mtu kwa mtu. Amri kumi zimeorodheshwa katika Bibilia katika kitabu cha Kutoka 20: 1-17 na Kumbukumbu La Torati 5:6-21 na nikama zifuatazo:
1) “Usiwe na Mungu mwingine ila mimi.” Amri hii inapinga kuabudu miungu mingine ila tu Mungu wa kweli. miungu mingine yote ni ya uongo.
2) “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mini, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.” Amri hii inapinga kujichongea sanamu, yenye inaonekana kwa macho na inamwakilisha Mungu. Hakuna sanamu yo yote tunaweza kutengeneza sanamu ambayo inaweza kumuwakilisha Mungu ukamilifu. Kuunda sanamu imwakilishe Mungu ni kuabudu miungu ya uongo.
3) “Usilitaje bure jina la BWANA , Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.” Hii ni amri kinyume na kulitumia neno la BWANA vibaya. Hatustahili kulichukuliwa neno la Mungu kimsaha. Tunastahili kuonyesha heshima kwake kwa kumtaja kwa heshima na njia inayompa utukufu.
4) “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote; wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.” Amri hii ni kutenga Sabato (Jumamosi, siku ya mwisho ya juma) kama siku ya kupumzika ambayo imetolewa kwa Mungu.
5) “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi uewayo na BWANA Mungu wako.” Amri hii kila mara inaamrisha kuwafanyia wazazi vyema kila wakati kwa heshima na nidhamu.
6) “Usiue.” Amri hii inapinga uuwaji wa wanadamu wengine.
7) “Usizini.” Amri hii inapinga kuwa na mapenzi na mtu mwingine isipokuwa mume au mke wako.
8) “usiibe.” Amri hii inapinga kuchukua cho chote kisicho chako bila ruhusa ya mwenye kitu hicho.
9) “Usimshuhudie jirani yako uongo.” Amri hii inakataza kushuhudia uongo mtu mwingine.Hii ni amri inayopinga kudanganya.
10) “Usitamani nyumba ya jirani yako,usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.”Hii ni amri inayopinga kutamani cho chote ambacho si chako. Kutamani kunapelekea kufunja amri zimetajwa hapo juu: uuwaji, uzinzi, na wizi. Kama ni makosa kufanya kitu, pia ni makosa kutamani kufanya kitu hicho hicho
Watu wengu wanaangalia kimakosa amri kumi kama sheria zilizoundwa kuwa, ikiwa zitafuatwa, zitaakikishia mtu kuingia mbinguni baada ya kifo. Kwa kulinganisha, lengo la amri kumi ni kuwalazimiza kugungdua kwamba kwa ukamilifu hawawezi kutii sheria (Warumi 7:7-11), na kwa hivyo wanihitaji huruma na neema za Mungu. Mbali na madai kwamba tajiri mdogo katika Mathayo 19:16, hakuna mtu atakaye tii amri kumi kikamilifu (Mhubiri 7: 20). Amri kumi zaonyesha kuwa wote tumetnda dhambi ( Warumi 3:23) na kwa hivyo tunahitaji rehema na neema za Mungu, ambazo ziko kupitia kwa imani katika Kristo Yesu.
English
Amri kumi ndio gani?