settings icon
share icon
Swali

Je, nini asili ya mafundisho ya Utatu?

Jibu


Utatu katika Ukristo ni fumbo la kipekee, halieleweki na ni la kushangaza. Ni ufunuo unaoonyesha Muumba-mweza yote haswa ni nani-sio mungu tu,lakini ni kiumbe asiye na kipimo ambaye amekuwapo katika umilele kama watu watatu sawa, wasio na mipaka na vile vile washirika tofauti. Asili ya mafundisho ya Utatu ni katika Biblia ingawa neno hilo Utatu halitumiki katika Biblia.

Kama Wakristo wote wa Imani halisi wanavyokubaliana, mafundisho ya Utatu yanafundisha kwamba Mungu ni mmoja tu lakini hujidhihirisha katika nafsi tatu. Mungu ana asili moja lakini kuna nguzo tatu za ufahamu; Mungu ni mmoja tu lakini ana nafsi tatu. Watu wasio Wakristo kimakosa huita jambo hili ukanganyo. Badala yake, mafundisho ya utatu ni fumbo linalodhihirishwa na Mungu katika Neno lake. Mkanganyo utakuwa tukidai kwamba Mungu ako na asili moja na pia asili tatu ama kwamba yeye ni Mtu mmoja na pia watu Watatu.

Tangu mwanzoni mwa kanisa, Wakristo wameelewa fumbo la Utatu hata kabla kuanza kutumia neno Utatu.

Kwa mfano, Wakristo wa kwanza walijua kwamba Mwana alikuwa Muumba (Yohana 1:1-2), "Mimi Ndiye" katika Agano la kale (Kutoka 3:14; Yohana 8:58), ni sawa na Baba (Yohana 14:9), na Hakimu wa dunia yote ( Mwanzo 18:25; Yohana 5:22), ambaye anapaswa kuabudiwa kwa kuwa Mungu ndiye anayestahili (Kumbukumbu la Torati 6:13; Luka 4:8; Mathayo 14:33).

Wakristo wa Kwanza walijua kwamba Roho mtakatifu alikuwa Mtu tofauti, ambaye alikuwa na fikra zake na mapenzi yake (Yohana 16:13), ambaye anatuombea sisi kama apendavyo Mungu (Warumi 8:27), kudhibitisha kwamba Yeye ni Mtu tofauti na Mungu Baba-kwa kuwa maombezi inahitaji watu wawili ( hakuna anayefanya maombezi peke yake). Kwa kuongeza, mwanadamu anaweza kusamehewa kwa kumfukuru Mungu Mwana, lakini sio kwa kumfukuru Mungu Roho Mtakatifu (Mathayo 12:32).

Waandishi wa Agano Jipya wanawataja pamoja watu watatu wa Utatu mara nyingi ( Kwa mfano., Warumi 1:4; 15:30; 2 Wakorintho 13:14; Waefeso 1:13-14; 1 Wathesalonike 1:3-6). Waumini wa kwanza walijua kwamba Baba na Mwana walituma Mtu wa tatu wa Utatu, Roho Mtakatifu-" Mshauri mwinine"-kuishi katika mioyo yetu (Yohana 14:16-17, 26; 16:7). Fumbo hii ilikubalika kikamilifu na kanisa la kwanza kama ukweli uliofunuliwa ingawa haikufahamika kama "Utatu Mtakatifu."

Agano la kale lilitoa ufafanuzi wa Utatu na hakuna kifungu cha maandiko ambacho kinapingana na fundisho hilo. Kwa mfano, katika Mwanzo 1:26 Mungu anasema kwa wingi, "Na tumfanye mtu kwa mfano wetu." Mungu anatangaza kwamba alikuwa peke yake alipoumba kila kitu, akinyoosha mbingu na kutandaza dunia "peke yangu" (Isaya 44:24). Walakini Yesu alikuwa chombo cha uumbaji wa Mungu (Yohana 1:1-3; Wakolosai 1:16), katika ushirika wa Roho Mtakatifu ambaye alikuwa akitanda juu ya maji (Mwanzo 1:2). Ni mafundisho ya Utatu tu yanayoweza kueleza haya yote.

Torati ilielezea wazo la Mungu aliye ndani ya Watu kadhaa na kutabiri kuja Kwake kwa kimwili. Agano la kale limejawa na marejeleo ya mtawala wa ulimwengu atakayekuja (Mwanzo 49:10) atakayezaliwa huko Bethlehemu (Mika 5:2), ambaye hakuwa tu Mwana wa Mungu (Isaya 9:6) lakini Masihi ambaye angekuwa Mungu katika mwili (Isaya 7:14; Zekaria 2:8-11). Lakini Wayahudi chini ya utawala wa Warumi walikuwa wanatafuta na kutumaini kupata Masihi mshindi, sio Mtumishi wa hali duni (Isaya 53). Israeli ilishindwa kumtambua Mwana wa Mungu kwa sababu ya hali yake hafifu. (Isaya 53:2; Mathayo 13:54-58; Yohana 10:33), na wakamuua (Zekaria 12:10; Matendo ya Mitume 2:36).

Miaka baada ya kifo cha nabii wa mwisho, Yohana, kulikuwa na majaribio mengi ya wanatheolojia Wakristo kufafanua na kuelezea kanisa juu ya Mungu. Maelezo ya ukweli wa kiroho kwa wanadamu wa ulimwengu kamwe hayatafahamika; baadhi ya maelezo ya walimu wengine yalikuwa ya uzushi, na mengine hayakuwa ya kweli. Baadhi ya makosa yaliyowekwa wazi katika nyakati za baada ya mitume yalikuwa, Yesu kuwa Mungu na kuoneka tu kama mwanadamu, wazo la Yesu kuumbwa badala ya Yeye kuwa wa milele, kuwepo kwa miungu tatu tofauti katika familia moja, na kwa Mungu mmoja anayetekeleza majukumu tatu kwa wakati tofauti.

Hakuna dini itakayokuwepo bila kujua nani au nini ambacho wafuasi wake wanaabudu kwa hivyo kulikuwa na hitaji kubwa la kufafanua Mungu kwa njia ambayo wafuasi wote wa Ukristo wangekubaliana kuwa "rasmi" au fundisho la kweli.

Inaonekana kwamba baba wa kanisa hilo Tertullian (BK 160–225) alikuwa wa kwanza kutumia neno Utatu kuelezea Mungu. Tertullian anatumia neno hilo katika kitabu chake Against Praxeus, kilichoandikwa mnamo 213 kuelezea na kutetea Utatu dhidi ya mafundisho ya wakati huo ya Praxeus, ambaye aliweka wazi mafundisho ambayo yalipinga Utatu. Kutoka hapo, tunaweza kuangazia zaidi ya karne moja ya majadiliano ya kanisa, mgawanyiko wa kanisa, na mjadala wa baraza la Nicea mnamo 325, wakati ambapo Utatu mwishowe ulidhibitishwa kuwa fundisho rasmi la kanisa.

Uangalizi wa mwisho. Theolojia ni jaribio la wanadamu wenye dosari kujaribu kuelewa maneno ya Biblia, kama vile sayansi ni jaribio la wanadamu wenye dosari kujaribu kuelewa ukweli kuhusu asili. Ukweli wote wa asili ni kweli, vilevile maneno yote ya biblia ni kweli. Lakini kama vile historia inavyoonyesha, wanadamu wakona mipaka na hufanya makosa mengi. Kwa hivyo ambapo kuna makosa au kutokubaliana katika sayansi au theolojia, zote zina njia ya kufanya marekebisho. Historia katika kanisa la kwanza inaoyesha kwamba waumini wengi wa Kikristo walikosea katika kuelezea asili ya kweli ya Mungu (somo kuu huhusu hitaji ya unyenyekevu). Lakini kupitia kusoma neno la Mungu kwa uangalifu, mwishowe kanisa liliweza kuelezea kile ambacho Biblia inafunza wazi na kile walijua kuwa kweli-kwamba Mungu yupo kama Utatu wa milele.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, nini asili ya mafundisho ya Utatu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries