settings icon
share icon
Swali

Je! Asili ya ubatizo ni gani?

Jibu


Kwanza, ni lazima ieleweke kwamba ubatizo ni tangazo la nje la uongofu wa ndani. Kwa maneno mengine, ubatizo ni tendo la sherehe linalofanyika baada ya mtu kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake. Hii kwa kawaida hufanywa mbele ya kanisa kama tangazo la hadhara la imani ya mtu.

Kuhusu asili ya ubatizo, wanatheolojia wa Kikristo wanapendekeza kwamba, ingawa ubatizo ulitumiwa na Yohana Mbatizaji, ubatizo wenyewe haukuanza na Wakristo au, kwa sababu hiyo, na Yohana. Wayahudi walifanya ubatizo kama kitendo cha jadi cha utakaso na kuanzisha waongofu kwa Uyahudi muda mrefu kabla ya kuja kwa Masihi. Asili ya ubatizo inaweza kupatikana katika kitabu cha Walawi ambapo makuhani Walawi waliamriwa kufanya utakaso wa mfano katika maji kabla na baada ya kutekeleza majukumu yao ya ukuhani. Mambo ya Walawi 16: 4 inatuambia, "Atavaa koti takatifu la kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani; atafunga mshipi wa kitani kiunoni, na kuvaa kilemba cha kitani. Haya ni mavazi matakatifu, kwa hiyo ni lazima aoge kwa maji kabla ya kuyavaa mavazi hayo." Maandiko pia yanasema katika Mambo ya Walawi 16: 23-24, "Kisha Aroni ataenda ndani ya Hema la Kukutania na kuvua yale mavazi ya kitani aliyoyavaa kabla ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu, naye atayaacha pale. 24Ataoga kwa maji katika mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake ya kawaida. Kisha atatoka na kutoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yake na sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya watu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe, na kwa ajili ya watu."

Ingawa kitendo kilichoelezewa katika vifungu hivi vya Agano la Kale haikuitwa hasa "ubatizo," vinaangazia jinsi sherehe takatifu (na vitendo) na utakaso ni muhimu kwa Mungu. "Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa toba" (Luka 3: 3; Matendo 19: 4) ulifuata dhana hii ya utakaso, ingawa utakaso wa mwisho kutoka kwa dhambi unapatikana tu kupitia Kristo, na ubatizo wa Yohana ulikuwa kielelezo cha ubatizo huo. Umuhimu wa ubatizo kama sherehe ya Agano Jipya ni kwamba, kama waumini wa Yesu Kristo, tumebatizwa katika kifo chake (Warumi 6: 3) na kufufuliwa kutembea katika maisha mapya (Warumi 6: 4). Bwana alifundisha umuhimu wa ubatizo kwa kiwango kwamba Yeye mwenyewe alibatizwa na Yohana Mbatizaji mwanzoni mwa huduma yake (Marko 1: 9).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Asili ya ubatizo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries