Swali
Je ni mbinu zipi tofauti za kujifunza bibilia?
Jibu
Kunazo mbinu tofauti tofauti tunaweza kutumia kujifunza bibilia kwa njia mwafaka na ya kueleweka. Kwa mujibu wa sehemu hii, tutazigawanya kwa viwango viwili vikuu: masomo ya vitabu na pia masomo ya anwani. Kabla tujadiriane namna tofauti za kujifunza bibilia, ni muhimu tutambue kuwa vyote vina vitu vinavyofanana na lazima zifuate mtindo ama sheria fulani ndipo tuepuke kutafsiri bibilia visivyo. Kwa mfano, njia yeyote ile ya kujifunza bibilia tutakayotumia, ni muhimu kwa makini somo lizingatie mazingira ya kifungu kinachosomwa, punde tu baada ya sura ama kitabu chenyewe na kadhalika katika mazingira yote ya bibilia. Lengo letu kuu ni kuweza kuelewa ni ipi ilikuwa maana halisi iliyokusudiwa katika kifungu hicho. Kwa maneno mengine ni kuwa, ni yapi yalikuwa malengo ya mwandishi, na ni vipi aliokusudia kuandikia wangeyaelewa aliyoyaandika? Kauli hii inatambua kuwa bibilia haikuandikwa pasipo kusudi, ila ni andiko la kihistoria lililoandikwa kwa wakati fulani kwa historia ikilenga akili za watu fulani kwa lengo maalumu. Baada ya kuelewa maana ya kifungu hiki, basi tunafaa kutafuta kuelewa namna inatuashiria sisi kwa nyakati hizi.
Somo la Vitabu: Mbinu hii ya kusoma vitabu inaangazia aidha kusoma kitabu chote kwenye bibiblia ama sehemu fulani ya kitabu, kama vile sura fulani, vifungu kadhaa, ama pia kifungu kimoja. Ikiwa ni mbinu ya kusoma sura ama kifungu baada ya kingine na pia kusoma kitabu chote, sheria na malengo ni sawia. Kwa mfano, ndio tuweze kusoma kitabu kizima kwa kina, ni muhimu pia kupitia malengo ya sura na hata vifungo vilivyomo. Kadhalika, ndiposa tuweze kuelewa kifungu fulani, tunafaa kuifahamu sura yote na ujumbe ulioko na kitabu hicho kifungu kinapatikana. Na ikiwa tunasoma kifungu pekee ama kitabu chote, lazima tuwe tunaangalia lengo kwa ujumla kwenye bibilia pia.
Kusoma ki anwani: Kunazo aina kadhaa za anwani tunazoweza kusoma. Baadhi ya mifano ikiwa ni kusoma kumhusu mtu fulani, na hapa tunasoma jinsi bibilia inasema kumhusu mtu fulani; kusoma maneno, tunaangazia vile bibilia inasema kuhusu neno fulani ama anwani; Na kusoma kwa maeneo, ambapo tunasoma kile tuwezayo kuhusu jiji, nchi ama taifa linalotajwa kwenye bibilia. Kusoma ki anwani ni muhimu kwa kweza kuelewa kile bibilia inafunza katika lengo fulani ama sura. Hata ivyo tunafaa kuwa maakini kuwa ile maoni inatolewa katika kusoma huku wa ki anwani isije ikatoa maana ya vifungu iliyokusudiwa ya awali ili iweze kumaanisha maana ambayo haitaweza kujitokeza hata baada ya kusoma sura ama kitabu chote. Mbinu hii ya kujifunza ki anwani ni ya maana kwa kupanga na kuelewa kile bibilia inafunza kwa anwani fulani.
Katita kusoma bibilia, ni muhimu kutumia mbinu tofauti za kusoma bibiblia kwa nyakati tofauti. Wakati mwingine tunaweza kutaka kuongeza muda kusoma kitabu na wakati mwingine tutafaidi pakubwa kwa kusoma bibilia ki anwani. Mbinu yoyote ile tunayoitumia tunafaa mwelekeo huu wa kimsingi: 1-Kuchunguza- Bibilia inasema nini? 2- kutafsiri-Bibilia inamaanisha nini? Na 3- Kutumia-Ni vipi maneno haya ya kweli ya bibilia inaangazia kwenye maisha yangu, ama ni nini umuhimu wa kifungu hiki kwa maisha ya sasa? Kwa kutumia mbinu yoyote ile kujifunza bibilia, tunafaa kuwa maakini katika neno la Mungu ili tuwe watenda kazi ambao hawatakuja kuaibishwa. [2Timotheo 2:15]
English
Je ni mbinu zipi tofauti za kujifunza bibilia?