Swali
Ni vipi mbinu tofauti za uandishi wa bibilia zinaweza kuadhiri jinsi tunavyofafanua bibiblia?
Jibu
Bibilia ni kusanyiko la kazi ya fasihi. Fasihi inajitokeza kwa namna tofauti ama kupangwa kwa njia maalumu, na kila moja inasomwa na kukubalika kwa jinsi ilivyo. Kwa mfano, Kuchanganya vitabu vya sayansi na vile vya udaktari vitasababisha madhara makubwa –vinafaa kueleweka jinsi kila kimoja kilivyo. Kadhalika vitabu vya sayansi na vile vya udakitari ni lazima vieleweke tofauti na ushahiri. Kwa hivyo, utafiti wa kina na ufafanuzi unaofaa ndio unatiliwa mkazo kwa lengo na mbinu katika kila kitabu ama fungu katika sura, Kadhalika, baadhi ya vifungu kwa kina na ufafanuzi yazo unatiwa mkazo kwa kuelewa mbinu za uhandishi zilizotumika. Kwa kukosa kuelewa mbinu iliyotumika ya uhandishi inaweza sababisha kutoelewa kwa maandishi ya vifungu.
Mbinu kuu za uhandishi kwenye bibilia ni: sheria, hisitoria, hekima, ushairi, simulizi, nyaraka, unabii, na maelezo yaliyo fiche. Mtasari ufuatao ni toafauti kati ya mbinu hizi na jinsi kila moja inavyoweza kufafanuliwa:
Sheria: Hii ni pamoja na vitabu vya Mambo ya Walawi na Torati. Lengo la sheria ni kueleza kusudi la Mungu kuhusu uongozi, kazi za muhubiri, majukumu ya kijamii na kadhalika. Ufahamu wa tabia za Kiibrania na sheria za nyakati, hali kadhalika ufahamu wa maagano, ni ziada katika kusoma nakala hizi.
Historia: hadithi na maelezo katika bibilia zimejumuishwa katika mbinu hii ya uandishi. Karibu kia kitabu kwa Bibilia kina sehemu ya historia, ila Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Yoshua, Waamuzi, 1 na 2 Samweli, 1 na 2 Wafalme na 2 Mambo yaa Nyakati, Ezra, Nehemia, na Matendo ya mitume zote sana ni za historia. Ufahaamu kuhusu historia ya kiulimwengu ni wa muhimu, kwa vile unaambatana kiukamilivu na historia ya kibibilia na kufanya ufafanuzi kuwa wa kina.
Hekima: Hii ni mbinu ambayo inafunza maana ya maisha na jinsi ya kuishi. Baadhi ya lugha inayotumika katika uhandishi wa fasihi ya hekima ni misemo na ushairi, na ili linafaaa kuchukuliwa kiundani wakati wa ufafanuzi. Baadhi ya vitabu hivyo ni Mithali, Yakobo na Mhubiri.
Ushairi: Hizi ni pamoja na vitabu vilio na mtiririko wa kisanii, vinaoambatana, vya majazi, kama vile Wimbo ulio Bora, Mambolezo, na Zaburi. Tunafahamu kuwa Zaburi nyingi ziliandikwa na Daudi mwenyewe aliyekuwa mwanamuzuki ama kiongozi wake wa ibada, Asafu. Kwa sababu ushairi ni ngumu kutafsiri, tunapoteza baadhi ya mtiririko wa kimuziki wakati wa utafsiri. Hata hivyo tunapata matumizi ya usawe, kufananisha, na kuzingatia katika fasihi hii kama vile tu kwenye muziki wa kisasa.
Usimulizi: Mbinu hii inatumika sana katika vitabu vya injili, ambavyo ni simulizi kumhusu Kristo, na pamoja na vitabu vya Ruthu, Esta na Yona. Msomaji anaweza kupata mbinu zingine zikijitokeza kwenye vitabu vya Injili, kama vile fumbo [Luka 8:1-15] na mazungumzo [Mathayo 24]. Kitabu cha Ruthu ni mfano wa hadithi fupi, inayopendeza kwa uelezo na ufafanuzi.
Nyaraka: Waraka ni barua, inayoandikwa kwa namna inayoeleweka. Kunazo barua 21 katika Agano Jipya kutoka kwa mitume kwenda kwa makanisa mbali mbali ama watu binafsi. Hizi barua zina mbinu inayofanana na barua za kisasa, ikiwa na ufunguzi, salamu, mwili na kufunga. Maana ya barua ni pamoja na kufafanua mafunzo ya hapo awali, kukemea, kuelezea, kurekebisha mafundisho ya uongo na pia kufunza Zaidi mafundisho ya Yesu. Msomaji atafanya vyema kuelewa utamaduni, historia na uhusiano wa wahusika wa awali ndiposa kupata maelezo Zaidi kutoka kwa vitabu hivyo.
Unabii na fasihi ya kubuni: Maandishi ya kiunabii ni vitabu vya Agno la kale vya Isaya hadi Malaki, na cha Agano jipya cha Ufunuo wa Yohana. Vinajumuhisha pamoja na utabiri wa matukio yajayo, thahatari kuhusu hukumu inayokuja, maono na mipang ya Mungu kwa Waisraeli. Fasihi ya kubuni ni mfano maalumu wa unabii, pakubwa unaohusika na sanamu na mifano na inayotabiri kuhusu janga na uharibifu. Mfano wa aina hii ya mbinu inatumika katika Danieli [mazimwi ya sura ya 7], Ezekieli [maandishi ya sura ya 3], Zakaria [taa ya dhahabu ya sura ya 4], na Ufunuo [waendesha farasi wane sura ya 6]. Vitabu vya unabii na fasihi ya kubuni ndivyo mara nyingi vimedhaniwa kuwa na upungufu na kuvitafsiri kibinafsi kukijumuishwa na hisia na maoni yasio sawa. Aidha, Amosi 3:7 inatuambia "Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake." Kwa hivyo tunafahamu ukweli ushasemwa, na unaweza kujulikana kupitia kwa utabiri wa makini sawia na kufahamu bibilia, na kwa njia ya maombi. Mambo mengine yatabakia kuwa fiche kwetu hadi kwa wakati ufaao utakapofika, kwa hivyo si vizuri kujifanya kuwa tunaelewa kila kitu inapofika ni kwa maandishi ya unabii.
Kuelewa kwa mbinu za uhandishi wa bibilia ni muhumu kwa mwanafunzi wa bibilia. Ikiwa mbinu isiyofaa imetumika katika kifungu, inaweza ikakosa kueleweka ama kufahamika, na hiyo inaweza kuleta kutoeleweka kwa ile Mungu alikusudia kusema. Mungu si mwandishi wa kuleta mchanganyiko [1 Wakorintho 14:33], na anatutaka "kitumia kwa halali neno la kweli" [2 Timotheo 2:15]. Kadhalika, Mungu anatutaka kujua mipango yake kuhusu ulimwengu na kwetu kama mtu binafsi. Ni jambo la kufurahisha kikamilifu tukija kufahamu jinsi ulivyo upana, na urefu, na ukubwa, na kina upendo wa Mungu ulivyo kwetu [Waefeso 3:18].
English
Ni vipi mbinu tofauti za uandishi wa bibilia zinaweza kuadhiri jinsi tunavyofafanua bibiblia?