settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu mateso?

Jibu


Neno "mateso" au aina yake inaonekana mara zaidi ya 70 katika Maandiko. Matumizi ya kwanza ya neno huelezea asili ya mateso wakati wa kuzaa: "Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala" (Mwanzo 3:16). Mazingira hapa ni kwamba Adamu na Hawa walikuwa wamefanya dhambi na uchungu wa kujifungua ni moja ya matokeo ya dhambi. Kwa sababu ya dhambi, dunia yote ililaaniwa, na mauti yakaingia kama matokeo (Warumi 5:12). Kwa hiyo, inaweza kuhitimishwa kwamba mateso ni mojawapo ya matokeo mengi ya dhambi ya awali.

Ingawa hiyo haijaelezewa katika Biblia, kimatibabu tunajua kuwa mateso ni zawadi. Bila hivyo hatujui wakati tunahitaji matibabu. Kwa kweli, ukosefu wa mateso ni mojawapo ya matatizo yanayohusiana na ukoma. Watoto hawawezi kujifunza kwamba kugusa jiko la moto ni wazo mbaya, wala kuhatarishwa na hali chungu ya matibabu bila machungu yanayohusiana nayo. Kwa kiroho, mojawapo ya faida ya mateso inaonyeshwa na Yakobo: "Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi" (Yakobo 1: 2-3). Kwa mujibu wa Yakobo, tunapovumilia majaribu ya mateso, tunaweza kufurahia kujua kwamba Mungu anafanya kazi ndani yetu kuzalisha uvumilivu na tabia kama Kristo. Hii inatumika kwa mateso ya akili, kihisia na kiroho pamoja na mateso ya kimwili.

Mateso pia hutoa fursa moja ya kupata neema ya Mungu. Fikiria kile Paulo alichosema: "Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu" (2 Wakorintho 12: 9). Paulo alikuwa akizungumza juu ya "mwiba wa mwili wake" ulikuwa unamsumbua. Hatujui ni nini, lakini ilikuwa inaonekana kuwa uchungu kwa Paulo. Alitambua kwamba neema ya Mungu ilipewa kwake ili aweze kuvumilia. Mungu atawapa watoto Wake neema ya kustahimili machungu.

Lakini habari njema ni kwamba Yesu alikufa mahali petu kwa ajili ya dhambi zetu: "Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa" (1 Petro 3:18). Kupitia imani katika Yesu Kristo, Mungu anampa muumini uzima wa milele na baraka zote zinazojumuishwa. Moja yao ni " Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita"(Ufunuo 21: 4). Mateso tunayopata kama sehemu ya asili ya kuishi katika ulimwengu ulioanguka, wenye dhambi, yatakuwa kitu cha zamani kwa wale ambao, kupitia imani katika Kristo, wataishi milele mbinguni pamoja Naye.

Kwa muhtasari, ingawa mateso si mazuri, tunapaswa kumshukuru Mungu kwa sababu inatuonya kuwa kuna kitu kibaya katika mwili wetu. Pia, inatufanya kutafakari juu ya matokeo mabaya ya dhambi na kuwa na shukrani sana kwa Mungu kwa kutengeneza njia ya sisi kuokolewa. Wakati mtu ana mateso, ni wakati mzuri wa kutambua kwamba Yesu alivumilia mateso ya kihisia na ya kimwili kwa niaba yetu. Hakuna mateso ambayo yanaweza kukaribia matukio ya kutisha ya kusulubiwa kwa Yesu, na alipatwa na mateso hayo kwa hiari ili atukomboe na kumtukuza Baba yake.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu mateso?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries