settings icon
share icon
Swali

Ufafanuzi bora wa bibilia ni nini?

Jibu


Ufafanuzi unamaanisha "kujionyesha ama kujieleza." Ufafanuzi wa bibilia unajumuhisha kuchunguza kifungu fulani katika maandishi ili kueza kuielezea kikamilivu. Utafiti ni sehemu Ya utafiti wa kisayansi. Mtu anayefanya kazi ya ufafanuzi ni mfafanuzi.

Ufafanuzi mwafaka wa bibilia unadhirika katika maandishi. "Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli" [2 Timotheo 2:15]. Kulingana na kifungu hiki, tunafaa kujishirikisha na neno la mungu vilivyo, kupitia kwa kuisoma kwa makini. Kama hatuwezi, tuna sababu ya kuaibika.

Kunazo sharia maalumu za ufafanuzi ambazo mwanafunzi makini wa bibilia anafaa kufuata:

1. Sheria ya lugha. Bibilia iliandikwa kwa lugha ya binadamu, na lugha ina maumbile maalulu na inafuata sharia fulani. Kwa hivyo, inatufaa kuifafanua bibilia kwa njia ambayo inafuata kanuni na sheria za lugha.

Kwa kawaida, mfafanuzi huanza ufahamu wa kifungu katika maandishi kwa kuelewa maneno yaliyotumika. Kuelezea ni msingi kwa kuelewa kifungu kwa jumla, na ni muhimu kuwa maneno yameelezewa kulingana na maana yake halisi na sio tu vile kulingana na matumizi ya kisasa. Kwa kuhakikisha ufasaha, mfafanusi hutumia kamusi ya kigiriki na Kiibrania katika utafsiri.

Kisha mtafiti huchunguza mpangilio, ama uhusiano wa lugha ya maneno katika kifungu. Hupata yanayokinzana, hufafanua ni yapi ya msingi na ni yapi yasiyo ya maana, na hupata matendo, masomo na vishirikishi vyao. Anaweza kufafanua kifungu ama viwili kwa mchoro.

2. Sheria ya maana ya nje. Tunalenga kuwa kila neno katika kifungu lina ukawaida, maaana fiche, ila wakati kuna maana muhimu kuitazama kama mbinu ya mazungumzo. Mfafanuzi haendi Zaidi kuifanya kiroho ama kuifafanua. Maneno humaanisha kile maneno humaanisha.

Kwa hivyo kama bibilia inataja farasi, inamaanisha farasi. Bibilia inaposema kuhusu inchi ya ahadi, inamaanisha inchi iliyopewa Waisraeli na haifai kufafanuliwa kumaanisha mbinguni.

3. Sheria ya kihistoria. Muda unaposonga, tamaduni hubadilika, maono ya mtazamo hubadilika, lugha pia hubadilida.Tunafaa kuwa makini dhidi ya kufafanua maandishi jinsi tamaduni zetu zinavyotazama vitu; ni lazima tuweke maandiko katika mtazamo wa kiasili kihistoria.

Mwanafunzi makini wa bibilia atazingatia mahali, tamaduni, matukio ya kisasa, na hata mtazamo wa kisiasa wa wakati huo wa kuandikwa kwa kifungu. kufahamu kwa tamaduni za Wayahudi za zamani utasaidia pakubwa katika kufahamu maandishi. Kufanya utafiti wake, mfafanuzi anaweza kutumia kamusi za bibilia, majalida na vitabu vya historia.

4. Sheria ya kuweka pamoja. Mtafsiri wa maandishi aliye bora ni maandishi yenyewe. Tunafaa kuchunguza kifungu kwa misingi ya mazingira yake ya karibu [vifungu vinavyo izunguka], maana yake kwa upana [kitabu kinachopatikana ndani yake], na maana yake kwa ujumla [bibili yenyewe kiujumla]. Bibilia haija jikanganya yenyewe. Maneno yoyote ya kitiolojia katika kifungu kimoja yanaweza kueleweka katika mafungu mengine ya kitiolojia katika sehemu zingine za maandishi. Ufafanuzi mwafaka wa bibilia unaafikiana na maana ya maandishi katika vifungo kwa jumla.

5. Sheria ya maonyesho. Baada ya kutafiti kifungu vilivyo na kuelewa maana yake, tunalo jukumu la kutumia maneno hayo katika maisha yetu. Kwa "kufahamu neno la kweli" ni Zaidi na mazoezi ya akili; ni matukio ya kubadili maisha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ufafanuzi bora wa bibilia ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries