settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kuwa mkaidi / ukaidi?

Jibu


Kwa tamaduni zingine, "mkaidi kama nyumbu" ni msemo unaotumik kulenga wale wasio imara. Zaburi 32: 8-9 inanakiri ukaidi nyumbu inaposema, "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;nitakushauri jicho langu likikushauri.Msiwe kama farasi wala nyumbu,walio hawana akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu sharti kuwazuia hao,au hawatakukaribia. "Inapofikia kufuata amri za Mungu, hatufai ukaidi wala kukosa mwelekeo au wasiwasi. Hatuai kutoa vichwa vyetu mbali na "kufanya shingo ngumu." Tunafaa kusoma uvumilivu na kuweza kuzalisha mikononi mwake. Sio mapenzi yetu kwa Mungu kututumia kidogo na anavyohitaji.

Biblia imenakiri matukio ya ulazi, ile ya nyumbu sawia na ya watu wakati fulani. Kwa Agano la Kale, Farao alitambulika kuwa mkaidi (Kutoka 7: 13-14), bali rejeo lake halikumfamyia yeye na taifa lake zuri lolote. Unyumbu ulidhihirishwa baadaye n wana Israel,taifa teule la Mungu,waliomkaidi Mungu mara kwa mara,waliokaidi upendo na ulinzi wa Mungu. Hakik kwa Kiebrania tasiri ya "ukaidi"inamaanisha "kugeuzwa mbali,kimaadili, ya kuasi, na kurudi nyuma."

Agano la Kale linanakiri kwa masikitisho historia ya Wayahudi ambao walimgeuka Mungu kwa ukaidi, wakasahau kazi zake,kukosa kutii torati zake, na kufuata miungu ya kiajabu. Kwa Kumbukumbu la Torati 9, Musa anasimulia ukaidi wa Israeli kuhusiana na ndama ya kidhahabu waliyoifanya katika Mlima Sinai. Wakati huo Mungu alimwambia Musa, "Nimeliona taifa hili na tazama ni taifa lenye shingo ngumu" (Kumbukumbu la Torati 9:13). Hamaki ya Mungu ilikuwa juu sana hadi akaonelea kuangamiza taifa lote kabisa kwa njia yao ya ukaidi, "shingo ngumu" (mstari wa 14

Mungu huonelea ukaidi kuwa dhambi kubwa sana kwamba alijumuisha kile kinachoonekana leo kuwa adhabu kali kwa anaye kaidi na waasi. Kma mwana alikosa kutii wazazi wake, hawezi itikia nidhamu na aliishi maisha yasiyofaa, wazazi walipaswa kumleta mbele ya wazee wa jiji lake na "waume wote wa mji wake na wamtupie mawe,afe;ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako;na Israel wote watasikia na kuogopa."(Kumbukumbu la Torati 21:21).Ukaidi na kumkataa Mungu na mamlaka yake iliyotambulika ni kosa kubwa, ambayo inaweza kuenezwa kama sumu katika jamii. Torati ya Musa dhidi ya ukaidi ililenga kukomesha kusambazwa.

Katika Agano Jipya,kuna mifano mingi kuhusu ukaidi. Yesu alipoponya mtu aliyepooza siku ya Sabato, Mafarisayo na moyo yao migumu ikahuzunika na kumkasirisha Yesu.Mioyo ya uasi ya Mafarisayo iliwafanya wakajaribu kumwua, badala ya kumsifu Bwana kwa nguvu zake za uponyaji na kukubali Masihi wao (Marko 3: 1-6). Stefano alipokuwa akifunga usemi wake kabla ya Sanhedrin, aliwatambua kwa ukaidi wao wa uovu: "Enyi wenye shingo ngumu,msiotahiriwa mioyo wala masikio,siku zote mnampinga Roho Mtakatifu;na ninyi ni vivyo hivyo." (Matendo 7:51).

Paulo alipowahubiria Wayahudi huko Korintho, waliendelea kukaidi ujumbe wa wokovu kupitia Yesu Kristo. Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikaa nao katika sinagogi yao, lakini "wengine walikaidi,wakakataa kuamini,wakiitukana ile Njia, "(Matendo 19: 9). Baadaye Paulo mbele ya mkutano pamoja na wanafunzi na kuacha waasi wa habari njema katika ukaidi wao na kutokuamini.

Kibahati mbaya, hii ndiyo hatima ya wanaomkaidi Kristo kwa muda. Mungu hatimaye atawaangusha kwa ugumu wa mioyo yao na hawatamrudi tena.Kwa kusikitisha matokeo ya ugomvi huo wa kiburi unadhihirika wazi katika Warumi 2: 5: "Bali kwa kadiri ya ugumu wako,na kwa kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ya ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kuwa mkaidi / ukaidi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries