Swali
Je, Biblia inasema nini kuhusu unafiki?
Jibu
Kwa asili, "unafiki" unamaanisha kitendo cha kudai kuamini kitu lakini kutenda kwa namna tofauti. Neno la kibiblia linatokana na neno la Kiyunani kwa "mwigizaji" — hasa, "anayevaa kinyago" — kwa maneno mengine, mtu anayejifanya kuwa kile ambacho yeye hayuko.
Biblia inaita unafiki kuwa dhambi. Kuna aina mbili unafiki unaweza kuchukua: ule wa kutangaza imani katika kitu na kisha kutenda kwa namna kinyume na imani hiyo, na ule wa kudharau wengine wakati sisi wenyewe tuna dosari.
Nabii Isaya alihukumu unafiki wa siku yake: "Bwana akanena, 'Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana name, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa'"(Isaya 29:13). Karne baadaye, Yesu alinukuu mstari huu, akiwa na hukumu sawa na viongozi wa kidini wa siku Yake (Mathayo 15:8-9). Yohana Mbatizaji aliwaita watu wengi wanafiki waliokuja kwake kubatizwa "wazao wa nyoka" na wakawaonya wanafiki "toeni matunda yapatanayo na toba" (ona Luka 3:7-9). Yesu alichukua msimamo sawa thabiti dhidi ya utakatifu — Aliwaita wanafiki "mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo" (Mathayo 7:15), "makaburi yaliyopakwa chokaa" (Mathayo 23:27), "nyoka" na "wana wa majoka" (Mathayo 23:33).
Hatuwezi kusema tunampenda Mungu ikiwa hatupendi ndugu zetu (1 Yohana 2:9). Upendo lazima uwe "usio na unafiki" (Warumi 12:9). Mnafiki anaweza kuonekana mwenye haki nje, lakini ni sura ya kinafiki. Haki ya kweli hutoka kwa mabadiliko ya ndani ya Roho Mtakatifu sio ukubalifu wa nje kwa sharia zilizowekwa (Mathayo 23:5; 2 Wakorintho 3:8).
Yesu alizungumzia aina nyingine ya unafiki katika Mahubiri ya Mlimani: "Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako"(Mathayo 7:3-5). Yesu hafundishi dhidi ya utambuzi au kuwasaidia wengine kushinda dhambi; badala yake, Yeye anatuambia tusiwe wenye kujivuna na kushawishiwa na wema wetu wenyewe kwamba tunashutumu wengine kutokana na nafasi ya haki ya kujitegemea. Tunapaswa kujichunguza kwanza na kurekebisha mapungufu yetu wenyewe kabla tufuate "madoa" kwa wengine (tazama Warumi 2:1).
Wakati wa huduma ya Yesu duniani, alikuwa na mapambano mengi na viongozi wa kidini wa siku hiyo, Mafarisayo. Wanaume hawa walikuwa na ujuzi sana katika Maandiko na wenye raghba kuhusu kufuata kila herufi ya Sheria (Matendo 26:5). Hata hivyo, katika kutii herufi ya Sheria, walitafuta kwa bidii mwanya uliowaruhusu kukiuka roho ya Sheria. Pia, walionyesha kukosa huruma kwa wenzake na mara nyingi walikuwa wakionyesha kwa kiasi kikubwa kile kinachojulikana kuwa kiroho ili kukusanya sifa (Mathayo 23:5-7; Luka 18:11). Yesu alikanusha tabia zao bila shaka, akisema kuwa "haki, huruma, na uaminifu" ni muhimu zaidi kuliko kufuata ukamilifu kulingana na viwango vya makosa (Mathayo 23:23). Yesu aliweka wazi kuwa tatizo halikuwa kwa Sheria bali njia ambayo Mafarisayo waliitekeleza (Mathayo 23:2-3). Leo, neno la mafarisayo lina maana sawa na unafiki.
Ni lazima ieleweke kuwa unafiki sio sawa na kuchukua msimamo dhidi ya dhambi. Kwa mfano, sio unafiki kufundisha kuwa ulevi ni dhambi hata kama tumekuwa walevi. Wakristo hawatakuwa wakamilifu; tutaendelea kutenda dhambi. Sio unafiki kushindwa kuishi kulingana na viwango vya kibiblia, lakini ni unafiki kusema tunamwamini Mungu na tunataka kumtii Yeye na kisha tusijaribu kufanya hivyo. Inaweza kuwa unafiki kufundisha dhidi ya ulevi na wakati huo huo kuwa mlevi kila wikiendi. Pia itakuwa unafiki kufanya kana kwamba, kwa sababu ulevi sio dhambi ambayo tunapambana nayo, hatuhitaji neema ya Mungu sana kuliko wale ambao wako.
Kama watoto wa Mungu, tunaitwa kujitahidi kwa utakatifu (1 Petro 1:16). Tunapaswa 'kuchukia maovu' na 'kuambatana na lililo jema' (Warumi 12:9). Hatupaswi kamwe kuashiria kukubali dhambi, hasa katika maisha yetu wenyewe. Yote tunayofanya yanapaswa kuwa sawa na kile tunachoamini na wale tuko katika Kristo. Kuigiza kuliachiwa jukwaa, sio kwa maisha halisi.
English
Je, Biblia inasema nini kuhusu unafiki?