Swali
Biblia inasemaje kuhusu unajisi?
Jibu
Kuna maelezo ya suala la ubakaji katika Biblia. Inavyotarajiwa,Biblia inapoelezea uhalifu wa ubakaji, inadhihirisha kama kukiuka mpango mzima wa Mungu kwa ajili ya kuponya mwili wa mwanadamu (Mwanzo 34).Unajisi umekemewa popote unapotajwa katika Biblia.Mfano, kunacho kipengele maalumu katika sheria zilizopewa taifa la Israeli kabla ya kuingia katika Nchi ya Ahadi wakiongozwa na Yoshua. Kipengele hiki (Kumbukumbu la Torati 22: 13-29) lilionyesha moja kwa moja kulazimisha mwanamke kushiriki mapenzi kinyume na hiari yake, au kile kinachojulikana kama ubakaji. Hii amri ililenga kulinda wanawake na kulinda nchi ya Israeli dhidi ya matendo ya dhambi.
Kumbukumbu la Torati 22: 25-27 linatoa adhabu ya Sheria za Musa zinazohitajika kwa mtu ambaye alinajisi mwanamke kwa ahadi ya kumwoa. Mwanaume huyo alinyongwa kwa kupigwa mawe ilhali mwanamke alichukuliwa asiye na makosa.Hata kama wakati wa Musa torati ya Musa ililenga nchi ya Israeli, sharia ilikuwa wazi kwamba unajisi ni dhambi machoni pa Mungu na, pia katika torati,adhabu yake ilikuwa kali sana -kifo kwa mnajisi.
Baadhi ya vipengele Fulani vyenye ugumu katika Agano la Kale juu ya suala hili. Mwanzo ni Kumbukumbu la Torati 22: 28-29, "Mtu mume akimwona kijana aliye mwanamwali ambaye hajaposwa,akamshika na kulala naye,wakaonekana yule mtu mume aliyelala naye na ampe baba yake yule kijana shekel hamsini za fedha,kisha na awe mkewe,kwa kuwa amemtweza;hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote." Kama anayenajisiwa hakuwa ameahidiwa ndoa, mnajisi alipata adhabu mbadala.
Imelazimisha tuangalie Kumbukumbu la Torati 22: 28-29 kutumia kioo cha tamaduni za kale. Wanawake walitndewa vibaya katika enzi hizo,na mikusanyiko ya kijamii. Hawakuruhusiwa kuwa na utajiri. Walipata shida kujitegemea kwa kukosa kazi. Mwanamke asiye na baba, mume, au mtoto,alikosa ulinzi wa kisheria. Utumwa na uzinzi zikawa chaguo mbadala kwake.Kama mwanamke asiyeoelewa hakuwa bikira, ilikuwa ni shida sana yeye kuolewa. Kama hakuwa wa kuoleka, baba yake alikosa majumkumu juu yake.
Fedha nyingi na kuwajibika kimaisha ndiyo iliyokuwa adhabu ya Mungu juu ya anayenajisi bikira –na ililenga mnajisi kuwajibikia matendo yake kwa.Ilikuwa ni wajibu wake kumsaidia kwa maisha yake yote;kwa kuharibu maisha yake. Kwa kuwa hatuishi katika utamaduni huo waliokuwa,hii haiwezi kuwa nzuri kwa kisasi cha sasa. Katika 2 Samweli 13, Mfalme Amnon alibaka ndugu yake Tamari. Hata baada yaye kumkataa Tamar alimbembeleza amuoe (ndugu yake wa nusu!) kwa hofu na aibu ya kuwa bado hajaolewa.Absalomu, ndugu yake wa kweli alikasirika sana hata akamuua Amnon. Hivyo ndivyo ubikira kwa wanawake ulivyokuwa na dhmani.
Wanaotoa Biblia makosa pia wanafafanua Hesabu 31 (na vipengele sawia) jinsi Waisraeli waliidhinishwa kuchukua wafungwa wa kike kutoka kwa nchi walizopata ushindi. Kulingana na Wakosoaji hao hii ni baadhi ya kuendeleza au hata kutangaza ubakaji katika Bibilia.Kipengele hicho hakijadokeza chochote kuhusu kunajisi wanawake walioungwa. Si sawa kulenga kuwa wanawake waliofungwa walikuwa wa kunajisiwa. Watumishi wa watu waliambiwa wajitakase wenyewe na wafungwa wao (mstari wa 19). Unajisi ungekiuka agizo hili (tazama Mambo ya Walawi 15: 16-18). Wanawake waliochukuliwa kama wafungwa hawakutambulika kama vyombo vya ngono.Je,wafungwa wwaliruhusiwa kuoleka na Waisraeli? Ndio.Je!kuna dhihirisho kuwa unajisi ulikuwa wa kulazimishwa kwa wanawake?Kwa kweli.
Unajisi haujatajwa moja kwa moja, katika Agano Jipya ila katika utamaduni wa Kiyahudi wa nyakati hizo, unajisi ulichukuliwa kuwa uzinzi. ngono, Hata kutoa kama sababu za kuthibitisha talaka,Yesu na mitume walikemea uasherati wa ngono(Mathayo 5:32).
Fauka ya hayo, Agano Jipya linadhihirisha kuwa Wakristo wanafaa kutii sheria za viongozi wao (Warumi 13). Unajisi sio tu kwamba ni makosa ya kimaadili;bali pia ni kinyume na torati katika sehemu nyingi., Yeyote angetenda uhalifu huu basi angetarajia kulipia matokeo ikiwa ni pamoja na kutiwa mbaroni na kufungwa.
Tunapaswa kutoa huduma nyingi na huruma kwa waathirika wa unajisi.Bibilia inadokeza sehemu nyingi kuhusu kuwakaribia walio kwa mahali pagumu na wanahitaji msaada. Wakristo wanafaa kuwa mfano wa upendo na huruma ya Kristo kwa kusaidia manusura wa unajisi kwa uwezo wowote ule.
Pamoja na unajisi, watu wanapaswa kuwajibika na mabaya wanayoyatenda. Hakuna mtu aliye zaidi ya neema ya Mungu zaidi ya hayo, Mungu anaweza kuwaonyesha msamaha ikiwa watatubu na kuacha njia zao mbaya hata kwa wale ambao wametenda dhambi mbaya zaidi (1 Yohana 1: 9 Inaweza kutoa matumaini na njia ya maisha mapya lakini haijaondoa adhabu kulingana na sheria.
English
Biblia inasemaje kuhusu unajisi?