settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu upumbavu?

Jibu


Upumbavu ni matokeo ya mtu kutumia vibaya akili Mungu amempa. Mjinga hutumia ujuzi wake wa kufikiria kwa kufanya maamuzi mabaya. Aina ya msingi ya upumbavu ni kukataa kuwepo kwa Mungu au kusema Mungu "hayupo" (Zaburi 14: 1). Biblia inahusisha upumbavu na kukasiraka uepesi (Mithali 14: 16-17), kunena uongo (Methali 19: 1), na kutotii wazazi (Methali 15: 5). Tunazaliwa na upumbavu wa kawaida, lakini nidhamu itatusaidia kujifunza kwa hekima (Mithali 22:15).

Methali 19: 3 inasema kuwa upumbavu hauna maana: "Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake..." Yesu katika Marko 7:22 hutumia neno linamaanisha "upuuzi" na kutafsiriwa kuwa "upumbavu." Katika hali hiyo Yesu anaelezea kuwa chenye hutoka nje ya moyo wa mwanadamu ndicho humdhalilisha. Upumbavu ni mojawapo ya ushahidi kwamba mtu ana asili ya uchafu, ya dhambi. Methali 24: 9 inasema, "Fikira za mpumbavu ni dhambi..." Kwa hiyo, upumbavu ni kuvunja sheria ya Mungu, kwa kuwa dhambi ni uasi wa sharia (1 Yohana 3: 4).

Kwa mpumbavu, njia ya Mungu ni upuzi: "Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi..." (1 Wakorintho 1:18, tazama mstari wa 23). Injili inaonekana kuwa upumbavu kwa wasiookolewa kwa sababu haina maana kwao. Mpumbavu yuko nje kabisa ya hekima ya Mungu. Injili inakwenda kinyume na akili ya asili ya asiyeamini na hata hivyo, "... Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa" (1 Wakorintho 1:21).

Muumini katika Kristo anapokea asili ya Mungu (2 Petro 1: 4), ambayo inajumuisha mawazo ya Kristo (1 Wakorintho 2:16). Kwa kutegemea nguvu za Roho Mtakatifu, muumini anaweza kukataa upumbavu. Mawazo yake yanaweza kumpendeza Bwana, na anaweza kufanya maamuzi yanayomtukuza Mungu anapoimarisha maisha yake na maisha ya wale walio karibu naye (Wafilipi 4: 8-9, Waefeso 5: 18-6: 4).

Tunapokuja katika hatima yetu ya milele, mmoja aidha ni mpumbavu, maana yake anakataa injili ya Kristo, au mmoja ni wa hekima, maana yake anaamini katika Kristo na kumpa maisha yake (ona Mathayo 7: 24-27). Muumini anagundua kuwa injili-kile alichofikiri kuwa upumbavu-kwa kweli ni hekima ya Mungu inayompa wokovu wa milele.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu upumbavu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries