settings icon
share icon
Swali

Je! Tunapaswa kuvisoma vitabu vingine, au ni Biblia pekee?

Jibu


Biblia inafundisha kwamba tunapaswa kutafakari juu ya maneno ya Mungu (Zaburi 1:2-4). Pia inafundisha kwamba, "mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo" (Wafilipi 4:8). Kwa maneno mengine, vitabu vingine ambavyo vinavyohimiza maisha adilifu vinaweza kusaidia katika kutembea kwetu na Kristo. Vitabu maoni, masomo ya Biblia, fasihi za ibada-kunayo vitabu vingi ambavyo vinaweza kukuza uelewevu wetu wa Maandiko.

Fauka ya hayo, vitabu vingine vinaweza kusaidia sehemu nyingi za maisha mazoea. Kutoka kwa Habari za matibabu, hadi ukarabati wa magari, habari tunayohitaji kwa maisha ya kila siku inaweza kupatikana katika vitabu.

Tatu, hadithi zingine ni muhimu kwa ujifunzaji na kujitumbuisha. Ili mradi kitabu hicho kinamheshimu Bwana, riwaya inaweza kuwasilisha ukweli, kama vile Yesu alifanya katika mifano Yake. Wakorintho wa Kwanza 10:31 inafundisha, "Basi, lolote mfanyalo, kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu." Hiki ndicho kiwango cha muumini. Ikiwa kitabu fulani kinasomwa kwa utukufu wa Mungu, basi kunayo sababu halali ya kukisoma.

Nne, vitabu vingine vinaweza kutusaidia kuelewa vizuri na kuwafikia wale ambao hawamjui Kristo. Biblia ii wazi kuwa tumeitwa kutakawafanye mataifa yote wanafunzi (Mathayo 28: 18-20). Vitabu vinavyosaidia katika azimio hili vinaweza kujumuisha kuisoma lugha, uchambuzi wa kitamaduni, na hata kazi za dini zingine. Ingawa uangalifu mkubwa unastahili kwa kitengo hiki cha mwisho, ni muhimu kufahamiana na fasihi ya tamaduni zingine ili uweze kufanikish akimamilifu kuwasilisha ukweli wa Biblia.

Ingawa, kunazo vitabu vingine vya Kikristo ambavyo havistahili kusomwa. Kwa hakika, vitabu ambavyo, "vinavyoita uovu wema na wema kuwa uovu" (Isaya 5:20) vinastahili kuepukwa. Pia, vitabu vilivyo na maelezo ya anasa au umwagaji damu havina umuhimu, hasa ikiwa vinajumuisha michoro au picha za ngono. Vitabu kama hivyo ni sehemu ya "kazi ya giza isiyo na matuda" (Waefeso 5:11), ambayo Paulo anaita "aibu" (Waefeso 5:12).

Mwisho, inapaswa kuwa wazi kuwa Biblia ndicho kitabu muhimu zaidi na inapaswa kupewa kipaumbele cha juu sana kati ya Wakristo. Vitabu vingine vinaweza kuwa na faida na kuwa na ukweli, lakini ni Biblia tu ambayo ni "pumzi ya Mungu" na imevuviwa (2 Timotheo 3: 16-17). Wakati mwingine, Paulo alisihi maandishi mengine (Matendo 17) wakati wa kumwasilisha Kristo kwa wengine, lakini marejeo yake mengi ni kwa maandishi yaliyovuviwa ya Agano la Kale.

Tumeitwa kuichunguza Biblia: "Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtendakazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli (2 Timotheo 2:15). Hii inahitaji muda mwingi wa kuyasoma Maandiko.

Yesu anakuwa mfano mkuu kwetu. Wakati alijaribiwa, alijubu namna gani? Mara tatu alitumia Neno la Mungu (Mathayo 4:1-11). Vitabu vingine vinaweza kusaidia katika kutembea kwetu na Mungu, bali havipaswi kutuposha kutoka kwa kujitolea kwetu kusoma Neno la Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunapaswa kuvisoma vitabu vingine, au ni Biblia pekee?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries