settings icon
share icon
Swali

Ikiwa una madeni mengi, unaweza kuacha kutoa sehemu ya kumi wakati unalipa deni?

Jibu


Inaruhusiwa kuacha zaka wakati wa kulipa deni. Kulipa madeni ni wajibu; Kutoa sehemu ya kumi ni "chaguo" kwa sababu rahisi kwamba amri ya kutoa sehemu ya kumi ilikuwa sehemu ya Sheria ya Musa, na Wakristo hawako chini ya Sheria. Tafadhali usielewe vibaya-kutoa kwa kazi ya Bwana ni muhimu sana. Kutoa dhabihu ya kifedha ni sehemu ya wito wa Mungu kwa kila Mkristo. Ikiwa haiwezekani kulipa deni kwa kweli na kuendelea kutoa zaka/kutoa sadaka wakati huo huo, haiwezi kuwa makosa kupunguza kutoa au kuacha kutoa kabisa, kwa muda, ili kulipa madeni yanayodaiwa.

Wajibu wetu moja usiobadilishwa kuelekea watu wengine ni kwamba tunawapende, tuwashughulikie wao kama tunavyotaka watushughulikie sisi (Mathayo 7:12). Sisi sote tunataka watu kutulipe madeni tunayowadai. Kwa hivyo, kama Wakristo, tunapaswa "msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sharia. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria" (Warumi 13:8-10).

Sheria ya kutoa sehemu ya kumi ya Agano la Kale ilikuwa utoaji wa Mungu wa kukidhi mahitaji ya kimwili ya makuhani kutoka kabila la Lawi. Walihitaji msaada ili kuhudumu katika hekalu na kukidhi mahitaji ya masikini (Hesabu 18:26; Kumbukumbu la Torati 26:12-15). Kwa hivyo, wakati Waisraeli walipokosa kutoa zaka ya hekalu, Mungu alionya, "Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu"(Malaki 3:8).

Zaka ilikuwa ni sehemu ya kumi ya mapato ya mwanadamu: "Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri ya kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sharia, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahmu" (Waebrania 7:5). Ukuhani wa Kilawi uliendelea kuhudumu katika hekalu wakati wa maisha ya Yesu duniani, na zaka zilihitajika. Lakini baada ya kifo, ufufuo, na kupaa kwa Bwana Yesu, mambo yalibadilika: "Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sharia nayo ibadilike" (Waebrania 7:12). Kristo sasa ndiye Kuhani Mkuu wetu. Wakristo sasa ni hekalu la Mungu na ukuhani Wake wa kifalme (Waebrania 4:14-15, 1 Wakorintho 6:19-20, 1 Petro 2:9-10).

Kuhani Mkuu wetu anatumikia Agano Jipya kwetu (sheria ya Mungu iliyoandikwa kwa mioyo yetu) kwa kutupa Roho Mtakatifu (Waebrania 12:24; 10:16). Sheria hii inafanya kazi kwa uwezo, na kutufanya tuwapende wengine kwa upendo uliozalishwa na Roho (Wagalatia 5:22-23). Ndiyo sababu Yohana anaandika, "Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Munu wakaaje ndani ya huyo?" (1 Yohana 3:17-18). Upendo wa Mungu unalazimisha Mkristo wa kweli kutoa, lakini hakuna waraka wowote wa Agano Jipya unaamrisha au hata kupendekeza kwamba Wakristo kulipe zaka au asilimia nyingine yoyote. Kutoa kwa Kikristo ni matokeo ya upendo wa Kikristo.

Wakristo wanaweza, ikiwa watachagua, kutoa zaka (sehemu ya kumi) ya mapato yao kwa kanisa, kukidhi mahitaji ya kiroho na ya kimwili katika ulimwengu wao masikini. Wengine watachagua kutoa chini ya sehemu ya kumi; wengine watachagua kutoa zaidi. Paulo anapendekeza kutoa kwa kanisa siku ya Jumapili: "Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake" (1 Wakorintho 16:2a).

Wakristo hawapaswi kuweka akiba lakini kutoa kama vile Mungu anavyoongoza. Ni pesa za Mungu. Zawadi zake zinazidi gharama. "Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzunu, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema"(2 Wakorintho 9:6-8).

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ikiwa una madeni mengi, unaweza kuacha kutoa sehemu ya kumi wakati unalipa deni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries