settings icon
share icon
Swali

Ni dhambi gani kubwa zaidi?

Jibu


Hakuna dhambi kubwa zaidi kuliko dhambi nyingine katika muktadha wa milele. Dhambi zote hututenganisha na Mungu, na dhambi zote zinapaswa kusamehewa. Pia, hakuna "dhambi kubwa zaidi" kwa maana ya dhambi "za kufa" na "kunyima nafsi neema ya kiungu", kama vile Kanisa la Katoliki linavyofundisha. Dhambi zote ni za "mauti" dhambi hata kama ni moja humfanya mkosaji afaiwe kifo cha kiroho na kujitenga kwa milele kutoka kwa Mungu. Wakati huo huo, Biblia inasema kuwa siku ya hukumu dhambi zingine zitafaa adhabu kubwa zaidi kuliko wengine (Mathayo 11:22, 24; Luka 10:12, 14).

Yesu pia alisema dhambi moja kuwa ndiyo "dhambi kubwa zaidi" (ingawa sio "kubwa zaidi") katika Yohana 19:11. Akizungumza na Pontio Pilato, alisema kuwa yule aliyempeleka kwa Pilato alikuwa na hatia ya "dhambi kubwa." Alimaanisha kuwa hatia ya mtu aliyemtoa kwa Pilato, kama Yuda au Kayafa, alikuwa mkuu kuliko Pilato kwa sababu ya tendo la makusudi na la baridi la kumpeana Yesu baada ya kuona ushahidi mkubwa wa miujiza na mafundisho Yake, yote yakimtibitisha bila shaka kuwa Masihi na Mwana wa Mungu. Dhambi hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko ile ya wale wasiomjua Yeye. Hii inaweza kuonyesha kwamba wale ambao wamepewa ujuzi wa Yesu kama Mwana wa Mungu na bado wanamkataa watakuwa chini ya adhabu kubwa zaidi kuliko wale ambao bado hawamjui Yeye: "Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa" (Yohana 9:41).

Matukio haya, hata hivyo, haithibitishi kuwa dhambi moja ni "dhambi kubwa zaidi" kwa zingine zote. Mithali 6: 16-19 ni orodha ya dhambi saba Mungu huchukia na huwa chukizo kwake: "Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu." Lakini hakuna hata mmoja kati ya saba inajulikana kama dhambi kubwa zaidi kuliko nyingine yoyote, na hakuna yenye imtambuliwa kama dhambi kubwa zaidi.

Ingawa Biblia haitaji dhambi moja kama dhambi kubwa zaidi, bali inahusu dhambi isiyo na msamaha, ambayo ni dhambi ya kutoamini. Hakuna msamaha kwa mtu anayekufa kwa kutokuamini. Bibilia ii dhahiri kwamba, kwa upendo wake kwa wanadamu, Mungu alitoa njia za wokovu wa milele — Yesu Kristo na kifo chake msalabani — kwa "amwaminiye" (Yohana 3:16). Hali pekee ambayo msamaha hautapeanwi ni kuhusu wale wanaokataa njia pekee za wokovu. Yesu alisema, "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" (Yohana 14: 6), akifanya wazi kwamba Yeye na yeye peke yake ndiye njia ya kufika kwa Mungu na wokovu. Kukataa njia pekee ya wokovu haisamehewi na, kwa maana hiyo, ni dhambi kubwa zaidi ya zote.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni dhambi gani kubwa zaidi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries