settings icon
share icon
Swali

Elimu ya ufahamu/epistemolojia ni nini?

Jibu


Epistemolojia inahusika na tawi la falsafa inayohusisha asili na upeo wa maarifa. Inashughulikia maswali kama, “Maarifa ni nini?” “Maarifa hupatikana namna gani?” “Ni nini watu wanajua?” “Ni jinsi gani tunajua kile tunajua?” ”Ni kwa nini tunajua tunachokijua?”

Kwa kawaida epistemolojia imegawanywa katika vikundi viwili. Kwanza, maarifa ya mapendekezo, ambayo yanaweza kufikiriwa “maarifa ambayo” ni kinyume na “maarifa ya jinsi gani.” Katika hisabati, kwa mfano, ni maarifa kwamba 1+1=2, lakini pia kuna maarifa ya kuitatua hisabati. Epistemolojia ya pili ni maarifa ya kibinafsi. Ujuzi wa kibinafsi hupatikana kwa uzoefu. Kwa mfano, ujuzi wa kinadharia wa fizikia unaohusika katika kudumisha hali ya usawa wakati wa kuendesha baiskeli hauwezi kubadilishwa kwa ujuzi wa vitendo (wa kibinafsi) unaopatikana wakati wa kufanya mazoezi ya baiskeli.

Epistemolojia pia inahusika na kauli za imani. Maarifa hujumuisha imani, na kwa hivyo kauli ya mtu ya imani haiwezi kupingana na ujuzi wake. Kinyume chake, maarifa kuhusu imani sio lazima yawe na uthibitisho wa ukweli wake. Kwa mfano, “Mimi najua kuhusu dini ya Kiislamu, lakini sijaiamini,” ni kauli thabiti.

Imani inachukuliwa kuwa na upendeleo, huku ukweli unachukuliwa kuwa usio wa mapendeleo, usiotegemea imani au uzoefu wa mtu binafsi. Ingawa mtu anaweza “kuamini” kwamba mkanamungu yuu kweli, mwelekeo kama huu hausiani na ikiwa ukanamungu uu kweli. Ukweli unajisimamia wenyewe na unapita imani ya mtu na maoni kuhusu uhalisi.

Msingi wa epistemolojia ni gani? Sayansi na mantiki potovu, ambayo kwayo mtu anaweza kupata ujuzi, hudokeza kwamba ulimwengu uwe wa mantiki na utaratibu na kwamba unatii sheria za hisibati zinazo zile zile kila wakati na kila mahali. Hata kama ikiwa hali ni tofauti sana kila maeneo ya anga, zinaweza kuwa tofauti sana, hata hivyo kuna usawa wa kimsingi.

Mkristo-ambaye anaamini katika uhalisi wa kisababishi kinachopita maumbile-anatarajia kuwe ndio utaratibu katika anga. Tangu Biblia inafunza kwamba Mungu huvitetea vitu vyote (Waebrania 1:3), Mkristo anatarajia ulimwnegu utende kwa utaratibu na usawaziko. Kwa kuwa Mungu yuko kila mahali na ni yuko thabiti ndani yake, Mkristo anatarajia kwamba maeneo yote ya ulimwengu yatatii sheria zile zile, ingawa hali za kimwili za maeneo mbalimbali ya ulimwengu yaneweza kuwa tofauti.

Mungu anipita wakati (2 Petro 3:8). Kwa hivyo, ingawa hali za zamani zinaweza kuwa tofauti na zile za sasa, sheria za asili huzibidilishwi kiholela. Mkristo ana msingi wa kutegemeza dhana yake kwamba ulimwengu wote mzima unaimarishwa kwa njia yenye uthibiti, na kwa hiyo ana msingi wa kupata ujuzi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Elimu ya ufahamu/epistemolojia ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries