Swali
Je! Ni nini maana ya eskatolojia zinduzi?
Jibu
Eskatologia zinduzi ni mpango fulani wa eskatolojia-utafiti wa mambo ya siku za mwisho au nyakati za mwisho. Eskatolojia zinduzi kimsingi inasema kwamba ufalme wa Mungu, kama ulivyotabiriwa katika Isaya 35, ulianza wakati wa kuja kwa Yesu mara ya kwanza na sasa uko hapa, ingawa hautakuwa umekamilika kabisa mpaka kuja Kwake kwa mara ya pili. Eskatolojia zinduzi pia wakati mwingine hujulikana kama "eskatolojia inayojulikana kwa sehemu" na inahusishwa na dhana ya "ishakuwa lakini bado."
Kimsingi, eskatologia zinduzi ni imani kwamba tunaishi katika nyakati za mwisho (au siku za mwisho), ambazo zilizinduliwa katika maisha, kifo, na ufufuo wa Yesu. Pamoja na ufalme wa Mungu kuzinduliwa na Yesu, kanisa lina uwezo wa kufikia ahadi za ufalme hivi sasa. Kinyume na maoni haya ni eskatolojia ya wakati, ambayo inauona ufalme wa Mungu kawa tofauti, kipindi cha baadaye ambacho ahadi zilizotolewa kwa Israeli zitatimizwa hapa duniani. Wanaoshikilia dhana ya mgao wa Mungu wanashikilia kuwa kuna tofauti kati ya kanisa la Agano Jipya na Agano la Kale (na kipindi cha ufalme uchao) wa Israeli. Eskatolojia zinduzi huaribu kwa njia hiyo Ilizi.
Kulingana na teolojia zinduzi, ahadi zote za ufalme zinaweza kutimizwa ndani ya kanisa. Kwa mfano, Isaya 35:5 inafanya ahadi kwamba, katika ufalme, "Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa." Ahadi hizi zinaweza tangazwa hii leo, tusema waendelezi wa dhana ya "ushafika lakini bado" ikiwa tuna imani itaufanya ufalme "upenye" ulimwenguni. Wazo ni kuwa: Yesu ndiye Mfalme aliye enzini mbinguni, na Ufalme wake ushaanzishwa, kwa hivyo vipofu wanapaswa kuona na viziwi kusikia. Eskatolojia zinduzi ni maarufu katika makundi ya Ukristo sisimuzi, kwa sababu inatoa msingi wa kuitisha miujiza hii leo.
Kimaandiko, kuna hali ambayo tunaishi katika nyakati za mwisho kwa sababu kurudi kwake Kristo kumekaribia. Pia kuna hali ambayo ufalme unatumika tayari. Wakolosai 3:1 inasema kwamba "mmefufuliwa pamoja na Kristo," ingawa kwa kweli, hii haiwezi kuwa inazungumzia ufufuo wa kimwili bado. Paulo lazima anazungumza kiroho. Mojawapo ya tatizo la Eskatolojia iliyozinduliwa ni kwamba huwa inatafuta utimilifu wa sasa hivi na wa kimwili wa ahadi zilizotolewa kwa Israeli, wakati Yesu alisema wazi, "Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu" (Yohana 18:36).
Mapema katika huduma ya Yesu, yeye alisema kwamba ufalme wa Mungu "umekaribia" (Mathayo 4:17). Lakini Israeli walimkataa mfalme wao na kwa kufanya hivyo, waliukataa ufalme. Miaka ya ufalme kwa sasa "inangojea" huku Mungu akiifanyia kanisa kazi, ambayo inajumuisha Wayahudi na watu wa Mataifa. Mara tu wakati wa kanisa utakapomalizika, Mungu tena atazingatia Israeli kuwa kiini cha kazi yake duniani. Yesu atarudi, Israeli watampokea Masihi wao, na ufalme wa Mungu utakuja.
English
Je! Ni nini maana ya eskatolojia zinduzi?