Swali
Je! Falsafa ya kilimwengu/ falsafa ya wokovu ni ya Kibibilia?
Jibu
Falsafa ya kiulimwengu ni imani kuwa kila mtu ataokolewa. Kuna watu wengi wanashikilia kwamba wokovu wa kifalsafa na kuamini kuwa watu wote hatimaya huishia mbinguni. Ingawaje ni wazo la wanaume na wanawake wanaishi maisha ya mateso ya milele huko jahannamu ambayo yawafanya wengine kukataa mafunzo ya maandiko juu ya hii hoja. Kwa wengini ni kutia msizitizo sana kwa upendo na huruma za Mungu- na kuibusilia mbali utakatifu na haki ya Mungu- ambayo yawaongoza kuamini kuwa Mungu atakuwa na huruma kwa kila nafsi. Lakini maandiko hayafunzi kuwa watu wengine wataishi maisha yao jahannamu.
La kwanza kabisa kwa yote, Bibilia ii wazi kuwa wasio kombolewa watakaa milele jahannamu. Maneno ya Yesu mwenye yanathibitisha kuwa muda uliotumika mbinguni kwa walio kombolewa utakua sawa na ule wa wasio kombolewa watakuwa jahannamu. Mathayo 25:46 yasema, “Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” Kulingana na ayah hii, adhabu wale ambao hawakombolewa ni ya mile vile maisha ya watakatifu ni ya milele. Wengine wanaamini kuwa wale walio jahannamu hatimaye wataangamizwa na wasiwe hai tena, lakini Mungu mwenyewe anathibitisha hiyo itakuwa ya milele. Mathayo 25:41 na Mariko 9:44 yaelezea jahannamu kuwa “moto wa milele” na “usioweza kuzimika.”
Mtu anaweza kuepukaje huu moto usio weza kuzimwa? Watu wengi wanaamini kuwa barabara zote-dini zote na imani zote- zaelekea mbinguni, au wanachukulia kuwa Mungu ni mwingi wa upendo na huruma kwamba atawaruhusu watu wote waingie mbinguni. Naam Mungu ni mwingi wa upendo na huruma; ni tabia hii ambayo ilimfanya Mungu akamtuma Mwanawe, Yesu Kristo, duniani kufa msalabani kwa ajili yetu. Yesu Kristo ndiye mlango wa peke unaotuelekeza mbinguni ambao tutakaa milele. Matendo ya Mitume 4:12 yasema, “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu Mungu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu” (1 Timotheo 2:5). Katika Yohana 14:6, Yesu anasema, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Yohana 3:16, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Ikiwa tutaamua kumkataa Mwana wa Mungu, hatutimizi itupasayo kuokolewa (Yohana 3:16, 18,36).
Aya kama hizi, inakuwa wazi kwamba falsafa ya kiulimwengu na falsafa ya wokovu zote sio imani za Kibibilia. Falsafa ya kiulimwengu yahitilafiana na chenye maandiko yafunza. Huku ikiwa watu wengi wanawalaumu Wakristo kwa kuwa wakarimu na “kuwa kando,” ni muimu kukumbuka kuwa haya ni maneno ya Kristo mwenyewe. Wakristo hawakuanzisha hoja hizi wao wenyewe; Wakristo wataja tu peke chenye Bwana amekwisha sema. Watu wanaamua kuukataa ujumbe huu kwa sababu hawataki kukabiliana na dhambi zao na kukubali kuwa wanamwihitaji Bwana awaokoe. Kusema kuwa wale wanaokataa nafasi ya Mungu amepeana kwa wokovu kupitia kwa Mwanake wataokolewa itakuwa kuudunisha utakatifu na haki ya Mungu na kubuuza haja ya Yesu kutolewa kama dhabihu kwa niaba yetu.
English
Je! Falsafa ya kilimwengu/ falsafa ya wokovu ni ya Kibibilia?