Swali
Ina maana gani kuwa sehemu ya familia ya Mungu?
Jibu
Biblia inafundisha kwamba Yesu Kristo na Baba ni Mmoja (Yohana 1: 1-4), na kwamba pia ni Mwana wa pekee wa Mungu (Waebrania 1: 1-4). Neno hili la familia linaonyesha Mungu anamwona Yesu kama mwanachama wa familia. Waumini wanaozaliwa tena wanaambiwa kuwa sisi, pia, ni wajumbe wa familia hii (Warumi 9: 8; 1 Yohana 3: 1-2). Tunawezaje kuwa sehemu ya familia hii ya Mungu? Tunapopata injili, tukikiri dhambi zetu, na kuweka imani yetu na kumtegemea Yesu Kristo, katika wakati huo tumezaliwa katika ufalme wa Mungu kama watoto Wake na kuwa warithi pamoja Naye milele (Waroma 8: 14-17).
Wakati Yesu Kristo anajulikana kama Mwana wa pekee wa Mungu, waumini hujulikana kama watoto waliozaliwa katika familia ya Mungu ambao wanahitaji kukua na kukomaa katika imani yetu (Waefeso 4: 11-16), na kama wana na warithi wanaokubaliwa katika familia yake (Wagalatia 4: 4-7). Neema na huruma ya Mungu sisiyo na kikomo zimefunuliwa katika Waefeso 1: 5-6, ambayo inasema Anawaokoa wenye dhambi, ambao "Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa."
Kama watoto wa Mungu, tunapata nini? Hakuna kitu kingine mbali na ufalme wa Mungu (Mathayo 25:34, 1 Wathesalonike 2:12; Waebrania 12:28)! Waefeso 1: 3 inatuambia kwamba waamini wanabarikiwa na kila baraka za kiroho katika ulimwengu wa mbingu katika Kristo. Baraka hizi za kiroho hazina kikomo, ni za milele, na kukaa ndani ya Kristo, na kwa neema ya Mungu tumepewa baraka hizi kama watoto Wake. Kama watoto wa kidunia hatimaye tunamiliki kile ambacho wazazi wetu wanaacha nyuma baada ya kifo chao. Lakini kwa Mungu waumini tayari wanavuna matunda ya urithi wetu kwa kuwa na amani naye kwa njia ya dhabihu ya Mwanawe msalabani. Tuzo nyingine za urithi wetu ni pamoja na zawadi ya kuishi kwa Roho Mtakatifu wakati tunapoamini katika Kristo (Waefeso 1: 13-14), ambayo inatuwezesha kuishi kumuishia Yeye kwa sasa, na kujua kuwa wokovu wetu uu salama milele (Waebrania 7: 24-25).
Kuwa sehemu ya familia ya Mungu ni baraka kubwa zaidi iliyotolewa kwa waumini na ambayo inapaswa kutusukuma kupiga magoti katika ibada kwa unyenyekevu. Hatuwezi kamwe kufanya chochote ili tustahili kwa hiyo ni zawadi yake ya upendo, huruma, na neema kwetu, hata hivyo, tunaitwa kuwa wana na binti wa Mungu aliye hai (Warumi 9: 25-26). Sote tunaweza kuitikia kwa imani mwaliko wake!
English
Ina maana gani kuwa sehemu ya familia ya Mungu?