Swali
Je! Kufidia kosa ni nini?
Jibu
Neno "kufidia" halionekani katika Agano Jipya, lakini Agano Jipya huwa inaelezea kikamilifu kipengee/sehemu ya dhabihu ya Kristo kwa ajili yetu. Kufidia inamaanisha "kufunika dhambi" na/au "kutakaza dhambi." Fidia inaangazia dhana kwamba madhara na ushushaji hadhi wa dhambi umeondolewa kupitia kwa neema ya Mungu. Neno linguine la fidia ni upatanisho, na hakika hii ndio mojawapo ya matokeo ya kifo fidia cha Yesu kwa ajili yetu.
Kwa njia ya fidia- kazi ya Kristo msalabani kwa ajili yetu — dhambi ya wale wote ambao watakaomwamini imefutwa. Kufutwa huko ni kwa milele katika matokeo yake, ingawa dhambi bado ingalipo kwa muda tu. Kwa maneno mengine, waumini wamekombolewa kutoka kwa adhabu ya dhambi. Hili nit endo la mara moja ambalo mwenye dhambi amehesabiwa haki na kufanywa mtakatifu machoni pa Mungu ambaye alibadilishana hali yetu ya dhambi na haki ya Kristo msalabani (2 Wakorintho 5:21). Utakaso ni mchakato unaoendelea ambapo waumini wamekombolewa kutoka kwa nguvu za dhambi katika maishani mwao na sasa wanawezeshwa na hali mpya kuzuia dhambi na kugeuka kutoka kwayo. Kutukuka ni wakati tumeondolewa kutoka kwa hali dhambi, ambako kutafanyika pindi tu tunapotoka ulimwengu huu na tukiwa tumefika mbinguni. Michakato hii yote-kuhalalishwa, kutakazwa na kutukuka-zinawezekana kupitia kwa fidia na kufutiliwa mbali kwa dhambi.
Ni vyema kutambua kuwa kunayo faida za kifo cha Yesu kwa ajili yetu. Mojawapo ambayo haijajumlishwa katika dhana ya fidia, lakini kama ya kweli na ya kibiblia, ni kuridhisha, ambayo ni "kutuliza ghadhabu." Kwa kweli kifo fidia cha Mungu Mwana kinaridhisha ghadhabu ya Mungu Baba dhidi ya uasi, uanadamu wenye dhambi (Yohana 3:36; Warumi 5:9). Fidia, kuhesabiwa haki, utakaso, kutukuka, uridhisho, na zingine nyingi-tunazo wingi wa sababu sisizohesabika za kumtukuza Mung una kukimbilia kwa uaminifu na imani.
English
Je! Kufidia kosa ni nini?