Swali
Gharika ya wakati wa nuu ilikuwa ya ulimwengu mzima au sehemu moja?
Jibu
Ufahamu wa Kibibilia kuhusu gharika waufanya wazi kwamba ilikuwa ya ulimwengu mzima. Mwanzo 7:11 yasema, “Siku zile chemichemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu madirisha ya mbinguni yakafunguka.” Mwanzo 1:6-7 na 2:6 zatuambia masingira kabla ya gharika yalikuwa tofauti kutoka yale tunayoyaona hii leo. Kwa msingi huu na maelezo mengine ya Kibibilia, ni bora kuwa na dhana kuwa kwa wakati mmoja ulimwengu ulikuwa umefunikwa kwa kivuli cha maji. Kivuli hiki kingekuwa cha mvuke, au pengine ungekuwa ukipaa angani, labda pengine kama uvumi wa zohali. Hii ni pamoja na safu ya maji katika chini ya ardhi, ambayo yameachiliwa kuja juu ya nchi (Mwanzo 2:6) ungechangia gharika ya ulimwengu.
Aya ya wazi kabisa yenye inaonyesha ikubwa wa gharika ni Mwanzo 7:19-23 kuhusu maji, “Maji yakapata nguvu juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa. Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja nay katika safina.
Katika ufahamu wa hapo jkuu, hatupati pekee "neno “wote” likitumika kila mara, lakini tunapata pia “milima yote mikuu iliyo chini ya mbingu ilifunikwa,” maji yakapaa na kufunika milima zaidi ya futi ishirini,”na “kila kiumbe chenye uhai katika nchi kilikufa.” Elezo hili wazi wazi laelezea gharika la ulimwengu mzima. Pia, kama gharika ingekuwa ya sehemu moja, ni kwa nini Mungu alimwambia Nuhu ajenge safina badala ya kumwambia Nuhu asonge na awafanye wanyama nao pia wasonge? Na ni kwa nini alimwamuru Nuhu kujenga safina kubwa inayotosha aina yote ya wanyama wa nchi wanaopatikana katika nchi? Kama gharika haikuwa ya ulimwengu mzima, hakungekuwa na haja ya safina.
Petero pia anaelezea kiulimwengu juu ya gharika katika 2 Petero 3:6-7, ambapo anasema, “Kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.” Katika aya hizi Petero analinganisha “kiulimwengu” hukumu inayokuja na gharika ya wakati wa Nuhu na anasema kwamba dunia ya wakati ule iligharikishwa kwa maji. Zaidi, wengi wa waandishi wa Bibilia wilikubali historia ya gharika ya ulimwengu mzima (Isaya 54:9; 1 Petero 3:20; 2 Petero 2:5; Waebrania 11:7). Mwisho, Bwana Yesu Kristo aliamini kitika gharika ya kiulimwengu na akaichukua kama mfano wa ule uharibifu wa ulimwengu ujao wakati atakaporudi (Mathayo 24:37-39; Luka 17:26-27).
Kunayo dhibitisho nyingi za Kibibilia ambazo zinalenga pigo kubwa la kiulimwengu kama vile gharika ya ulimwengu mzima. Kunayo yale maganjo ya makaburi yanayopatikana kila bara na makaa ya mawe ambayo hayajachimbwa, na yanahitaji kufunikwa kwa haraka na majani. Yale makaa ya mawe yapatikanayo baharini pia yanapatika katika sehemu za juu za milima ulimwengu kote. Tamaduni katika sehemu zote za ulimwengu ziko na aina ya hekaya ya gharika. Hizi hoja zote na zingine nyingi ni thibitisho la kuwepo kwa gharika ya ulimwengu mzima.
English
Gharika ya wakati wa nuu ilikuwa ya ulimwengu mzima au sehemu moja?