settings icon
share icon
Swali

Je! Kauli ya Yesu kwa wanafunzi wake katika Luka 9:27 (ona pia Mathayo 16:28; Marko 9:1) haikuwa sahihi?

Jibu


Luka 9:27 inasema, "Amin, nawaambia, wako baadhi ya watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu." Angalia pia Mathayo 16:28 na Marko 9:1 kwa nukuu mfanano. Katika kila kitabu cha Injili, tukio linalofuata ahadi hii kutoka kwa Yesu ni mbadilisho. Badala ya kutafsiri ahadi ya Yesu kuwa inarejelea kurudi Kwake ili kuanzisha ufalme Wake duniani, muktadha unaonyesha kwamba Yesu alikuwa anarejelea kubadilika kwake. Neno la Kiyunani lilotafsiriwa "ufalame" pia linaweza tafsiriwa "utukufu wa ufalme," kumaanisha kuwa hao wanafunzi watatu waliosimama walimwona Kristo vile alivyo-Mfalme wa mbinguni- tukio lililotokea wakati wa ubadilisho.

"Kugeuka sura" kunarejelea tukio lililoelezewa katika vifungu vilivyonukuliwa hapo juu wakati Yesu alimchukua Petro, Yakobo, na Yohana kwenda juu ya mlima, ambapo alikutana na Musa na Eliya — wakiwakilisha Sheria na Manabii wa Agano la Kale — na alizungumza nao. Wanafunzi walimwona Yesu katika utukufu na ukuu wake wote, akiongea na Musa na Eliya waliotukuzwa. Huu ni mtazamo wa mara moja wa kile kitatokea katika ufalme wa Yesu. Wanafunzi walishikwa na butwaa wakati walimwona Yesu "walianguka chini kifudifudi" (Mathayo 17: 6).

Inaonekana kawaida kutafsiri ahadi hii katika Mathayo 16:28; Marko 9:1; na Luka 9:27 kuwa rejeleo kwa kugeuka kwake Yesu ambako "baadhi" ya wanafunzi walishuhudia hayo siku sita baadaye, kama vile Yesu alikuwa amekwisha tabiri. Katika kila Injili, kifungu kinachofuata baada ya ahadi hii kutoka kwa Yesu ni ugeuko, ambayo unamwonyesha Yesu katika utukufu wake wote ambao utaonekana tena katika Ufalme wa Mungu. Vifungu vya muktadha vinaifanya iwezekane kuwa hii ndio tafsiri sahihi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kauli ya Yesu kwa wanafunzi wake katika Luka 9:27 (ona pia Mathayo 16:28; Marko 9:1) haikuwa sahihi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries