settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa Mungu hataki mtu yeyote aangamie, bali wote waje katika toba (2 Petro 3:9)?

Jibu


Mara nyingi ni muhimu aya za Biblia katika muktadha wake, na hasa hii ni kweli na 2 Petro 3:9, ambayo inasoma, "Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama watu wengine wanavyokudhani kukawia. Badala yake, yeye anawavumilia ninyi, maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba." Sehemu nusu ya pili ya aya hii, "hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba," mara nyingi imetumika kupinga fundisho la unyakuzi.

Muktadha wa 2 Petro 3:9 ni elezo la wakejeli walitilia shaka kuwa Yesu hatarudi kuhukumu ulimwengu kwa moto (2 Petro 3:3-7). Wenye dharau hukejeli, "Hii itatoka wapi (aya ya 4). Katika aya ya 5-6 Petro anawakumbusha wasomi wake kuwa hapo mbeleni Mungu aliuangamiza ulimwengu na gharika katika wakati wa Noa. Katika aya ya 7, Petro anajulisha wasomi wake kuwa mbingu ya sasa na ulimwengu vitaharibiwa kwa moto. Petro pia anajibu swali ambalo alijua lilikuwa kwa akili za wasomi wake kuwa, "ni kipi kinamfanya Mungu kukawia?" katika aya ya 8, Petro anaambia wasomi kuwa Mungu yuu na anazidi kila dhana ya nyakati. Inaweza onekana kwamba tumekuwa tukingoja kwa muda mrefu, lakini kwa Mungu ni kufumba na kufumbua macho. Na katika aya ya 9, Petro anafafanua ni kwa nini Mungu amekawia (katika mtazamo wetu wa wakati). Ni huruma ya Mungu ambyo inajelewesha hukumu Yake. Mungu anangoja kuwapa watu wengi nafasi ya kutubu. Wakati huo huo, katika aya inayofuata ya 9, Petro anawahimiza wasomi wake kuishi maisha matakatifu wakitarajia kuwa siku moja Yesu atarudi.

Katika muktadha, 2 Petro 3:9 inasema kwamba Mungu anachelewesha kuja kwake na hukumu ili awape watu fursa zaid ya kutubu. Hakuna vile 2 Petro 3:9 inakanganya dhana kuwa Mungu ananyakua watu fulani kwa wokovu. Kwanza katika muktadha, unyakuzi sio kile haswa aya inasungumzia. Pili, kutafsiri "hataki mtu yeyote aangamie" kama "hawezi ruhusu mtu yeyote kuangamia" huelekeza katika fundisho potovu. Lakini Mungu "hawezi tamani" mtu yeyote kuangamia na bado kunyakua watu wengine kwa wokovu. Hakuna kitu chochote kisichofaa juu ya hilo. Mungu hakukusudia dhambi iingie ulimwenguni kupitia kwanguka kwa Adamu na Hawa, bali aliikubalia. Kwa kweli, ilikuwa sehemu ya mpango wake wa uungu. Mungu hakukusudia Mwanawe wa pekee kusalitiwa, kuteswa, na kunyongwa, bali alihirusu. Hii pia ilikuwa mpango kuu wa Mungu

Kwa njia hiyo hiyo, Mungu hakusudii mtu yeyote kuangamia. Bali anatamani wote waje katika toba. Kwa wakati huo, Mungu anatambua kuwa si kila mtu atakujÄ… katika toba. Ni jambo lisilopingika kuwa wengi wataangamia (Mathayo 7:13-14). Badala ya kuwa mkanganyiko wa 2 Petro 3:9, unyakuzi wa Mungu na kuwavuta baadhi kwa wokovu ni dhihirisho kuwa kwa hakika hata mtu yeyote aangamie. Isingalikuwa ni kwa sababu ya unyakuzi na wito wa Mungu, kila mtu angeangamia (Yohana 6:44; Warumi 8:29-30).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa Mungu hataki mtu yeyote aangamie, bali wote waje katika toba (2 Petro 3:9)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries