settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini maana ya huduma mara tano?

Jibu


Dhana ya huduma tano hutoka kwa Waefeso 4:11, "Ndiye aliweka wengine kuwa (1) mitume, wengine kuwa (2) manabii, wengine kuwa (3) wainjilisti, wengine kuwa kuwa (4) wachungaji na (5) walimu." Hasa kwa ajili ya aya hii, wengine wanaamini kuwa Mungu amesharejesha, au anarechesha, ofisi za mtume na nabii katika kanisa hii leo. Waefeso 4: 12-13 inatuambia kwamba madhumuni ya huduma hizi tano ni, "kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa 13mpaka sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua sana Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Kristo." Hivyo, kwa kuwa mwili wa Kristo hakika haujajengwa kufikia umoja katika imani na haujafikia kipimo chote cha utimilifu wa Kristo, kwa haraka mawazo hufikiria kuwa, ofisi za mtume na nabii lazima ziwe bado zinafanya kazi hii leo.

Walakini, Waefeso 2:20 inatuarifu kwamba kanisa "limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni." Ikiwa mitume na manabii walikuwa msingi wa kanisa, je! Bado tunaujenga msingi? Waebrania 6: 1-3 inatuhimiza tuendelea kutoka kwa msingi huo. Ingawa Yesu Kristo anafanya kazi kanisani hii leo, jukumu lake kama jiwe kuu la pembeni la kanisa lilikamilishwa na kifo chake, kuzikwa, kufufuka, na kupaa kwake mbinguni. Ikiwa kazi ya jiwe la pembeni, ii kwa namna hiyo imekamilika, basi ndivyo ilivyo kazi ya mitume na manabii, ambao walikuwa msingi, imekamilika.

Je! jukumu la mitume na manabii lilikuwa lini? Llikuwa ni la kutangaza ufunuo wa Mungu, kufundisha ukweli mpya ambao kanisa lilihitaji kukua na kustawi. Mitume na manabii walitimiza utume huu. Namna gani walitimiza? Kwa kutupa Neno la Mungu. Neno la Mungu ni ufunuo kamili wa Mungu. Biblia ina kila kitu ambacho kanisa linahitaji kujua ili likue, listawi, na litimize utume wa Mungu (2 Timotheo 3: 15-16). Kazi ya jiwe la pembeni ya mitume na manabii imekamilika. Kazi inayoendelea ya mitume na manabii hudhihirishwa katika Roho Mtakatifu akinena kupitia na kutufundisha Neno la Mungu. Kwa maana hiyo, huduma aina tano bado zinafanya kazi hii leo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini maana ya huduma mara tano?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries