Swali
Ni nini hufanyika baada ya kufa?
Jibu
Swali hili laweza kuwa na utata mwingi. Biblia haifafanui wazi wazi juu ya lini mtu atafika katika hatima yake ya milele. Biblia inatuambia ya kuwa baada ya mtu kufa, hupelekwa mbinguni au jehanamu kulengana na hoja ya kuwa alikuwa amemkubali ama kumkataa Kristo kama mwokozi. Kwa walioamini, kufa ni kuondoka katika mwili na kuenda kukaa na Bwana (wakorintho wa pili 5:6-8; wafilipi 1:23). Kwa wasioamini, kufa ina maana ya hukumu ya milele jehanamu (Luka 16:22-23).
Hapa ndipo kwenye utata juu ya ni nini hufanyika baada ya kifo. Ufunuo wa Yohana 20:11-15 inaeleza juu ya wale walio kuzimu wakitupwa katika ziwa la moto. Ufunuo wa Yohana 21 na 22 inazungumzia juu ya mbingu mpya na dunia mpya. Kwa hivyo ina maana ya kuwa mpaka wakati wa ufufuo wa mwisho, baada ya kufa mtu hubaki katika mahali Fulani kwenye mfano wa mbinguni na kuzimu. Mahali pa mtu anapofaa kukaa milele hapatabadilika ila makazi ya muda yatabadilika. Muda Fulani baada ya kufa, waumini watapelekwa katika mbingu mpya na nchi mpya (ufunuo wa Yohana 21:1) na wasioamini katika ziwa la moto (ufunuo wa Yohana 20:11-15). Haya ndiyo makao ya milele ya watu yanayotegemea kama mtu alimwamini Yesu Kristo pekee kwa wokovu kutokana na dhambi zake.
English
Ni nini hufanyika baada ya kufa?