Swali
Bibilia inasema nini kuhusu adhabu ya kifo?
Jibu
Sheria ya Agano La Kale iliruhusu adhabu ya kifo kwa matendo tofauti tofauti: Uuaji (Kutoka 21:1), utekaji nyara (Kutoka 21: 16), Ukatili (Kutoka 22: 19), uzinzi (Mambo Ya Walawi 20:10), usenge (Mambo Ya Walawi 20:13), kuwa nabii wa uongo (Kumbukumbu La Torati 13:5), ukahaba na ubakaji (Kumbukumbu La Torati 22: 4), na mendo mengine mengi maovu. Ingawa Mungu kira mara alionyesha huruma wakati adhabu ya kifo ilistahili. Daudi alifanya uzinzi, bali Mungu akutaka maisha yake yachukuliwe (2 Samueli 11:1-5, 14-17; 2 Samueli 12:13). Mwishowe, kila dhambi tuifanyayo inastahili adhabu ya kifo kwa sababu mshahara wa dhambi ni kifo (Warumi 6:23). Kwa shukrani nyingi, Mungu alionyesha upendo wake kwetu si kwa kutuhukumu (Warumi 5:8).
Wakati Mafarisayo walimleta mwanamke ambaye alipatikana akifanya uzinzi na wakamuuliza, ikawa atapigwa mawe hadi kifo, Yesu akasema, “Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe” (Yohana 8:7). Hii isitumike kuonyesha kuwa Yesu alikataa hukumu ya kifo katika matukio yote. Yesu hasa alikuwa akifunua utabeli wa Wafarisayo. Wafarisayo walitaka kumnasa Yesu kwa kuvunja sheria ya Agano La Kale; kwa kweli hawakutaka kujali kama mwanamke atapigwa mawe (palikuwa wapi yule mume aliyepatwa akifanya uzinzi naye?) Mungu ndiye aliyeanzisha adhabu ya kifo: “Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu” (Mwanzo 9:6). Mungu aliunga adhabu ya kifo katika matukio machache. Yesu pia alionyesha neema wakati adhabu ya kifo ilistahili (Yohana 8: 1-11). Mtume Paulo wazai wazi alitambua uwezo wa serikali kuweka adhabu ya kifo kwenye ilistahili (Warumi 13:1-7).
Mkristo anastahili kuichukulia adhabu ya kifo namna gani? Kwanza, lazima tukumbuke kuwa Mungu ndiye ameanzisha hukumu ya kifo katika ulimwengu wake; kwa hivyo, litakuwa jambo la kudhania kwetu kufikiria kuwa lazima tuanzishe adhabu ya juu/kali sana. Mungu ndiye ako na kiwango cha juu cha adhabu ya wastani kwa mwanadamu yeyote; Yeye ni mkamilifu. Kadri hii ya adhabu haitumiki kwetu peke hata kwake yeye mwenyewe. Kwa hivyo, Anapenda, upendo usio na mwisho, na ako na uhuru usio na mwisho. Tunaweza kuona kuwa ako na ghadhabu isiyo na mwisho na yote imetunzwa kwa kadri kamilifu.
Pili lazima tutambue kwamba Mungu ameipa serikali mamlaka ya kuamua wakati hukumu ya kifo inastahili (Mwanzo 9:6; Warumi 13:1-7). Litakuwa jambo lisilo la kibibilia kusema kwamba Mungu anapinga hukumu ya kifo katika mamna yote. Wakristo waziwai furahia wakati hukumu ya kifo inatumika, lakini kwa wakati huo, Wakristo wasipige vita haki ya serikali inapowahukumia kifo waalifu wa dhambi mbaya sana.
English
Bibilia inasema nini kuhusu adhabu ya kifo?