settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu ibada ya mababu?

Jibu


Kuabudu mababu kunahusisha dini inahusisha imani na mazoea ya dini yenye maombi na sadaka kwa roho za jamaa wao waliokufa. Kuabudu mababu hupatikana katika tamaduni nyingi ulimwenguni kote. Maombi na sadaka hufanywa kwa sababu inaaminkai kwamba roho za mababu huishi katika ulimwengu wa asili na hivyo zinaweza kuathiri hatima na bahati ya jamaa wanaoishi. Roho za mababu pia hujukuliwa kkama mpatanishi kati ya wanaoishi na Muumba.

Kifo hakikua kiigizo pekee cha kuamua kama utaabudiwa kama babu. Mtu huyo lazima awe alikuwa ameishi maisha ya kimaadili na tofauti kubwa katika jamii ili kufikia hali hiyo. Mababu wanaaminika kushawishi maisha ya vizazi vya baadaye kwa kuwabariki au kuwalaani, kwa kweli wanatumika kama miungu. Kwa hiyo wawaombee, kuwatunukia saka, na kutoa sadaka hufanyika ili kuwashawishi na kupata kibali chao.

Ushahidi wa ibada ya wazee umepatikana katika maeneo ya Mashariki ya Kati huko Yeriko unaoenda nyuma hadi karne ya 7 kabla ya Kristo. Ilikuwapo katika tamaduni za kale za Kigiriki na Kirumi pia. Kuabudu mababu umekuwa na ushawishi mkubwa zaidi juu ya dini za Kichina na Afrika na hupatikana katika dini za Kijapani na za Amerika ya asili ambapo inajulikana kama kuwaheshimu mababu.

Biblia inasemaje kuhusu ibada ya mababu? Kwanza, Biblia inatuambia kwamba roho za wafu zinakwenda mbinguni au Jahannamu na hazibaki katika ulimwengu wa asili (Luka 16: 20-31, 2 Wakorintho 5: 6-10; Waebrania 9:27, Ufunuo 20: 11-15). Imani kwamba roho huendelea kuishi duniani baada ya kifo na kuathiri maisha ya wengine sio ya kimaandiko.

Pili, hakuna mahali popote katika Biblia tumeambiwa kuwa wafu hufanya kazi kama wapatanishi kati ya Mungu na mwanadamu. Lakini tunaambiwa kwamba Yesu Kristo alipewa nafasi hiyo. Alizaliwa, aliishi maisha yasiyo na dhambi, alisulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu, alizikwa ndani ya kaburi, alifufuliwa na Mungu, ameonekana na mashahidi wengi, alipaa mbinguni, na anaishi sasa upande wa kulia wa Baba ambapo anaomba kwa niaba ya wale ambao wameweka imani yao na kumtegemea Yeye (Matendo 26:23; Warumi 1: 2-5; Waebrania 4:15, 1 Petro 1: 3-4). Kuna Mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu, na huyo ndiye Mwana wa Mungu, Yesu Kristo (1 Timotheo 2: 5-6; Waebrania 8: 6, 9:15, 12:24). Kristo pekee anaweza kuchukua jukumu hilo.

Biblia inatuambia katika Kutoka 20: 3-6 kwamba hatusitahili kuabudu mungu mwingine isipokuwa Bwana Mungu. Zaidi ya hayo, kwa kuwa waganga na wachawi walifikiriwa kuwa na uwezo wa kuwasiliana na wafu, pia walikataliwa waziwazi na Mungu (Kutoka 22:18, Mambo ya Walawi 19:32, 20: 6, 27, Kumbukumbu la Torati 18: 10-11; : 3; Yeremia 27: 9-10).

Shetani daima amejaribu kumshinda Mungu, na anatumia uongo juu ya kuabudu miungu mingine na hata mababu ili ajaribu kuwafukuza watu mbali na ukweli wa kuwepo kwa Mungu. Kuabudu mababu ni mbaya kwa sababu inakabiliana na maonyo ya Mungu juu ya ibada hiyo, na inatafuta kuchukua nafasi ya Yesu Kristo kama Mpatanishi wa Mungu kati ya Mungu na wanadamu.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu ibada ya mababu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries