Swali
Je! Ni kwa nini ibada ya ushirika ni muhimu?
Jibu
Maandiko yako wazi kuwa Yesu alilifia kanisa (Matendo 2028; Waefeso 5:25) na kwamba kanisa ni mwili Wake ((Warumi 12: 5; 1 Wakorintho 10:17; 12: 12-27; Waefeso 1: 23; 4:12; 5:30; Wakolosai 1:18, 24; Waebrania 13: 3). Kushiriki katika kanisa ni muhimu kwa afya ya kiroho ya Mkristo binafsi.
Kwa hivyo, je! ni kwa nini Wakristo wanapaswa kuhudhuria kanisa? Kwanza kabisa, kuhudhuria mikusanyiko ya ushirika ni agizo la kibiblia. Waebrania 10: 24-25 inatuambia tusiache kukutana pamoja. Ni muhimu kwamba wapokeaji wa barua hii walikuwa katika hali ya tishio la mateso. Kuhudhuria kanisa hadharani kungeweza kuwaweka katika hali ya kudhulumiwa. Amri hii inaonyesha kwamba faida za kuhudhuria kanisa huzidi uwezekano wowote wa tishio.
Maisha ya Kikristo hayakusudiwa yawe ya upweke. Sitiari zote za kibiblia kwa kanisa zinaonyesha uwingi, bali sio umoja: sisi ni mwili, kundi, jengo, na taifa takatifu. Katika Ukristo wa kibiblia hakuna "mbwa mwitu pweke"
Sababu ya pili ya kuhudhuria kanisa ni wingi wa baraka za kiroho tumewekewa. Kwa mfano, kuhudhuria kanisa kunakuza ushirika na kuhimizana. Katika kitabu cha Matendo, tunaambiwa kwamba wale walioamani katika siku za mwanzo "Nao wakawa wanadumu katika. . . ushirika" (Matendo 2:42). Kifungu cha Waebrania kilichotajwa hapo juu kinafunua kwamba moja wapo ya madhumuni ya kukusanyika pamoja ni "kuhimizana." Sisi sote tunahitaji kutiwa moyo. Ibada ya ushirika hutoa himizo kwetu. Kuhudhuria kanisa pia husaidia katika kuzuia kuanguka kutoka kwa imani na uasi. Bila kushiriki mara kwa mara katika ibada ya ushirika, mtu huyumbishwa kiroho.
Sababu nyingine ya kuwa na ibada ya ushirika ni ile kauli ya hadhara inafanya. Ikiwa sisi tunashiriki ibada mara kwa mara, tunaonyesha hadharani utiifu wetu kwa amri ya kumpenda Mungu. Kusema tunampenda Kristo huku tukipuuza mwili wake ni unafiki. Kuhudhuria kanisa mara kwa mara pia kunaonyesha uunguji wetu mkono kwa kazi ya Mungu ulimwenguni-kwamba tu upande wa Yesu badala ya kuwa kinyume naye (Mathayo 12:30).
Zaidi ya hayo, kuabudu Pamoja na wengine huleta faida ambazo hazipatikani katika ibada ya kibinafsi. Tunapohudhuria ibada ya pamoja, tunasikia kuhubiriwa kwa Neno la Mungu hadharani. Kugeukia huduma ya mitandao (kama vile redio au runiga au huduma inayopeperushwa mtandaoni) sio tu kunaondoa uharaka wa kuhubiri hadharani, lakini pia kunaweza kukuza hali ya ukapera, na kubinafsisha Ukristo. Kuhudhuria kanisani pia kunatuwezesha kushiriki Meza ya Bwana, tangazo la hadhara la mwili na damu ya Bwana Yesu (1 Wakorintho 11:26).
Yohana anatuambia kwamba tunajua kuwa tumetolewa toka kifo na kuletwa katika uzima kwa sababu tunawapenda kaka na dada zetu katika Kristo (1 Yohana 3:14). Kukusanyika pamoja kwa mafundisho, ibada, na himizo la pamoja ni ishara ya upendo kwa wale ambao wamekombolewa ni ishara ya kuokolewa kwetu kwa uzima wa milele.
English
Je! Ni kwa nini ibada ya ushirika ni muhimu?