settings icon
share icon
Swali

Ibada ya kweli ni nini?

Jibu


Mtume Paulo alieleza kikamilifu ibada ya kweli katika Warumi 12: 1-2: "Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya ungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu"

Kifungu hiki kina sifa zote za ibada ya kweli. Kwanza, kuna msukumo wa ibada: "huruma za Mungu." Huruma za Mungu ni kila kitu alichotupa ambacho hatukustahili: upendo wa milele, neema ya milele, Roho Mtakatifu, amani ya milele, furaha ya milele, imani ya kuokoa, faraja, nguvu, hekima, tumaini, uvumilivu, fadhili, heshima, utukufu, haki, usalama, uzima wa milele, msamaha, upatanisho, uthibitisho, utakaso, uhuru, maombezi na mengi zaidi. Ufahamu na uelewa wa zawadi hizi za ajabu hutuhamasisha kumwaga sifa na shukrani-kwa maneno mengine, ibada!

Pia katika kifungu hiki ni maelezo ya namna ya ibada yetu: "itoeni miili yanu iwe dhabihu iliyo hai na takatifu." Kuwasilisha miili yetu inamaanisha kutoa kwa Mungu sisi wenyewe. Marejeo ya miili yetu hapa inamaanisha hali yetu ya kibinadamu, ubinadamu wetu wote-mioyo yetu, fikra, mikono, mawazo, mtazamo-vinapaswa kuwasilishwa kwa Mungu. Kwa maneno mengine, tunapaswa kutoa udhibiti wa mambo haya na kuyapeleka kwake Yeye, kama vile dhabihu halisi ilitolewa kabisa kwa Mungu juu ya madhabahu. Lakini jinsi gani? Tena, kifungu hicho ni wazi: "kwa kufanywa upya nia zenu." Tunafanya upya akili zetu kila siku kwa kusafisha "hekima" ya ulimwengu na kuibadilisha na hekima ya kweli inayotoka kwa Mungu. Tunamwabudu Yeye kwa fikra zetu zilizofanywa upya na kusafishwa, si kwa hisia zetu. Hisia ni mambo ya ajabu, lakini isipokuwa yameumbwa na akili iliyojaa katika Kweli, zinaweza kuwa na uharibifu, nje ya nguvu za udhibiti. Ambapo akili inakwenda, ridhaa inafuata, na vivyo hivyo hisia ufanya. 1 Wakorintho 2:16 inatuambia sisi tuna "akili ya Kristo," sio hisia za Kristo.

Kuna njia moja tu ya kufanya upya akili zetu, na hiyo ni kwa Neno la Mungu. Ni ukweli, ujuzi wa Neno la Mungu, ambalo ni kusema ujuzi wa huruma za Mungu, na tukomerudi nyuma tulipoanzia. Kujua ukweli, kuamini ukweli, kushikilia imani juu ya ukweli, na kupenda ukweli kwa kawaida husababisha ibada ya kweli ya kiroho. Ni imani ikifuatiwa na upendo, upendo ambao ni jibu la kweli, sio msisitizo wowote wa nje, ikiwa ni pamoja na muziki. Muziki kama vile hauhusiani na ibada. Muziki hauwezi kuzalisha ibada, ingawa kwa hakika inaweza kuzalisha hisia. Muziki sio asili ya ibada, lakini inaweza kuwa uonyesho lake. Usitazame muziki ili kushawishi ibada yako; angalia muziki kama tu kujieleza kwa kile kinachosababishwa na moyo ambao umejaa huruma za Mungu, kutii amri zake.

Ibada ya kweli ni ibada ya Mungu. Watu huwa wanapatikana katika mahali ambapo wanapaswa kuabudu, ni muziki gani wanapaswa kuimba katika ibada, na jinsi ibada yao inavyoonekana kwa watu wengine. Kuzingatia vitu hivi hupoteza hoja. Yesu anatuambia kwamba waabudu wa kweli wataabudu Mungu kwa roho na kwa kweli (Yohana 4:24). Hii inamaanisha sisi tunaabudu kutoka moyoni na jinsi Mungu amejenga. Kuabudu kunaweza kujumuisha kuomba, kusoma Neno la Mungu kwa moyo wa wazi, kuimba, kushiriki katika ushirika, na kuwahudumia wengine. Sio kikwazo kwa kitendo kimoja, lakini inafanywa vizuri wakati moyo na mtazamo wa mtu ni mahali pazuri.

Ni muhimu pia kujua kwamba ibada imehifadhiwa tu kwa Mungu. Yeye pekee ndiye anastahili na sio watumishi Wake yeyote (Ufunuo 19:10). Hatupaswi kuabudu watakatifu, manabii, sanamu, malaika, miungu yoyote ya uwongo, au Maria, mama ya Yesu. Hatupaswi pia kuabudu kwa matarajio ya kitu fulani, kama vile uponyaji wa kimuujiza. Ibada ufanyika kwa Mungu-kwa sababu Yeye anastahili-na kwa radhaa Yake pekee. Ibada inaweza kuwa sifa ya umma kwa Mungu (Zaburi 22:22, 35:18) katika mazingira ya makanisa, ambapo tunaweza kutangaza kwa njia ya sala na kusifu ibada yetu na shukrani kwake na kile ametutendea. Ibada ya kweli inahisiwa ndani na kisha kuonyeshwa kupitia matendo yetu. "Kuabudu" bila ya wajibu haipendezi Mungu na ni bure kabisa. Anaweza kuona kupitia unafiki wote, na Yeye huchukia. Anaonyesha hili katika Amosi 5: 21-24 vile Anazungumzia hukumu inayokuja. Mfano mwingine ni hadithi ya Kaini na Abeli, wana wa kwanza wa Adamu na Hawa. Wote wawili walileta zawadi za sadaka kwa Bwana, lakini Mungu alifurahishwa tu na Abeli. Kaini alileta zawadi bila ya wajibu; Abeli alileta kondoo wake wazuri kutoka kondoo wake. Alileta kwa imani na kupendeza kwa Mungu.

Ibada ya kweli haijawekewa mipaka tu kwa kile tunachofanya kanisani au sifa za wazi (ingawa mambo haya yote ni mazuri, na tunaambiwa katika Biblia kuyafanya). Ibada ya kweli ni kukubalika kwa Mungu na nguvu zake zote na utukufu katika kila kitu tunachofanya. Aina ya juu ya sifa na ibada ni utii kwake na Neno Lake. Ili kufanya hivyo, lazima tujue Mungu; hatuwezi kukosa kumjua Yeye (Matendo 17:23). Kuabudu ni kumtukuza na kumsifu Mungu-kuonyesha uaminifu na kupendeza kwa Baba yetu.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ibada ya kweli ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries