settings icon
share icon
Swali

Imani hai katika 1 Petro 1:3 ni gani?

Jibu


Petro wa Kwanza 1:3 yasema, "Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu."

Mtume Petro anafungua waraka wake kwa maneno ya kumsifu Mungu Baba na Mwanawe Yesu Kristo, akikumbusha wasomi kuwa wokovu ni karama ya neema ya Mungu. Bado Petro anasema kuwa waumini wamepewa "tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu." Ni nini haswa Petro anamaanisha wakati anasungumzia juu ya "Imani iliyo hai"?

Petro anasimulia kwamba ni "uzao upya" ambao utatoa tumaini letu lilohai, ukihakikisha kuwa wokovu ni karama kutoka kwa Mungu. Kama vile mtoto mchanga hafanyi chochote ili azaliwe, tunapata kuzaliwa tena sio kwa sababu ya kuwa sisi ni nani au chochote tumefanya. Sisi ni uzao wa Mungu (Yohana 1:13) kupitia ufufuo wa Yesu kutoka wafu. Wokovu hutubadilisha kile tulivyo (2 Wakorintho 5:17), ukitufanya tufie dhambi na kuwa hai kwa haki ndani ya Kristo Yesu (Waefeso 2:5). Uzao huu upya hutupa sababu ya tumaini-hakikisho la wokovu.

Wafafanusi wa Biblia mara nyingi humwita Petro mtume wa tumaini. Katika kifungu hiki, Petro anaunganisha kuzaliwa kwetu kupya-wokovu wetu na dhana ya "tumaini lililo hai." Imani Petro anaizungumzia sio fikira tamanifu ambayo mara nyingi inahusishwa na neno tumaini hii leo. Tunaweza kusema, "natumai haitanyesha," au "natumai nitapita mtihani." Lakini hii sio aina ya tumaini ambayo Petro ako nayo.

Neno la Kigiriki kwa "tumaini" katika kifungu hiki linamaanisha "shauku, tumainifu jasiri." Tumaini hili la muumini haliko "hai" tu bali ni "kinjufu." Mbali na tumaini tupu, lililokufa la dunia hii, "imani hii iliyo hai" ni ya kutia nguvu, li hai, na tendaji katika moyo wa muumini. Ni tarajio na la kuendelea. Imani yetu iliyo hai hutoka kwa Mwokozi aliye hai na ambaye pia amefufuka. Imani hai ya Petro ni Yesu Kristo.

Mtume ananena na Wakristo ambao wanakabiliwa na mateso kule Asia ndogo. Maneno yake yalikusudiwa kuwahimiza/tia moyo katika mateso. Hatima yao ilikuwa salama kwa sababu ya ufufuo wa Yesu Kristo. Tumaini lao lilikuwa katika ushindi wa Wake juu ya kifo na ufufuo Wake. Mateso yoyote Wakristo wangekumbana nayo katika ulimwengu huu hayangelinganishwa na baraka ufufuo wa baadaye na maisha yajayo katika milele.

Imaini iliyo hai inategemea kale- Yesu alifufuka kutoka kwa wafu (Mathayo 28:6). Inaendelea katika wakati uliopo- Yesu yuu hai (Wakolosai 3:1). Na linavumilia hadi wakati ujao- Yesu anaahidi uzima wa milele, maisha yaliyofufuliwa (Yohana 3:16; 4:14; 5:24; warumi 6:22; 1 Wakorintho 15:23). Tumaini lililo hai pia hutuwezesha kuishi bila kufa moyo tunapokabiliana na mateso na majaribio katika maisha haya tunamoishi: "Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele (2 Wakorintho 4:16-18).

Kitu cha Imani yetu iliyo hai kinaelezewa katika 1 Petro 1:4 kama "urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu." Tuko na urithi ambao kamwe hautadhiriwa na kifo, kuchfuliwa na dhambi, au kunyauka wakati unapopita; una kinga ya kifo, kinga ya dhambi, na kinga ya umri. Urithi huu una kinga ya dosari kwa sababu Mungu anaulinda na kuutunza mbinguni kwa ajili yetu. Uu salama kabisa. Kamwe hakuna kitu kinaweza kudhoofisha hakika yetu urithi ujao.

Watu hawawezi ishi muda mrefu bila imani. Imani hutunenea katika hali ngumu na tukiwa na hofu ya kile kitatokea baadaye. Katika ulimwengu ulioanguka mahali ambapo watu wanakabiliana na umaskini, magonjwa, njaa, udhalimu, majanga, vita, na ugaidi, tunahitaji tumaini lilohai. Biblia inatuambia katika Waefeso 2:12 kuwa wale hawajampokea Kristo Yesu hawana tumaini. Waumini wamebarikiwa na tumaini la kweli na hakika kwa ufufuo wa Yesu Kristo. Kwa nguvu ya Neno la Mungu na kujazwa kwa Roho Mtakatifu, imani hii iliyo hai uepesisha akili na nafsi zetu (Waebrania 4:12). inabadilisha mawazo yetu, maneno na matendo yetu. Hapo awali tulikuwa wafu katika dhambi zetu, lakini sasa tu hai kwa imani ya ufufuo wetu wenyewe.

Imani hai ya muumini ii dhabiti na salama: "Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni. Yesu mwenyewe ametangulia kuingia humo kwa ajili yetu na amekuwa kuhani mkuu milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki" (Waebrania 6:19-20). Yesu Kristo ndiye Mwokozi, wokovu, na imani yetu iliyo hai.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Imani hai katika 1 Petro 1:3 ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries