settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inatufundisha kuwa na imani kama ya watoto?

Jibu


Bila shaka, imani ni kiini cha maisha ya Kikristo. Imani inahimizwa katika Biblia yote na inaonyeshwa kuwa ya lazima kabisa. Kwa kweli, "pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu" (Waebrania 11: 6). Sura nzima ya Waebrania 11 ni kuhusu imani na wale waliokuwa nayo. Imani ni zawadi kutoka kwa Mungu, kama tunavyoona katika Waefeso 2: 8-9, na sio kitu ambacho tunajiundia sisi wenyewe. Wakristo wote wamepokea zawadi ya imani kutoka kwa Mungu, na imani ni sehemu ya silaha za Mungu-ngao ambayo tunajikinga na "mishale ya moto ya mwovu" (Waefeso 6:16).

Biblia haituhimizi kamwe kuwa na imani "kama mtoto", angalau si kwa maneno mengi. Katika Mathayo 18: 3 Yesu anasema kwamba lazima tuwe "kama watoto wadogo" ndiposa tuingie katika ufalme wa Mungu. Kifungu cha maneno ya Yesu ni swali la wanafunzi, "Ni nani aliye mkuu zaidi katika ufalme wa mbinguni?" (Mstari wa 1). Kwa kujibu, Yesu "Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi" (mistari 2-5).

Kwa hiyo, wanafunzi walipozingatia kile kilichoashiria "ukuu" mbinguni, Yesu anatoa mtazamo mpya: njia "ya juu" ni "chini." Upole unahitajika (tazama Mathayo 5: 5). Yesu anawahimiza wanafunzi (na sisi) kutaka kuwa na unyenyekevu wa mtoto pamoja na imani yao. Wale ambao hupenda kwa hiari kuchukua nafasi ya chini kabisa wao ndio wakuu kwa mtazamo wa mbinguni. Mtoto mdogo hana tamaa, kiburi, na majivuno na hivyo ni mfano mzuri kwetu. Watoto ni wanyenyekevu na wenye kufundishwa. Hawana uwezo wa kujivunia au unafiki. Unyenyekevu ni wema unaopeanwa na Mungu; kama Yakobo anasema, "Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza" (Yakobo 4:10).

Ingawa imani haijatajwa katika Mathayo 18: 1-5, tunajua kwamba sio unyenyekevu tu unaomkaribisha mtu mbinguni; ni imani katika Mwana wa Mungu. Imani ya unyenyekevu na isiyojitokeza inaweza kuitwa "imani kama ya mtoto." Wakati Yesu alitaka kuwabariki watoto, alisema, "Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisaKweli nawaambieni, yeyote asiyepokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hataingia kamwe" (Marko 10: 14-15). Je, watoto hupokea zawadi namna gani? Kwa uwazi, uaminifu, na furaha isiyo na kifani. Aina hiyo ya uhalisi ya furaha lazima iwe ni alama ya imani yetu tunapopokea zawadi ya Mungu katika Kristo.

Bila shaka, kwa urahisi watoto hupotoshwa na kuongozwa. Katika kutojua kwao wao huwa hukosa ukweli na kuvutiwa na hadithi na minongono. Lakini hiyo sio maana ya kuwa na imani kama mtoto. Yesu alisisitiza imani ya unyenyekevu na uaminifu kwa Mungu, na alitumia kutokuwa na hatia kwa mtoto kama mfano. Kuhamasisha imani ya watoto, tunapaswa tu kumchukua Mungu katika Neno Lake. Kama watoto wanavyotumaini baba zao wa kidunia, tunapaswa kuamini kwamba "Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao" (Mathayo 7:11).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inatufundisha kuwa na imani kama ya watoto?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries