Swali
Kwa nini nizungumze kuhusu Imani yangu katika mahali pa kazi?
Jibu
Kama wafuasi wa Kristo, kuna sababu nyingi kwa nini tunapaswa kuwa na tamaa ya kushiriki Imani yetu katika hali zote. Hata hivyo, katika suala la mahali petu pa kazi kuna zingatio moja lingine. Kama wafanyakazi, tumefanya ahadi ya kujitolea kwa mwajiri wetu faida kamili ya huduma yetu kwa muda fulani. Kuwa shahidi mzuri wa Kikristo lazima kwanza tufuate kupitia ahadi hii. Jitihada za Kiinjilisti hazipaswi kuingiliana na majukumu tuliyoahidi kutimiza (1 Wathesalonike 5:12-14). Ikiwa watafanya, basi matendo yetu yatasaliti maneno yetu na uaminifu wa ushahidi wetu unapotea. Hivyo, tunapaswa kuwa na tamaa ya kuwa wafanyakazi bora mwajiri wetu ako nao (Wakolosai 3:23). Hii itatoa mamlaka fulani kwa maneno yetu baadaye wakati tunashiriki Imani yetu.
Miongoni mwa sababu mingi ya kushiriki Imani yetu ni masharti tatu:
1) Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo anaiamuru: Wakati wa nyakati Zake za mwisho duniani na wanafunzi Wake, Kristo angesema chochote. Kile alichagua kuwaambia ni kwamba wao wangeenda na Baraka na nguvu Zake kuhubiri Injili ili wengine wangekuja kujua nguvu ya kuokoa na uhusiano uliobarikiwa na Yesu Kristo (Mathayo 28:18-20).
2) Jukumu inahitaji. Tumekombolewa na Kristo, basi tumepewa kitu ambacho si chetu wenyewe. Bila neema ya Mungu tungepotea kwa milele yote. Bahati ni wengi wetu tunakuja kwa Imani na wokovu sababu mtu fulani alishiriki na sisi; jinsi gani basi hatuwezi kufanya sawa kwa wengine? Yesu alisema kwamba vile tumepokea bure, tunapaswa kupeana bure (Mathayo 10:8). Tumeaminika na Mungu kuwa wajumbe kwa waliopotea (Matendo 1:8; 1 Wathesalonike 2:4).
3) Shukrani inaichochea. Mtazamo wa shukrani za dhati ni moja ya vitu vingi ambazo zinafanya muumini wa kweli katika Yesu Kristo. Tunapochunguza Zaidi kwa uaminifu upotovu wa mioyo yetu, tunatambua zaidi jinsi msamaha ni kubwa sana ambao ulikuwa na umeendelezwa kwetu, na tunakuwa na shukrani zaidi kwa Mungu kwa kutukomboa. Hii shukrani inajionyesha yenyewe katika kumpa Yeye heshima kwa kile Yeye ametufanyia—kile ambacho hatuwezi kujifanyia wenyewe. Njia bora ya kumshukuru Mungu ni kumpa Yeye utukufu wote kwa kile ametufanyia na kuwaambia wengine juu ya upendo Wake mkubwa na huruma.
Jinsi gani tunaweza kushiriki Imani yetu katika mahali pa kazi? Kwanza, kuna ushuhuda "tulivu"—moja ambao unaongea kwa wingi bila maneno kabisa. Inahusisha kuwa mfanyakazi mtiifu na mwaminifu, sio kuwasema vibaya wajiri wetu au wafanyakazi wezetu. Hakuna mwenye anafanya kazi na bosi kamili au mwenzi kamili, lakini ikiwa tutafanya kazi na mtazamo uliotolewa katika Wakolosai 3:23, "Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu," tutaleta heshima kwa Mungu kwa kumfanyia vitu vyote Yeye, Bosi pekee kamili kweli. Wakati tunamfanyia kazi Bwana, uwezo wetu wa kushughulikia matatiso ya kikazi na kuwatendea wengine kwa unyenyekevu na uvumilivu kutatufanya wa pekee miongoni mwa wafanyakazi wezetu. Wakati wengine wanatambua mtazamo wetu, watatoa maoni kila wakati kuihusu, kutupa nafasi ya kueleza yule tunamtumikia hasa na jinsi ameathiri maisha yetu. Kwa maneno mengine, wakati mwingine tunahitaji "kutembea matembezi" ili kupata nafasi ya "kuongea maongezi."
Wakati milango inafunguka kushiriki Imani yetu, lazima "Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu" (1 Petro 3:15). Hii inamaanisha bidi kuhusu usomaji wetu wa Biblia katika kujitayarisha kwa milango hiyo iliyofunguka. Ikiwa "mtaruhusu neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote" (Wakolosai 3:16), mtakuwa tayari kila wakati. Hatimaye, omba kwa Mungu afungue nafasi ya kushiriki Kristo na wengine—zile "teuzi za kiuungu" na watu ambao mioyo yao imetayarishwa na Mungu kupokea ukweli Wake kutoka kwetu.
English
Kwa nini nizungumze kuhusu Imani yangu katika mahali pa kazi?