settings icon
share icon
Swali

Injili ya Barnaba ni nini?

Jibu


Ni muhimu sana kuwa tusichanganyishwe na Injili ya Barnaba [ca.AD 1500] na barua ya Barnaba [ca.70—90]. Waraka wa Barnaba uliandikwa mwisho wa karne ya 1, ila sio na yule Barnaba aliyetajwa katika agano jipya. Ingawa iko Zaidi ya mchanganyo wa injili na historia, waraka wa Barnaba haukuwahi tambulika kuwa maana na kanisa la kwanza ama shirika lolote la kanisa.

Kwa hivyo Injili ya Barnaba haina msingi wa uinjilisti na iliandikwa miaka 1400 baada ya wakati wa Barnaba. Hii inadhihirika na ukweli kuwa haikuwahi tajwa na baba mkuu wa kanisa lolote ama mwanahistoria wa kanisa lolote baada ya karne ya 16

Kwa upinzani, vitabu vya Agano Jipya vyote viliandikwa mapema [kabla ya AD100] na walioshuhudia, ama waliowahoji washuhuda wa Bwana Yesu Kristo [1 Yohana 1:1-5, Luka 1:1-4]. Vitabu vine vya injili vinavyopatikana katika Agano Jipya havikuwahi tiliwa shaka kwa ukweli wake.

Hata Injili ya Barnaba ingeandikwa wakati wa mitume, haingeweza kuwa na ule umuhimu wake kwa sababu ya makosa yaliyomo ya kihistoria na kisheria. Kwa mfano, Injili ya Barnaba inakisia kuwa Yesu hakudai kuwa mkombozi [tazama Mathayo 26:63-64]. Injili ya Barnaba pia inaangazia kuwa Yesu alizaliwa wakati Pilato alikuwa gavana [ila historia inaonyesha kuwa Pilato alikwa gavana mnano 26 ama 27 AD]

Zaidi ya hayo, Injili ya Barnaba inaweka mashirika yasiyo wazi, kwa kuwa inapendelewa na Waislamu maana inafundisha kuhusu Yesu sawasawa na Korani. Injili ya Barnaba inaangazia kuwa Kristo hakufa msalabani, jinsi ilivyo katika Korani kwenye Sura 4:157. Wanahistoria wanakubaliana kwa pamoja kuwa Injili ya Barnaba iliandikwa katika karne ya 15-16 AD, kuwa kiasi kikubwa pengine na Waislamu wanaotafuta namna ya kupinga Kristo jinsi anavyosimuliwa katika bibilia.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Injili ya Barnaba ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries