Swali
Injili ya Filipo ni nini?
Jibu
Sawia na injili ya Thomaso, Injili ya Filipo ni kusanyiko la mazungumzo kwa kiasi kikubwa ya Yesu. Injili ya Filipo inaangazia Zaidi "zaka ya ndoa" kama "tendo lililofiche". Injili ya Filipo haijaangaziwa kama iliandikwa na Filipo mtume wa Kristo. Imepewa kichwa "injili kulingana na Filipo" kwa sababu Filipo ndiye tu mtume wa Yesu aliyetajwa humo {73:8}
Andiko karibu lote la Injili ya Filipo lilipatikana kule maktaba ya Nag Hammadi Misri mwaka wa 1945. Imeandikwa katika lugha ya Kikoptic na kupewa tarehe karibu karne ya 4 kabla Kristo. Injili ya Filipo ni kusanyiko la matukio katika Injili, na inawakilisha kusanyiko ya maono ya Yesu na mafudisho yake. Wakati kunazo vifungo vichache katika Injili nya Filipo vinavyofanana na Injili nne katika bibilia, kusoma katika Injili ya Filipo itadhihirisha tofauti zinazodhihirika na pia utofauti uliopo kwenye maandishi kuhusu Yesu alikuwa nani na alikuja kufanya nini.
Jambo kuu katika Injili ya Filipo ni lile inayosema kuhusu uhusiano wa Yesu na Mary Mgdalene. katika kitabu chake maarufu cha THE DA VINCI CODE, mwandishi Dan Brown anaaangazia Injili ya Filipo kama kielezo kuwa Yesu alimwoa /alihusiana na mary Magdalene. Ila, Injili ya Filipo haijadokeza kuwa Yesu aliolewa na Mary Mgdalene. Haijaeleza aidha kuwa Yesu alihusika kimapenzi na Mary. Ile sehemu moja ambayo inahusikana na tukio hili imeharibiwa kabisa, na sehemu kubwa haisomeki. Haya ndiyo Injili ya Filipo inaelezea, kwa alama za"…"kumaanisha sehemu zinazokosa: na mpenzi wa…Mary Magdalene..zaidi…watumishi…kumbusu…kwake…na wanafunzi wengine…wakamwambia…mbona unampenda kutuliko sisi sote?" Hata tukachukulia kuwa Yesu alikuwa akimbusu Mary Magdalene, onyesho halijaonyesha lolote ila uhusiano wa kirafiki. mwanamme ambaye hajaoa kumbusu mwanamke amabaye hajaolewa katika uso, hata kama sio kawaida katika kizazi hicho, bila shaka sio kielelezo kuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Zaidi ya hayo yote, hata ingawa injili ya Filipo ilielezea kuwa Yesu aliolewa na Maria Magdlene, hiyo haingeweka hilo wazo kuwa kweli. injili ya Filipo haikuandikwa na Filipo mtume ama yeyote aliyekuwa amekutana na Yesu. Andiko halisi la Injili ya Filipo imekisiwa kuwa tarehe ya karne ya 3 ikiwa mapema, kama miaka 200 kabla ya kifo cha Yesu. Umuhimu wa kipekee wa kuisoma Injili ya Filipo ni kujifunza kwamba kulikuwa na kudanya kwingi katika karine za kwanza za kanisa la kristo.
English
Injili ya Filipo ni nini?