settings icon
share icon
Swali

Injili ya Petroni nini?

Jibu


Injili ya Petroina mchanganyiko wa kazi ya injili inayo kiziwa kuandikwa na Petroila inatoa mtazamo usio wa kweli kuhusu Yesu Kristo. Injili ya Petroina vifungu 60 na inahusika na matendo na matukio yanayozunguka hatima ya maisha ya Yesu Kristo. Nakala halisi inafikiriwa kuwa iliandikwa mnamo c. AD 150, ila dondoo la mwanzo wa maandishi hayo yaliandikwa mnamo karne ya 8 ama 9.

Kutajwa kwa mara ya kwanza kwa injili ya Petroilitendeka na Askofu Serapion wa Antiokia [c. AD200] katika waraka mada yake ikiwa "kuhusu yale yanayojulikana kama injili ya Petero." Katika barua hiyo Serapion akatoa wasia kwa viongozi wa kanisa wasije wakasoma hiyo injili kwa waumini wao kwa maana ilikuwa na upungufu wa injili. Pia alikemea injili ya Petrokama isiyo ya kweli na ya kubuni.

Docetism ni nini? Tukio moja la Docetism [Marcionism] inasisitiza kuwa Kristo alikuwa wa kiroho na takatifu sana na hangeweza kuwa binadamu. Alionekana tu kuwa na nyama na damu, mwili wake mtakatifu ukiwa hauonekani. Mashirika mengine yalishikilia kuwa, wakati Yesu alikuwa mwanadamu, Kristo alikuwa kiumbe mwingine kando aliyeingia katika mwili wa Yesu kwa mfano wa njiwa wakati wa ubatizo wake, ikimpea nguvu ya kufanya miujiza. Utambulisho wake kama kristo ulimpeleka msalabani. Docetism ilikataliwa katika kikao cha kwanza cha Nicaea kabla 325AD na kuchukuliwa kuwa ya maana na wakatoliki na wapinzani wao. Docetism pakubwa ilitupiliwa mbali katika karne ya kwanza.

Injili ya Petroinanakiri kuwa pale msalabani Yesu alilia, "Nguvu zangu,nguvu zangu ,mbona umeniacha," badala ya "Mungu wangu,Mungu wangu,mbona umeniacha?" [Mariko 15:34]. Na katika kusulubiwa,Injili ya Petrokimakusudi haijataja kuwa Yesu alikufa, na kusema badala yake kuwa "alitwaliwa mbinguni." Hili wazo la kuepuka kifo kamili cha kinadhihirika katika Korani, Sura 4:157-158: Ila Allah akamchukua kwake." Injili ya Petroinaashiriria kuwa Kristo "alitwaliwa"kwenda kwa uwepo wa kipekee punde tu nguvu zake za kipekee zilipomtoka mwili wake wa kibinadamu, ambao ulikuwa tu makazi yake kwa muda mfupi. Haya mafundisho, pamoja na misemo kuwa Yesu "alibakia kimya, kama amabaye hakuhisi uchungu" pale msalabani, inanakiri makosa ya Docetism.

Namna nyingine Injili ya Petroinakinzana na zile za Mathayo, Mariko, Luka na Yohana ni maelezo kuhusu matukio baada ya mwili wa Yesu kulazwa kaburi. Injili ya Petroinazungumzia kuwa walinzi "waliona mbingu zikifunguka, na wanaume wawili wanateremka na mwanga mwingi na kuelekea kwenye kaburi……Tena wanaona wanaume watatu wakitoka kwenye kaburi, na wawili walikuwa wakimshikilia mmoja,na msalaba ukiwa unawafuata. Na vichwa vya hao wawili vikafikia mbingu, ila kichwa cha yule aliyekuwa kaelekezwa kikazidi kikapita mbingu. Na kisha wakasikia sauti kutoka mbinguni, ikisema, "umewahubiria wale waliolala".Na jibu likasikika kutoka kwa msalaba, "ndio". Haya maandishi yanaegemea mikusanyiko ya injili.

Haya ni baadhi ya mapungufu yaliyokuwa kwenye injili ya Petero:

Kusulubishwa kunafanyika kule Roma, na si Yerusalemu.

Yusufu wa Arimathea anatajwa kuwa rafiki wa karibu wa Pontio Pilato.

Pontio Pilato ananyanganywa majukumu yote. Herode Antipa anachukua usukani, na kufanya majukumu ambayo, kulingana na injili ya Luka Herode alikataa kuyakubali.

Yesu "anatwaliwa" kutoka msalabani na kifo chake hakijatajwa popote.

Viumbe wawili wasiotambulika wanaingia kwenye kaburi na, watatu wanatokea.

Msalaba unaelezewa kuwa unaoegelea kutoka kaburini na kusema "ndiyo" kuitikia suti itokayo mbinguni.

Hakujatajwa washuhuda waanaomwona Yesu akiwa hai baada ya kutolewa kaburini.

Na kama hayo hayajatosha kuweka kutoaminika kwa ukweli wa Injili ya Petro, pia tunao ushuhuda wa Eusebius. Mwanahistoria alifanya ufafanuzi katika Injili ya Petrokatika maandishi yake na kusema kuwa Apollo hapo awali alikuwa sanamu ilivyotajwa katika injili ya Petero, na sio Yesu Kristo. Eusebius alisema kuwa jina la Yesu Kristo liliandikwa juu ya jina la APollo.

Injili ya Petro inakinzana na vitabu vingine vya injili katika baadhi ya sehemu muhimu,pamoja na kifo cha kimwili na kufufuka kwa Mkombozi wetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Injili ya Petroni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries