Swali
Je! Injili ya Q ni gani? Je! Kunayo ushahidi wowote wa Injili ya Q?
Jibu
Injili ya "Q" inapata kichwa chake kutokana na neno la Kijerumani la quelle ambalo linamaanisha "chanzo." Wazo lote la injili ya Q msingi wake uu katika dhana kuwa vidokezo vya Injili za (Mathayo, Marko, na Luka) vinakaribiana kiasi kwamba huenda walipashana habari/au chanzo kimoja. Hiki chanzo kingine kimepewa jina "Q." hoja maarufu sana ya kuwepo kwa injili ya Q ni hii: (1) Injili za Mathayo, Marko, na Luka ziliandikwa baada ya AD 70 na kwa hivyo hazingeweza kuandikwa na Mitume Mathayo, Yohana Marko, au daktari Luka. (2) Tangu waandishi wa Injili hawakuwa washuhudiaji wa kwanza, lazima walitumia vianzo vingine, (3) Tangu Marko ndio Injili fupi na ina nyenzo ya asili, Marko ndio iliandikwa ya kwanza na Mathayo Pamoja na Luka walitumia Marko kama chanzo. (4) Kwa kuwa kuna mfanono kati ya Mathayo na Luka ambao hauonekani katika Luka, Mathayo na Luka huenda walitumia chanzo kingine. (5) Chanzo hiki, Q, kilikuwa mkusanyiko wa maneno ya Yesu, kama yale ya Injili ya Tomaso.
Wakati wa kuzingatia uwezekano wa injili ya Q, in muhimu kukumbuka kuwa hakuna Ushahidi kamwe umewai patikana wa kuwepo kwa injili ya Q. Hakuna hata kipande kimoja cha hati ya Q kimewai patikana. Hakuna baba wa kanisa la kwanza aliwai taja chochote chenye kingeweza kuwa injili ya Q. Pili, kunao Ushahidi wa kutosha kuwa Injili ya Mathayo, Marko, na Luka ziliandikwa kati yam waka wa AD 50 na 65, na sio baada ya AD 70. Wengi wa baba wa kanisa la kwanza huchukulia kuwa Mitume Mathayo, Yohana Marko, na Luka daktari ndio waliziandika. Tatu, kwa kuwa Injili ziliandikwa na Mathayo, Marko, na Luka, ziliandikwa na washuhudiaji wa Yesu Kristo/au marafiki wa karibu wa wale waliomshuhudia Yesu. Kwa hivyo, ni kiasili kuwa lazima tutarajie mfanano. Ikiwa injili inanakili maneno yale yale yaliyozungumzwa na Yesu, lazima tutarajie walioshuhudia kwa macho kusimulia Yesu akisema mambo yale yale.
Mwishowe, hakuna ubaya wowote na wazo la waandishi wa Injili kutumia Injili zingine kama vyanzo. Luka anasema katika Luka sura ya 1 kwamba alitumia vyanzo vingine. Kuna uwezekano kuwa Mathayo na Luka walitumia Marko kama chanzo. Inawezekana kwamba kulikuwa na chanzo kingine zaidi ya Marko. Uwezekano wa kutumia chanzo cha "Q" sio sababu ya ni kwa nini dhana ya injili ya Q inapaswa kukataliwa. Matumizi ya chanzo ambacho kilikuwa na maneno ya Yesu haiondoi kuvuviwa kwa Maandiko. Sababu ya Injili ya Q inapaswa kukataliwa ni dhanio la watetezi wengi wa injili wa Q — ambayo ni kwamba Injili hazijavuviwa na Mungu.
Idadi kubwa ya wale wanaoendeleza dhana ya injili ya Q hawaamini kuwa Biblia imevuviwa (pumzi ya Mungu). Watetezi wengi wa Q hawaamini kwamba Injili ziliandikwa na Mitume na washirika wao wa karibu, au kwamba Injili ziliandikwa katika kizazi cha Mitume. Hawaamini kwamba inawezekana kuwa waandishi wawili au watatu wangeweza kutumia maneno yale yale bila kutumia maandishi ya mwingine kama chanzo. La muhimu, watetezi wengi wa Q wanakataa uvuvio wa Roho Mtakatifu kuwasaidia waandishi wa Injili kunakili kwa usahihi maneno na kazi za Yesu Kristo. Tena, matumizi ya chanzo cha "Q" sio shida. Shida ni sababu ambayo watetezi wengi wa injili ya Q wanaamini kuwa "Q" ilitumika, ambayo ni kukataa uvuvio wa Maandiko (Mathayo 5:18; 24:35; Yohana 10:35; 16: 12-13; 17:17. 1 Wakorintho 2:13; 2 Timotheo 3: 15-17; Waebrania 4:12; 2 Petro 1: 20–21).
English
Je! Injili ya Q ni gani? Je! Kunayo ushahidi wowote wa Injili ya Q?