Swali
Injili ya Thomaso ni nini?
Jibu
Injili ya Thomaso ni maandishi ya kikoptiki yaliyopatikana mwaka wa 1945 katika Nag Hammadi kule Misri. Maandishi hayo yana dondoo 114 yanayohusiana na Yesu. Baadhi ya nukuu hizo zinafanana na zile zinazopatikana kwenye Injili za Mathayo, Mariko, Luka na Yohanna. Misemo zingine zilibaki fiche hadi kufumbuliwa ama hata kupinga yaliyoandikwa katika vitabu vine vya injili.
Siku moja mwaka wa 1945 Desemba, kando ya mto Nile, Wamisiri wawili walikuwa wakitafuta mawe ya kipekee ya naitireti iliyotumika kama mbolea. Wakakuta kikombe kikubwa, kilichokuwa kama mita moja urefu, lililofichwa na jiwe kubwa. Ndani yake walikuta kusanyiko la vitabu vya ngozi na manakala. Mahali ambapo hizo vitabu vilipatikana ni karibu na manasteri ya kitambo, yaliyowekwa wazi na mwazilishaji wa kikristo,"senobitiko" monastisimu kule Misri, pachomiasi. Nag Hammadi, kijiji kilichokuwa hapo karibu kililipea hilo kusanyiko jina lake.
Maktaba ya Nag Hammadi ina jumla ya jumbe hamsini na mbili ama majalada yaliyoandikwa kwa lugha ya kikoptic kwenye papirasi na kukusanywa kwa majalida kumi na tatu, kumi na mbili zikiwa na kifungo tofauti ya ngozi. Arobaini kati yao hapo mwanzo zilikuwa hazijajulikana kati ya wasomi wa kisasa. Kati ya maandishi hayo, mengi yameandikwa kwa kuhusisha kiginostiki. Vijikaratasi vilivyopatikana kufunga majalida nane vilikuwa na tarehe kuonyesha hivyo vitabu viliandikwa katika karne ya nne, na moja kati ya hivyo inaonekana katoka kwa monasiteri. Majaribio ya kuvipea vitabu hivyo tarehe mwafaka inaendelea. Kwa jumla, inaeza semeka kuwa mikusanyiko ya hiyo ni ya kutoka karne ya nne. Inaweza kuwa kwamba jumbe hizo za kikoptic ni za miaka mingi ya awali, kadhalika jalida la awali [pengine lililoandikwa katika kigiriki ama kiromania] kutoka kwalo utafsiri wa kikoptic ulitolewa ukikiziwa kuwa miaka mingi Zaidi.
Injili ya Thomaso inaweza kuwa katika Kikanoni?
Wakuu wa kanisa la kwanza walifuata baadhi ya kanuni zifuatazo kuthathmini ikiwa kitabu cha Agano Jipya lilifunuliwa na Roho Mtakatifu : 1] Je,mwandishi alikuwa mtume ama kuwa na uhusiano wa karibu na mtume? 2] Je kitabu hicho kilikubaliwa na mwili wa Kristu kikamilifu? 3] Kitabu hicho kilikuwa na mwelekeo wa kanuni ama mafunzo ya kitamaduni? 4] Je kitabu hicho kilikuwa na ukweli wa kitamaduni na kiroho kitakachoangazia kazi ya Roho Mtakatifu?
Injili ya Thomaso inakosa kanuni hizi zote. Injili ya Thomaso haikuandikwa na mtumishi wa Yesu Thomaso. Viongozi wa kanisa la kwanza duniani kote waliitambua Injili ya Thomaso kama isiyo ya kweli. Injili ya Thomaso ilikataliwa na wafuasi wengi wa kanisa la kwanza. Injili ya Thomaso ina mafunzo mengi yanayokinzana na vitabu vya injili katika bibilia na kwenye Agano Jipya. Injili ya thomaso haina alama za kazi iliyoelekezwa na Roho mtakatifu.
Je kunayo mijadala Zaidi inayokamilisha Injili ya Thomaso ili ijumuishwe kwenye Bibilia? Ikiwa tutachunguza jumbe zote 114 zilizoko kwenye haya maandishi, basi tutapata baadhi zilizo sawia na zile zingalipo tayari, baadhi zenye ukinzani kiasi, ila sehemu kubwa haziwezi patikana popote kwenye nakala nzima. Maandiko lazima yawe na uwezo wa kujifafanua, na sehemu kubwa ya jumbe hizo kwenye injili ya Thomaso haziwezi kutambulika popote kwenye maandiko.
Pingamizi moja katika Injili ya Thomaso inayofanya isijumuishwe katika bibilia ni jina "usiri" linalofafanuliwa kutoka baadhi ya jumbe 114 na kazi hiyo yenyewe. Hakuna mahali kwenye maandishi neno la Mungu limewekwa "fiche "ila kupeanwa kwa wote wasome na kuelewa. Injili ya Thomaso kwa uwazi inajaribu kuweka baadhi ya maneno kuwa fiche.
Injili ya Thomaso ni kusanyiko la maneno ya Injili, ikiweka wazi kutoridhishwa na baadhi ya Wakristo. Injili ya Thomaso kwa ufupi ni kusanyiko lisilo kweli, kama vile tu Injili ya Yuda, injili ya Maria, na pia injili ya Filipo. Kadhalika mfuasi Thomaso jina la utani kuwa Thomaso asiyeamini inakubalika huku. Tunafaa zote kuishuku Injili ya Thomaso.
English
Injili ya Thomaso ni nini?