settings icon
share icon

Injili ya Luka

Mwandishi: Injili ya Luka haimtaji mwandishi wake. Kutoka Luka 1: 1-4 na Matendo 1: 1-3, ni wazi kwamba mwandishi mmoja aliandika Luka na Matendo, akivielekeza vitabu vyote viwili kwa "Thiopilasi aliyekuwa bora zaidi," pengine mtu mkubwa wa Kirumi. Utamaduni kutoka siku za mwanzo wa kanisa imekuwa kwamba Luka, daktari na rafiki wa karibu wa Mtume Paulo, aliandika Luka na Matendo (Wakolosai 4:14; 2 Timotheo 4:11). Hii itamfanya Luka mtu wa pekee wa Mataifa kuwahi kuandika vitabu vyovyote vya maandiko.

Tarehe ya kuandikwa: Injili ya Luka huenda iliandikwa kati ya 58 na 65 AD

Kusudi la Kuandika: Kama ilivyo na muhtasari mbili za injili zingine-Mathayo na Marko-kusudi la kitabu hiki ni kuonyesha Bwana Yesu Kristo na yote yeye "alianza kufanya na kufundisha, hadi siku alichukuliwa juu mbinguni" (Matendo 1: 1-2). Injili ya Luka ni ya kipekee kwa kuwa ni historia angalifu sana- "nakala ya utaratibu" (Luka 1: 3) Sambamba na akili ya kimatibabu ya Luka - mara nyingi hutoa maelezo ambayo nakala zingine zinaacha. Historia ya Luka ya maisha ya Mganga Mkuu inasisitiza huduma yake kwa-na huruma kwa watu wa mataifa mengine-Wasamaria, wanawake, watoto, watoza ushuru, wenye dhambi, na wengine waliochukuliwa kama watu waliotengwa na jamii katika Israeli.

Mistari muhimu: Luka 2: 4-7: "Yusufu aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeyé ni wa mbari na jamaa ya Daudi; ili aandikwe pamoja na Miriamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba. Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akmzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni. "

Luka 3:16, "Yohana alijibu akawaambia wote, kweli mimi nawabatiza kwa maji; Lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. "

Luka 4: 18-19, 21: "'Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 'Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. "

Luka 18: 31-32: "Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate, nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka. "

Luka 23: 33-34: "Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la kichwa, ndipo walipomsulubisha Yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. Yesu akasema, 'Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura. "

Luka 24: 1-3: "Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu."

Muhtasari kwa kifupi: Kinaitwa kitabu kizuri zaidi kilichowahi kuandikwa, Luka anaanza kwa kutueleza kuhusu wazazi wa Yesu, kuzaliwa kwa binamu yake, Yohana mbatizaji, safari ya Miriamu na Yusufu kwenda Bethlehem, mahali ambapo Yesu alizaliwa katika hori; na ukoo wa Yesu kupitia kwa Miriamu. Huduma ya hadharani ya Yesu inaonyesha huruma yake kamili na msamaha kupitia kwa hadithi za mwana mpotevu, tajiri na Lazaro, na msamaria mwema. Wakati wengi wanaamini katika upendo huu usiokuwa na madhara ambao unapita mipaka yote ya binadamu, wengine wengi -hasa viongozi wa kidini- huyapa changamoto na kupinga madai ya Yesu. Wafuasi wa Kristo wanatiwa moyo kuhesabu gharama ya uanafunzi, wakati maadui zake wanatafuta kifo chake msalabani. Hatimaye, Yesu anasalitiwa, anajaribiwa, kuhukumiwa na kusulubiwa. Lakini kaburi haliwezi kumshikilia yeye! Ufufuo wake unahakikisha kuendelea kwa huduma yake ya kutafuta na kuokoa waliopotea.

Mashirikisho: Kama mtu wa Mataifa, marejeleo ya Luka kwa Agano la Kale ni machache sana ikilinganishwa na Injili ya Mathayo, na mengi ya marejeleo ya Agano la kale yako katika maneno yaliyozungumzwa na Yesu kuliko katika masimulizi ya Luka. Yesu alitumia Agano la Kale kujitetea dhidi ya mashambulizi ya Shetani akimjibu kuwa "Imeandikwa" (Luka 4: 1-13); kujitambulisha mwenyewe kama Masihi aliyeahidiwa (Luka 4: 17-21); kuwakumbusha Mafarisayo juu ya kutokuwa na uwezo wa kushika sheria na mahitaji yao ya mwokozi (Luka 10: 25-28, 18: 18-27); na kuwashangaza katika mafunzo yao walipomjaribu na kumtega (Luka 20).

Vitendo Tekelezi: Luka anatupa picha nzuri ya Mwokozi wetu mwenye huruma. Yesu "hakukatishwa tamaa" na maskini na wenye mahitaji; kwa kweli, walikuwa lengo lake kimsingi la huduma yake. Israeli wakati huu Yesu alikuwa anafahamiwa sana katika mafunzo waliyokuwa wanapata kumhusu. Wadhaifu na wenye kunyanyaswa walikuwa kawaida hawana nguvu kuboresha maisha yao na hasa walifahamu sana ujumbe kwamba "Ufalme wa Mungu u karibu nanyi" (Luka 10: 9). Huu ni ujumbe ambao ni lazima tuupeleke kwa wale walio karibu nasi ambao wanahitaji kuusikia. Hata katika mataifa tajiri-pengine hasa hivyo- uhitaji wa kiroho ni kubwa sana. Wakristo lazima wafuate mfano wa Yesu na kuleta habari njema ya wokovu kwa maskini wa kiroho na wenye mahitaji. Ufalme wa Mungu u karibu na wakati unazidi kuyoyoma kila siku.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Injili ya Luka
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries