settings icon
share icon

Injili ya Marko

Mwandishi: Ingawa Injili ya Marko haimtaji jina la mtunzi wake, ni ushuhuda mkubwa wa mababa wa kanisa la kwanza kwamba Marko ndiye mwandishi. Alikuwa mshirika wa Mtume Petro, na bila shaka mwana wake wa kiroho (1 Petro 5:13). Kutoka kwa Petro alipokea taarifa halisi ya matukio na mafundisho ya Bwana, na kuhifadhi habari hiyo katika maandishi.

Kawaida imekubalika kwamba Marko ndiye Yohana Marko wa Agano Jipya (Matendo 12:12). Mama yake alikuwa tajiri na mkristo maarufu katika kanisa la Yerusalemu, na pengine kanisa lilimkutana katika nyumba yake. Marko alijiunga na Paulo na Barnaba katika safari yao ya kwanza ya umishonari, lakini si kwa ya pili kwa sababu ya kutokubaliana mkubwa kati ya watu hawa wawili (Matendo 15: 37-38). Hata hivyo, karibu na mwisho wa maisha ya Paulo akamwita Marko ili kuwa pamoja naye (2 Timotheo 4:11).

Tarehe ya kuandikwa: Injili ya Marko huenda ndiyo moja ya vitabu vya kwanza kuandikwa katika Agano Jipya, pengine katika 57-59 AD

Kusudi la Kuandika: Wakati Mathayo imeandikwa hasa kwa Wayahudi wenzake, injili ya Marko inaonekana kuwa ililengwa kwa waamini wa Kirumi, hasa watu wa mataifa. Marko aliandika kama mchungaji kwa Wakristo ambao hapo awali walikuwa wamesikia na kuamini Injili (Warumi 1: 8). Alitamani kwamba wawe na hadithi ya kihistoria ya maisha ya Yesu Kristo kama mtumishi wa Bwana na Mwokozi wa dunia ili kuimarisha imani yao katika uwepo wa mateso makali na kuwafundisha nini maana ya kuwa wanafunzi wake.

Mistari muhimu: Marko 1:11: "Na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe. "

Marko 1:17: "'Yesu akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.'"

Marko 10: 14-15: "Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie, kwa maana watoto kama hawa Ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kabisa. '"

Marko 10:45: "Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bila kutumikia, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi"

Marko 12:33: "'na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia '"

Marko 16: 6: "Naye akawaambia, msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulubiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka. '"

Marko 16:15: "Akawaambia, enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe"

Muhtasari kwa kifupi: Injili hii ni ya kipekee kwa sababu inasisitiza matendo ya Yesu zaidi ya mafundisho yake. Imeandikwa tu, kusonga kwa haraka kutoka sehemu moja katika maisha ya Kristo hadi kwa nyingine. Haianzi na nasaba kama katika Mathayo, kwa sababu watu wa Mataifa hawangehitaji kujua ukoo wake. Baada ya utangulizi wa Yesu wakati wa ubatizo wake, Yesu alianza huduma yake kwa watu katika Galilaya na kuwaita wanafunzi wanne wa kwanza wa wanafunzi wake kumi na wawili. Kinachofuata ni rekodi ya maisha ya Yesu, kifo na ufufuo.

Nakala ya Marko si tu mkusanyiko wa hadithi, ila ni masimulizi yaliyoandikwa kuonyesha kuwa Yesu ni Masihi, si tu kwa Wayahudi, bali kwa watu wa mataifa mengine pia. Katika taaluma ya nguvu, wanafunzi, wakiongozwa na Petro, walikubali imani yao kwake (Marko 8: 29-30), ingawa walishindwa kuelewa kikamilifu Umasihi wake mpaka baada ya ufufuo wake.

Tunapofuata safari yake kupitia Galilaya, maeneo jirani, na kisha Yudea, tunatambua ni haraka ya kasi aje aliweka. Aligusa maisha ya watu wengi, lakini aliacha alama isiyofutika kwa wanafunzi wake. Wakati wa mabadiliko (Marko 9: 1-9), aliwapa watatu wao onyesho la awali la kurudi kwake baadaye katika nguvu na utukufu, na tena ilidhihirishwa kwao yeye alikuwa nani.

Hata hivyo, katika siku zilizongoza kwa safari yake ya mwisho Yerusalemu, tunawaona wakikanganyikiwa, wakiwa na hofu na kusita. Katika kukamatwa kwa Yesu, Yeye alisimama peke yake baada ya wao kukimbia. Katika masaa yaliyofuata ya majaribio ya dhihaka, Yesu alitangaza kwa ujasiri kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa aliyebarikiwa zaidi, na kwamba Yeye atakuwa mshindi katika kurudi kwake (Marko 14: 61-62). Matukio ya hali anga yalitokea wakati wa kusulubiwa, kifo, kuzikwa na kufufuka hayakushuhudiwa na wengi wa wanafunzi wake. Lakini wanawake kadhaa waaminifu walishuhudia mateso yake. Baada ya Sabato, mapema asubuhi ya siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini na viungo vya kuzikwa. Wakati waliona jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, wakaingia kaburini. Haukuwa mwili wa Yesu walioona, bali malaika aliyevikwa mavazi meupe. Ujumbe wa furaha waliopata ulikuwa, "Amefufuka!" Wanawake walikuwa wainjilisti wa kwanza, walivyoeneza habari njema ya ufufuo wake. Ujumbe huu umetangazwa duniani kote katika karne zilizofuata hadi mpaka kwetu siku hizi.

Mashirikisho: Kwa sababu walengwa wa Marko walikuwa watu wa Mataifa, yeye hanukuu mara kwa mara kutoka kwa Agano la Kale kama Mathayo, ambaye alikuwa anaandika hasa kwa Wayahudi. Haanzi na historia ya maisha ya kuhusisha Yesu na watawala wa kiyahudi, lakini badala yake anaanza na ubatizo wake, mwanzo wa huduma yake hapa duniani. Lakini hata huko, Marko ananukuu kutoka kwa unabii wa Agano la Kale kuhusu mtume - Yohana Mbatizaji-ambao atawaonya watu ili "kuandaa njia kwa ajili ya Bwana" (Marko 1: 3; Isaya 40: 3) walipongojea kuja kwa Masihi wao.

Yesu anarejelea kwa Agano la Kale katika vifungu kadhaa katika Marko. Katika Marko 7: 6, Yesu anawakemea Mafarisayo kwa ibada yao ya juu juu ya Mungu kwa midomo yao tu, ilhali nyoyo zao zilikuwa mbali naye na anamrejelea nabii wao wenyewe, Isaya, kuwatia hatiani kwa kuifanya roho zao ngumu (Isaya 29:13). Yesu alitaja unabii mwingine wa Agano la Kale ambao ulikuwa utimizwe usiku ule ule wanafunzi watakapotawanyika kama kondoo wasio na mchungaji wakati Yesu alikamatwa na kuuawa (Marko 14:27; Zekaria 13: 7). Alirejelea tena Isaya wakati aliposafisha Hekalu la wanaobadilishana fedha (Marko 11: 15-17; Isaya 56: 7; Yeremia 7:11) na kwa Zaburi wakati Alieleza kwamba alikuwa jiwe kuu la msingi la imani yetu na la Kanisa (Marko 12: 10-11; Zaburi 118: 22-23).

Vitendo Tekelezi: Marko anamwonesha Yesu kama Mtumishi wa Mungu anayeteseka (Marko 10:45) na kama mmoja ambaye alikuja kutumikia na kujitoa sadaka kwa ajili yetu, katika sehemu ya kutuhamasisha kufanya hivyo. Tunapaswa kuhudu kama alivyofanya, na ukuu huo wa unyenyekevu na kujitoa kwa huduma za wengine. Yesu alituhimiza kukumbuka kwamba kuwa wakuu katika ufalme wa Mungu, ni lazima tuwe mtumishi wa wote (Marko 10:44). Kujinyima lazima kuzidi mahitaji yetu ya kutambuliwa au malipo, kama vile Yesu alikuwa tayari kudhalilishwa kama alivyotoa maisha yake kwa ajili ya kondoo.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Injili ya Marko
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries