Swali
Je! Jahannamu ni kitu cha kweli? Jehannamu ni ya milele?
Jibu
Ni jambo la kufurahisha kwamba asiri mia kubwa ya watu wanaamini kwa kuwepo kwa mbinguni kuliko kuwepo kwa jahannnamu. Kulingana na bibilia, ingawa jahannamu ipo vile mbinguni ipo. Bibilia kwa wazi na ukamilifu yafunza kwamba jahannamu ni mahali halisi wenye dhambi/na wasioamini wametumwa baada ya kifo. Wote tumetenda dhambi kinyume na Mungu (Warumi 3:23). Hukumu ya haki kwa hiyo dhambi ni kifo (Warumi 6:23). Jinsi dhambi zetu zote ni kinyume na Mungu (Zaruri 51:4), na jinsi Mungu hana mwisho na anaishi milele, adhabu ya dhambi, kifo lazima pia kiwe hakina mwisho na ni cha milele. Jahannnamu ni hiki kifo hakina wiwhso na ni cha milele ambacho tumekipokea kwa sababu ya dhambi zetu.
Adhabu ya wafu wenye dhambi jahannamu imeelezwa katika Bibilia yote kama “moto wa milele” (Mathayo 25:41), “moto usiozimika” (Mathayo 3:12), “aibu na kudharauliwa milele” (Danieli 12:2), mahali ambapo “moto hauzimiki (Mariko 9:44-49), mahali pa “mateso” na “moto” (Luka 16:23-24), “uaribivu wa milele” (2 Wathesalonike 1:9), mahali ambapo “moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele” (Ufunuo 14:10-11), na “ziwa la moto” mahali ambapo wenye dhambi “watateswa usiku na mchana milele yote” (Ufunuo 20:10).
Adhabu ya wenye dhambi jahannamu ile isiyo na kikomo kama vile furaha ya watakatifu mbinguni haina kikomo. Yesu mwenyewe alisema kwamba adhabu ya jahannamu ni ya milele vile maisha mbinguni ni ya milele (Mathayo 25:46). Wenye dhambi wote wako chini ya ghadhabu ya Mungu. Wale walio jahannamu watatambua haki kamili ya Mungu (Zaburi 76:10). Wale walio jahannamu watajua kwamba hukumu yao ni ya haki na wao wenyewe ndio watajilaumu (Kumbukumbu La Torarti 32:3-5). Naam, jahannamu ni halisi. Naam, jahannamu ni mahali pa mateso na adhabu idumuyo milele. Na Mungu atukuzwe kupitia Yesu, kuwa tunaweza kuepuka haya mauti ya milele (Yohana 3:16, 18, 36).
English
Je! Jahannamu ni kitu cha kweli? Jehannamu ni ya milele?