settings icon
share icon
Swali

Je, Masihi inamaanisha nini?

Jibu


Masihi inatoka kwa neno la Kiebrania mashiach na inamaanisha "aliyetiwa Wakfu" ama "mteule."

Neno sawia la Kigiriki ni Christos ama kwa Kiingereza, Christ. Jina "Yesu Kristo" ni sawa na "Yesu Masihi." Katika nyakati za Biblia, kupaka mtu mafuta ilikuwa ishara kuwa Mungu alikuwa akimtakasa ama kumtenga mtu huyo kwa ajili ya kutekeleza jukumu fulani. Kwa hivyo, "aliyetiwa wakfu" alikuwa mtu aliyekuwa na kusudi maalum, kusudi lililoamuriwa na Mungu.

Katika Agano la Kale, watu walitiwa wakfu kwa majukumu ya nabii, kuhani na mfalme. Mungu alimwambia Elia amtie mafuta Elisha ili awe nabii wa Isreaeli ( I Wafalme 19:16). Haruni aliwekwa wakfu kama kuhani mkuu wa kwanza wa Israeli ( Mambo ya Walawi 8:12). Samweli aliweka wakfu Sauli na Daudi kuwa Wafalme wa Israeli (I Samweli 10:1; 16:13). Wanaume hawa wote walikuwa na majukumu yaliyo "tiwa wakfu." Lakini Agano la Kale lilitabiri kuwa Mkombozi ajaye, aliyechaguliwa na Mungu kukomboa Israeli (Isaya 42:1; 61:1-3). Mkombozi huyu alijulikana na Wayahudi kama Masihi.

Yesu wa Nazareti alikuwa na ndiye Masihi aliyetabiriwa (Luka 4:17-21; Yohana 4:25-26). Katika Agano Jipya tunaona dhibitisho kwamba Yesu niye Mteule: "Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake" (Yohana 20:31). Tunasikia ushuhuda kwamba Yesu ni "Masihi, Mwana wa Mungu aliye hai" (Mathayo 16:16). Kufufuka kwake Yesu kutoka kwa wafu ni dhibitisho la mwisho kwamba Yesu ni Masihi aliyeahidiwa, aliyewekwa Wakfu. Matendo ya Mitume 10:39-43 inatoa ushuhuda wa kufufuka kwake na ukweli kwamba "Yeye ndiye aliyeteuliwa na Mungu kuwa hakimu wa walio hai na wafu."

Yesu anatimiza jukumu la Nabii, Kuhani, na Mfalme, dhibitisho ya kwamba yeye ni Masihi. Yeye ni Nabii kwa sababu alijawa na pia kuhubiri Neno la Mungu. (Tazama Yohana1:1-18; 14:24 na Luka24:19); Kuhani, kwa sababu kifo chake kililipia dhambi zetu na kutupatanisha na Baba (tazama Waebrania 2:!7; 4:14); na mfalme, kwa sababu baada ya kufufuka kwake, Mungu alimpa mamlaka yote. (Tazama Yohana 18:36; Waefeso 1:20-23; na Ufunuo 19:16).

Wayahudi wa wakati wa Yesu walitarajia Masihi kukomboa Israeli kwa kupindua utawala wa Warumi na kuanzisha ufalme wa kidunia (Tazama Matendo ya Mitume 1:6). Baada ya kufufuka kwa Yesu ndipo hatimaye wanafunzi wake walianza kuelewa ambacho unabii katika Agano la Kale ulimaanisha Masihi angefanya (Tazama Luka 24:25-27). Masihi "aliwekwa wakfu" kwanza kuwaokoa watu wake kiroho; kuwakomboa kutoka kwa dhambi (Yohana 8:31-36). Alikamilisha wokovu huu kupitia kifo na kufufuka kwake (Yohana 12:32; Yohana 3:16). Baadaye, Yesu Masihi atakomboa watu wake kutoka kwa maadui, atakapoweka ufalme wake duniani (Tazama Isaya 9:1-7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Masihi inamaanisha nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries