Swali
Je! Yesu anatuombea?
Jibu
Maombi ni kitendo cha kuwasiliana na Mungu. Tunajua kuwa ilikuwa sehemu kubwa ya maisha ya Yesu alipokuwa duniani (Luka 6:12; Marko 14:32; Mathayo 26:36). Alitumia muda wake mwingi akiwa na Babake. Muda mwingi, chenye alichoomba kuhusu tunaweza kukisia tu; walakini, sehemu chake katika Agano Jipya zinatuambia uhalisi wa kile alichoomba. Katika Mathayo 19:13, aliwaombea watoto wadogo. Katika Luka 22:32, anatuambia kumba aliiombea imani ya Petro ibaki kuwa imara. Na katika Yohana 17 ombi kuu la ukuhani la Yesu, aliwaombea wanafanzi wake "wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao" (aya ya 20). Ambao ni sisi. Na sasa Yesu amepaa mbinguni, angali anatuombea. Huduma yake kwa niapa yetu ingali inaendelea (Waebrania 7:25).
Yesu ni "Mwombezi kwa Baba" (1 Yohana 2:1). Wakili ni yule anayetutetea kesi kwa niapa ya mwingine. Mawakili husimama mahali pa wale wasioweza kujitetea wenyewe. Yesu kama wakili wetu, anasimama mahali petu mbele ya Baba na kutuombea. Uwakili wa Yesu ni wa hakika kutekeleza, kwa sababu Yeye ndiye yule Baba alisema, "Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye" (Mathayo 3:17). Maombi ya Yesu kwa ajili yetu ni ya kila wakati, na ni makamilifu.
Tunaye mtetezi katika Kristo, lakini pia tunaye mshitaki: Shetani ambaye hutushitaki usiku na mchana (Ufunuo 12:10; Zekaria 3:1). Adui wetu aliye na mwisho huzitangaza dhambi zetu mbele za Mungu, akiwakejeli na kuwadalalisha wale ambao Yesu alijinunulia. Lakini Warumi 8:33-34 inasema kuwa tusiogope uongo wa Shetani kwa sababu Yesu mtetezi wetu ana nguvu zaidi: "Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu mwenyewe huwaondolea hatia! Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka kwa wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye anatuombea."
Katika Yohana 17, Yesu anawaombea wanafunzi wake na kutoka ombi hili tunaweza kujifunza aina ya vitu ambavyo Yesu anatuombea sasa. Yesu anatuombea kuwa tuweze kutenda na kuwa vitu hivi:
• Mjue Mungu na mwana wake, Yesu Kristo (aya ya 3)
• Kulindwa na ukafiri (mstari wa 11)
• Kuwa mmoja roho kama vile Baba na Mwana walivyo mmoja (aya ya 11)
• Kujazwa na furaha Yake (mstari 13)
• Kulindwa na yule mwovu (aya ya 15)
• Kutakaswa kupitia kwa Neno la Mungu (aya ya 17)
• Kaa kuunganika katika Kristo katika vizazi vyote (aya ya 20-25)
• Hebu na upendo wetu utangaze ujumbe wa Kristo kwa ulimwengu (aya ya 23)
• Kuungana naye mbinguni milele yote (aya ya 24)
• kupata aina ile ile ya upendo na kila mmoja upendo ambao Baba na Mwana wanashiriki (aya ya 26)
Waebrania 4:14-16 inamwelezea Yesu kama Kuhani Mkuu. Kwa sababu ya uombezi wake kwetu, tumepeta ruhusa ya kumfikia Baba sisi wenyewe: "Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu. 15Huyu Kuhani Mkuu wetu anaelewa kabisa unyonge wetu; yeye mwenyewe alijaribiwa kama sisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi. Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu mwenye neema, tupokee huruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida." Licha ya kile tutakumbana nacho katika maisha haya, tunaweza kuishi na hakika jasiri kuwa, ikiwa sisi ni wa Kristo, Yeye anatuombea kila wakati.
English
Je! Yesu anatuombea?