settings icon
share icon
Swali

Yesu alimaanisha nini aliposema," Jitwike msalaba wako na kunifuata"(Mathayo 16:24, Marko 8:34, Luka 9:23)?

Jibu


Hebu tuanze na kile ambacho Yesu hakumaanisha. Watu wengi hutafsiri "msalaba" kama mzigo fulani ambao wanapaswa kubeba katika maisha yao: uhusiano wa kulazimisha, kazi isiyo na shukrani, ugonjwa wa kimwili. Na kiburi cha kujisikitikia, wanasema, "Huo ni msalaba wangu lazima niubebe." Tafsiri kama hiyo sio kile Yesu alimaanisha wakati aliposema, "Jitwike msalaba wako na kunifuata."

Wakati Yesu alibeba msalaba Wake Golgotha ili asulubiwe, hakuna mtu alikuwa akifikiria msalaba kama mfano wa mzigo wa kubeba. Kwa mtu wa karne ya kwanza, msalaba ulimaanisha kitu kimoja na kitu kimoja pekee: kifo kwa njia ya uchungu na ya aibu zaidi wanadamu wanaweza kuendeleza.

Miaka elfu mbili baadaye, Wakristo wanaona msalaba kama alama ya kutunza ya kupatanishwa, msamaha, neema, na upendo. Lakini katika siku za Yesu, msalaba haukuwakilisha chochote ila kifo cha maumivu makali. Kwa sababu Warumi walilazimisha wahalifu walio na hatia kubeba misalaba yao hadi mahali pa kusulubiwa, kuchukua msalaba kulimaanisha kubeba kifaa chao cha kutekeleza huku wakipata dhihaki wakielekea kufa.

Kwa hivyo, "Jitwike msalaba wako na kunifuata" inamaanisha kuwa tayari kufa ili kumfuata Yesu. Hii inaitwa "kufa kwa nafsi." Ni mwito wa kujisalimisha kabisa. Baada ya Yesu kuamuru kubeba msalaba, alisema, "Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wotw, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?" (Luka 9:24-25; Mathayo 16:26; Marko 8:35-36). Ingawa mwito ni ngumu, tuzo halilinganishwi.

Popote Yesu alienda, aliwavuta watu. Ingawa mara nyingi watu hawa walimfuata Yeye kama Masihi, mtazamo wao juu ya nani alikuwa Masihi kweli -na kile angeweza kufanya-ulipotosha. Walifikiri kwamba Kristo angeweza kuanzisha ufalme uliorejeshwa. Waliamini kuwa atawaokoa huru na utawala dhalimu wa wamiliki wao wa Kirumi. Hata wanafunzi wendani kabisa wa Kristo mwenyewe walifikiri ufalme ungekuja karibuni (Luka 19:11). Wakati Yesu alianza kufundisha kwamba angekufa mikononi mwa viongozi wa Kiyahudi na wakabaila wa Mataifa (Luka 9:22), umaarufu wake ulipotea. Wafuasi wengi waliotetemeka walimkataa. Kwa kweli, hawakuweza kuua mawazo yao wenyewe, mipango, na tamaa, na kuzibadilisha kwa ajili Yake.

Kumfuata Yesu ni rahisi wakati maisha yanaenda vizuri; msimamo wetu wa kweli Kwake unafunuliwa wakati wa majaribio. Yesu alituhakikishia kwamba majaribu yatakuja kwa wafuasi wake (Yohana 16:33). Ufuasi unataka dhabihu, na Yesu hakuficha gharama hiyo.

Katika Luka 9:57-62, watu watatu walionekana kuwa tayari kumfuata Yesu. Wakati Yesu aliwauliza maswali zaidi, kujitolea kwao kulikuwa nusu ya moyo kwa ubora. Walikosa kuhesabu gharama ya kumfuata. Hakuna yeyote alikuwa tayari kuchukua msalaba wake na kusulubisha juu yake maslahi yake mwenyewe.

Kwa hivyo, Yesu alionekana kuwazuia. Ni tofauti gani kutoka utoaji wa injili kamili! Ni watu wangapi wanaweza kuitikia wito wa madhabahu ambao ulienda, "Njoo umfuate Yesu, na unaweza kukabiliana na kupoteza marafiki, familia, sifa, kazi, na hata maisha yako"? Idadi ya waongofu wa uongo ingeweza kupungua. Mwito kama huo ndio Yesu alimaanisha wakati aliposema, "Jitwike msalaba wako na kunifuata."

Ikiwa unashangaa ikiwa uko tayari kuchukua msalaba wako, zingatia maswali haya:
"Je! Uko tayari kumfuata Yesu ikiwa ina maana ya kupoteza baadhi ya marafiki zako wa karibu zaidi?
"Je, uko tayari kumfuata Yesu ikiwa ina maana ya utenganishaji na familia yako?
"Je! Uko tayari kumfuata Yesu ikiwa ina maana kupoteza sifa yako?
"Je! Uko tayari kumfuata Yesu ikiwa ina maana ya kupoteza kazi yako?
"Je, uko tayari kumfuata Yesu ikiwa inamaanisha kupoteza maisha yako?

Katika maeneo mengine duniani, matokeo haya ni ukweli. Lakini angalia maswali haya yamekiraiwa, "Je, uko tayari?" Kumfuatia Yesu haimaanishi kwamba mambo haya yote yatatokea kwako, lakini uko tayari kuchukua msalaba wako? Ikiwa itafika kiwango katika maisha yako ambapo unakabiliwa na chaguo-Yesu au raha ya maisha haya-ni gani utachagua?

Kujitolea kwa Kristo inamaanisha kuchukua msalaba wako kila siku, kuacha matumaini yako, ndoto, mali, hata maisha yako yenyewe ikiwa kuna haja kwa sababu ya Kristo. Ikiwa tu uko tayari kuchukua msalaba wako unaweza kuitwa mwanafunzi Wake (Luka 14:27). Tuzo ina thamani ya malipo. Yesu alifuatilia wito wake wa kifo kwa nafsi yake ("Jitwike msalaba wako na kunifuata") na zawadi ya uzima ndani ya Kristo: "Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona" (Mathayo 16:25).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu alimaanisha nini aliposema," Jitwike msalaba wako na kunifuata"(Mathayo 16:24, Marko 8:34, Luka 9:23)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries