settings icon
share icon
Swali

Jukumu la Roho Mtakatifu ni gani katika maisha yetu hii leo?

Jibu


Zaidi ya yote kila karama zote zilizo tolewa kwa wanadamu na Mungu, hakuna iliyo kubwa zaidi kuliko uwepo wa Roho Mtakatifu. Roho ana kazi nyingi, majukumu, na kazi. Kwanza, anafanya kazi katika moyo wa kila mtu kila mahali. Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba angemtuma Roho ulimwenguni "kuushawishi ulimwengu kuhusiana na hatia ya dhambi, haki na hukumu" (Yohana 16:7-11). Kila mtu ana "fahamu ya Mungu," hata kama watakubali au kukana hilo. Roho anatumia ukweli wa Mungu kwa mawazo ya watu kuwashawishi kwa hoja haki na kutosha kwamba wao ni wenye dhambi. Akijibu hili imani huleta watu katika wokovu.

Mara tu tunapookolewa na kuwa mali ya Mungu, Roho anaweka makazi katika mioyo yetu milele, kutuhakikishia na kuthibitishia ahadi ya hali yetu ya milele kama watoto wake. Yesu alisema atatumia Roho kuwa Msaidizi wetu, Msaidizi, na kiongzi. "Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi hata milele" (Yohana 14:16). Neno la Kigiriki linalotafsiriwa hapa "Mshauri wa" maana yake "moja aitwaye pamoja na" na ana wazo la mtu ambaye anatia moyo na kusihi. Roho Mtakatifu huchukua makazi ya kudumu katika mioyo ya waumini (Warumi 8:9; 1 Wakorintho 6:19-20, 12:13). Yesu alitoa Roho kama "fidia" kuwa wakati hayupo, afanye kazi kwetu sisi ambayo angefanya kama yeye binafsi bado angebaki nasi.

Miongoni mwa kazi hizo ni ile ya kufumbua ukweli. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani mwetu unatuwezesha kuelewa na kutafsiri neno la Mungu. Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba "wakati Yeye, Roho wa Kweli, atakuja, atawaongoza kwenye ukweli wote" (Yohana 16:13). Yeye anaonyesha akili zetu kusudi lote la Mungu kama linahusiana na ibada, mafundisho, na maisha ya Kikristo. Yeye ndiye kiongozi wa mwisho, kwenda mbele, kuongoza njia, kuondoa vizuizi, kufungua akili, na kufanya mambo yote wazi na ya wazi. Yeye anaongoza katika njia tunayopaswa kwenda katika mambo yote ya kiroho. Bila mwongozo huo, tutakuwa watu wanaoweza kuanguka katika makosa. Sehemu muhimu ya ukweli Yeye inaonyesha ni kwamba Yesu ni nani vile alivyokiri yeye ni nani (Yohana 15:26, 1 Wakorintho 12:3). Roho anatusadikishia uungu wa Kristo na mwili wake, Yeye kuwa Masihi, mateso yake na kifo chake, ufufuo na kupaa kwake, kuadhimishwa kwake katika upande wa kulia wa Mungu, na jukumu lake kama hakimu wa wote. Anatoa utukufu wote kwa Kristo katika mambo yote (Yohana 16:14).

Mojawapo wa majukumu mengine ya Roho Mtakatifu ni kuwa yeye ndiye anapeana karama. Wakorintho wa kwanza 12 inaeleza vipawa vya kiroho kwa ajili ya waumini ili tuweze kufanya kazi kama mwili wa Kristo hapa duniani. karama hizi zote, ndogo na kubwa, zinapewa na Roho ili sisi tuweze kuwa mabalozi wake kwa ulimwengu, kuonyesha neema yake na kumtukuza Yeye.

Roho pia anfanya kazi kwa kuzalisha matunda katika maisha yetu. Wakati Yeye hukaa ndani yetu, huanza kazi ya kuvuna matunda yake katika maisha yetu- upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kujitawala (Wagalatia 5:22-23). Haya si matendo ya mwili yetu, ambayo ni uwezo wa kuzalisha matunda hayo, lakini ni bidhaa za uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu.

Maarifa kwamba Roho Mtakatifu wa Mungu amechukua makazi katika maisha yetu, kwamba anafanya kazi hizi zote za miujiza, kwamba Yeye anaishi na sisi milele, na kwamba kamwe hatatuacha na huleta furaha kubwa na faraja. Namshukuru Mungu kwa thamani hii kubwa ya karama ya Roho Mtakatifu na kazi yake katika maisha yetu!

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Jukumu la Roho Mtakatifu ni gani katika maisha yetu hii leo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries