Swali
Je, ni nini husababisha kugawanyika kanisani? Je, upendo unaeza rudi aje kanisani baada ya kugawanyika?
Jibu
Tofauti ambazo hupelekea kanisa kugawanyika ni za huzuni na huwa ni za kawaida katika mwili wa Kristo. Matokeo ambayo huletwa na kugawanyika kwa kanisa bila kuzingatia ata sababu ya mgawanyiko huo huwa za uharibifu mkubwa kwenye kanisa. Mgawanyiko kwenye kanisa hueka waumini ambao wamekomaa kwenye dhiki na kufadhaika, na wale ambao ni wachanga hukata tamaa, pia husababisha maafa kwa wahubiri na familia zao na huleta lawama kwa jina la Kristo. Lakini kuna matumaini kwamba upendo unaeza rejea kwa kanisa ambayo imegawanyika.
Kanisa ni kama hosipitali ambayo imejaa watu waliojeruhiwa na wagonjwa, lakini kanisani ugonjwa ni dhambi na wale ambao wanaumizwa kwa sababu ya dhambi ya wengine ndio wanafananishwa na majeruhi. Dhambi ambayo inaeza sababisha shida mingi kwa kanisa ni ukosaji wa msamaha miongoni mwa waumini. Hakuna mkristo amekamilika, na hakuna mhubiri ama kiongozi ama askofu ambaye ni mkamilifu. Wakati watu hawa wote ambao si wakamilifu wanakusanyika pamoja, kutokubaliana, kuumizana hisia na kutoelewana ni vitu ambazo haziezi epukika. Ikiwa tunatarajia wengine kutufanyia mazuri, tamaa huwa miongoni mwetu na hatuezi epuka na inaweza kuumiza hisia zetu na kuleta chuki. Majibizano kati yetu inafaa kuwa jinsi tunafaa kusamehana kwa fadhili na huruma( Waefeso 4:32; Wakolosai 3:13) na kwa mapenzi ya kikristo ambayo hufunika dhambi mingi ili tuweze kuhudumiana kikristo(1Petero 4:8-11). Tunapojitolea kusamehea, kupendana na kuhudumia wengine tutaona tofauti jinsi tunazuruhisha chuki zetu. Lakini tukishikilia tofauti zetu za maoni, haswa maoni ambayo hayahusiki na maneno muhimu na kuanza kusengenyana huwa inaongeza mgawanyiko, na waumini wengi wa kanisa huumia na hii inaathiri ujumbe wetu wa mahubiri kwa ulimwengu
Mgawanyiko wa kanisa unaeza tokea wakati mtu mmoja anatafuta kudanganya watu ama kwa miradi fulani ili ajinufaishe. Inaeza kuwa kuna ubaguzi kwa kulinda sheria, na kwa wale wachache ambao hawalindi sheria izo huwa wanadhulumiwa. Inaeza kuwa kwamba kuna tafsiri moja ya mafundisho ambayo si maana na imezingatiwa kubaini ni nani ako ama hayuko sawa, ama kuna mwenye anapigania uongozi kutoka kwa mhubiri ama wazee na amedanganya makundi fulani ya watu ili wamuunge mkono aweze kuchukua uongozi huo. Cha kuhuzunisha ni, maoni tofauti kuhusu mitindo za kuimba na muziki mara nyingi huleta kugawanyika kanisani. Sababu mingi hutolewa kwa mgogoro huo, lakini zote zimekita mizizi kwa kiburi na kujipenda. Yakobo 4:1-3 inasema "Mapigano na ugomvi wote kati yenu inatoka wapi? Hutoka katika tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu. Mnatamani vitu na kwa vile hamvipati mko tayari kuua; mwatamani sana kupata vitu,lakini hamvipati, hivyo mnagombana na kupigana. Hampati kile mnachotaka kwa sababu hamkiombi kwa Mung.Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tama zenu."
Kitu ingine ya kutilia maanani ni kuwa, si kila mtu anayekaa kanisani kila wiki ni mkristo wa kweli, na si kila mtu anayesema jina la Kristo ni wake, hii ni ukweli ambao alisema kwa kitabu cha Mathayo 7:16-23. Tunaeza jua ukweli na uongo kwa kuangalia matunda yake. Wakristo wa kweli wanaonyesha matunda ya kiroho kwa uwazi ambayo iko ndani yao (Wagalatia 5:22-23), magugu penye ngano imepandwa huleta mfarakano. Tunafaa kuwa macho kwa wale adui anatuletea kwa maisha yetu na tuonyeshe hekima na utambuzi kwa kutumia heshima ya kanisa penye inafaa (Mathayo 18:15-20) na tuongee ukweli ulio na upendo kwa kila kitu (Mathayo 10:16; Waefeso 4:15).
Mwisho,kila kanisa limeundwa na wanachama wake wa kipekee na jinsi hawa wanachama wanaishi inaathiri jinsi kanisa linafanya mipango zake. Paulo anaonya kanisa la Roma liweze kuishi na maisha ya heshima, "Tuishi maisha ya heshima kama inavyopasa wakati wa mchana, si kwa ulafi na ulevi; si kwa ufisadi na uasherati; si kwa ugomvi na wivu."( Warumi 13:13). Wanachama wa kanisa huwa wanashawishiwa na maandili mbaya ya kila siku, na saa moja takatifu kanisani kila wiki ijatosha kupambana na maandili haya. Wokovu moyoni imekamilishwa na kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Ni jukumu la kila muumini kumfuata Kristo kwa bidii na kufanya kazi ya ukuaji wa roho kwa kusoma Biblia, kutenga wakati na Mungu kupitia maombi na kuabudu pamoja na waumini wengine ata nje ya kanisa (Wafilipi 2:12-13). Kuenda kanisa ni kitu ya maana lakini kuishi maisha ya kikristo ni muhimu kuliko kuenda kanisa kila wiki. Viwango vya ulimwengu ni kujitangaza,kujithamini, na kujiabudu, na kuongeza manufaa kwa wengine ikiwa wamejitolea kutuiga jinsi sisi wenyewe tuko. Mtazamo huu hupelekea kuwa kwa mfarakano na chuki ambayo inatokana na tabia ya kuabudu miungu ya kibnafsi. Jibu linapatikana Tito 2:11-13: " Maana Mungu ameidhihirisha neema yake inayookoa watu wote, hiyo inatufundisha kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia ili tuishi katika ulimwengu wa sasa kwa njia ya werevu, haki na kuionesha heshima yetu kwa Mungu. Kadri tunavyosubiri ile siku iliyobarikiwa tunayoitumaini ambapo utukufu wa Mungu wetu Mkuu na Mwokozi Yesu Kristo itakapofunuliwa." Kwa wale ambao wako na imani kwa Kristo wamehesabika kuwa wa Mungu na wamepata neema yake, na inatusaidia kuepuka tamaa za kidunia, kuachana na usherati na kuishi kikristo kwa kuonyesha wengi upendo: "Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu; kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake." (Wafilipi 2:3)
Mgawanyiko wa kanisa humalizwa kupitia kudhubu na kuwa mnyenyekevu. Ikiwa kuna kutokubaliana, kitu ya muhimu kufanya ni makundi yote mbili kudhubu kitu yeyote mbaya ilisemwa ama kutendwa kwa njia ambayo si ya kufurahisha wakati wa mgawanyiko. Kudhubu ni kuomba msamaha kutoka kwa yule ambaye amekosewa kwa sababu ya tabia fulani. Kuwa mnyenyekevu ina maana kila mmoja anafaa kukubali msamaha wa mwingine, na kukubaliana kuishi kwa upendo wa kikristo.
Na kuna hali zingine kuachana na hicho kikundi ni suluhu mwafaka. Ikiwa uongozi wa kanisa unaacha misimamo ya maandiko kwa masuala muhimu kama Uungu wa Yesu Kristo, kuzaliwa kwa bikira,Mungu ka muumba,msukumo na mamlaka ya maandiko, ama mafundisho ya kimsingi ni bora kuachana na kikundi/kaanisa.
Sababu za mgawanyiko kanisani ni mingi, lakini sababu kuu yenye huchangia mgawanyiko ni ile kuwa kuna mtu ameacha kumzingatia Yesu Kristo na kuanza kutumia miradi za kanisa kujinufaisha. Kanisa linafaa kuwa hai ama la muhimu kuliko ata miradi. Mtume Paulo anatumia mfano wa mwili kufananisha kanisa. Katika kitabu cha 1Wakoritho 12 na Warumi 12, anaita kanisa mwili wa Kristo. Tunafaa kuwa mwili unaofanya mapenzi ya kichwa ambayo ni Yesu Kristo. Ikiwa kila mtu katika mwili anazingatia kufanya mapenzi ya Mungu na kumuabudu Yesu Kristo kwa upendo na unyenyekevu, basi kutakua na mgawanyiko lakini mgawanyiko huo utasuluhishwa kwa njia ya upendo na inayofaa.
English
Je, ni nini husababisha kugawanyika kanisani? Je, upendo unaeza rudi aje kanisani baada ya kugawanyika?