settings icon
share icon
Swali

Kanuni iliyofungwa- je! Maana yake ni gani?

Jibu


Kanuni ya Maandiko inarejelea vitu vytoe katika Biblia ya Kikristo na Biblia ya Kiebrania ambazo kwa Pamoja vinaunda Neno la Mungu lililokamilika na lenye pumzi Yake. Ni vitabu tu pekee vya kanuni ya Biblia vinachukuliwa kuwa na mamlaka katika masuala ya imani na mazoezi. Dhana ya kanuni kufungwa ni kuwa Biblia imekamilika; hakuna vitabu vingine vinaongezwa tena. Mungu haongezei Neno Lake.

Kanuni ya Maandiko iliamuliwa na Mungu, na sio mwanadamu. Kufanya utofautisho huu ni muhimu. Vitabu ambavyo vimekubaliwa havikuchukuliwa kuvuviwa kwa sababu Mungu alivivuvia katika wakati vilikuwa vinaandikwa. Watu wa Mungu waliwajibika tu kwa kuvigundua au kuitambua kanuni ya Biblia. Mchakato wa utambuzi ulianza na wasomi wa Kiyahudi na waalimu na kutamatizwa na Wakristo wa kanisa la mapema mwishoni mwa karne ya nne.

Kukamilika au kufungwa kwa kanuni ya Maandiko iliyoundwa wakati kanisa la kwanza lilipoipima na kutambua kilichokuwa hakika Neno la Mungu lililovuviwa. Kusungumza kibinadamu, mchakato ulipoendelea udhaifu uliingia, lakini mwishowe kusudi la Mungu lilidhihirika.

Leo hii Waprotestanti wanajumuisha vitabu 66 vya Agano la Kale na Jipya katika kanuni ya Biblia. Wakatoliki wa Kirumi na baadhi ya makanisa kadhaa ya Orthodox ya Mashariki wanakubalia maandishi zaidi yanayoitwa Apokirifa, mkusanyiko wa vitabu ambavyo havitambuliwa kuwa vya mamlaka au kuongozwa na Mungu katika Uyahudi na Ukristo wa Kiprotestanti.

Manufaa maalum ya kanuni kufungwa ni kwamba vitabu vya kuongezea haviwezi ongezwa katika Biblia na hakuna hata mojawapo ya vitabu ambavyo viko kwenya kanuni vinaweza kuondolewa. Mungu ashasungumza.

Kanuni kufungwa inamaanisha kuwa vitabu vingine vya dini ambavyo wafuasi wa dini wanadai vimevuviwa na Mungu vinafaa kukataliwa na kuchukuliwa kuwa vya uwongo. Kitavu cha Momoni, Kurani, Vedas, mabishano makuu, Sayansi na Afya yenye Ufunguo wa Maandiko- hivi vyote ni kazi ya mwanadamu na sio zao la Roho Mtakatifu wa Mungu.

Kanuni kufungwa pia inaashiria kuwa hakuna mtume au malaika hii leo ambao wanapokea ujumbe kutoka kwa Mungu. Kanisa limetunukiwa na waalimu na wahubiri wa Neno hii leo, lakini mtu yeyote anayedai kuwa na ufunuo mpya kutoka kwa Mungu, na kuudai kuwa umevuvishwa naye Mungu, au kudai mamlaka sawia nay a Biblia yeye anapotosha watu. Huzuni ni kuwa watu wengi katika kanisa wanatii ndoto na maono yaliyonenwa kutoka kwa madhabahu na kutoka kwa wale wanaodai kuwa "Mungu amewanenea."

Lakini, je! kungegunduliwa kitabu kingine cha unabii hii leo? Je! sembuze barua aliyopotea ailiokuwa imeandikwa na mtume Paulo ingepatika? Hata kama barua nyingine ingepatikana, na iweze kuthibitishwa kuwa ya Paulo, hatuwezi kuiongeza kwa kanuni ya Maandiko. Tunachukulia kuwa Paulo aliandika barua nyingi kwa makundi tofauti katika kipindi chake cha huduma, lakini baadhi ya hizo hazikuifadhiwa, kumaanisha kuwa haikuwa mapenzi ya Mungu ya hizo kujumuishwa katika kanuni (ona 2 Wakorintho 7:8 kwa uwezekano wa urejeleo wa barua ambazo sio za kanuni ya Biblia).

Yuda, mojawapo ya vitabu vya mwisho kujumuishwa katika kanuni ya Biblia kabla ifungwe, anasema, "Wapendwa, ingawa nilikuwa ninatamani sana kuwaandikia kuhusu wokovu ambao tunaushiriki sisi sote, niliona imenipasa kuwaandikia na kuwasihi kwamba mwitetee imani iliyokabidhiwa watakatifu kwa nafasi moja itoshayo" (Yuda 1:3). Maneno "imani" katika kifungu hiki hurejelea jumla ya kile Wakristo wanaamini, mafundisho yote ya mitume, au imani zote za Kikristo. Kwa maneno mengine kila kitu tunachoamini katika imani ya Kikristo kishakwisha tolewa au kufunuliwa kwa waumini kupitia kwa mitume na manabii. Kupitia kwa Maandiko, Mungu ametupa ufahamu wa mwisho na kamilifu wa kuishi imani ya Kikristo.

Kanuni yenye haijafungwa itaruhusu vitabu au vifungu vya Maandiko kuongezwa kwa Biblia kupitia kwa ufunuo endelefu. Kwa kuongeza vitabu kwa kanuni ya Biblia, kwa njia ingine tunasema kuwa Biblia ya sasa haijakamilika, au kuna vitu inakosa.

Mithali 30:5-6 inatuonya kuwa tusiongeze chochote kwa maneno ya Mungu: "Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia. Usiongeze kwenye maneno yake, ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo."

Kumbukumbu la Torati 4:2 inatuonya kuwa tusiongeze au kuondoa chochote kutoka kwa amri ya Mungu: "Usiongeze wala usipunguze chochote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo ya Bwana Mungu wenu ambayo nawapa" (ona pia Kumbukumbu 12:32).

Mwishoni mwa kitabu cha Ufunuo, kitabu cha mwisho cha Biblia, tunasoma onyo hilo hilo: "Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Mtu yeyote akiongeza humo chochote, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19Kama mtu yeyote akipunguza humo chochote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki" (Ufunuo 22:18-19).

Kuikubali kanuni iliyofungwa inamaanisha kukubali dhana kuwa Mungu amekwisha funua kila kitu chenye watoto wake wanapaswa kujua. Pia inamaanisha kuwa kila kitu amefunua katika Maandiko ni pumzi Yake. Chochote kisiongezwe, na chochote kisitolewe au kupuuzwa.

Kanuni iliyofungwa haimanishi kuwa Mungu ameacha kujifunua Mwenyewe kwa watu Wake hii leo kuwa hakuna ufunuo mpya wa kweli nje ya kile ambacho amekwisha funua katika Biblia kwa kanisa. Mungu ameweka katika kanuni ya Maandiko kila kitu tunachohitaji kujua kumhusu, juu vile tulivyo, vile tunapaswa kuishi, na kile kitatokea baadaye (ona 2 Timotheo 3:16,17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kanuni iliyofungwa- je! Maana yake ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries