Swali
Karama ya kiroho ya rehema ni gani?
Jibu
Katika Uhubiri wa Yesu wa Mlimani, mojawapo ya sifa za heri ni "Heri walio na huruma, maana watahurumiwa" (Mathayo 5: 7). Hurumani ni kile tunachoonyesha tunapoongozwa na Mungu kuwa na huruma katika mtazamo wetu, maneno na vitendo. Ni zaidi ya kuhisi huruma kwa mtu; ni upendo kimatendo. Huruma huitaji kujibu mahitaji ya dharura ya wengine na kupunguza machungu, upweke, na huzuni. Huruma hushughulikia matatizo ya kimwili, kihisia, kifedha, au kiroho kwa huduma ya kujitolea. Huruma huwatetea wa kiwango cha chini, maskini, wanaokandamizwa, na waliosahaulika na mara nyingi anatekeleza kwa niaba yao.
Mfano mzuri wa rehema hupatikana katika Mathayo 20: 29-34: "Yesu alipokuwa anaondoka majini Yeriko, umati wa watu ulimfuata. Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaza sauti: "Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie!" Ule umati wa watu ukwakemea na kuwaambia wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti: "Bwana Mwana wa Daudi, utuhurumie!" Yesu akasimama, akawaita na kuwauliza, "Mnataka niwafanyie nini?" Wakamjibu, "Bwana, tunaomba macho yetu yafumbuliwe." Basi, Yesu akwaonea huruma, akawagusa macho yao, nap apo hapo wakaweza kuona, wakamfuata." Kumbuka kwamba watu wale vipofu walihusisha huruma si kwa hisia lakini kwa hatua. Tatizo lao la kimwili ni kwamba hawakuweza kuona, hivyo kwao, tendo la rehema lilikuwa Kristo kuingilia kati ili warejeshee macho yao. Rehema ni zaidi ya hisia; daima hufuatanishwa na hatua.
Karama hii ina matumizi halisi ya huduma ya kazi pamoja na wajibu wa kufanya hivyo kwa furaha (Warumi 12: 8). Zaidi ya hayo, sisi sote tumeitwa kuwa na huruma. Yesu anasema katika Mathayo 25:40 kwamba "kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi." Mathayo 5: 7 huahidi huruma kwa wale walio na huruma kwa wengine. Kama wafu wa kiroho na vipofu wenye dhambi, sisi sio bora zaidi kuliko wale watu wawili vipofu katika Mathayo 20. Kama vile walikuwa wanategemea kabisa huruma ya Kristo ili kurejesha macho yao, ndivyo tunavyomtegemea Yeye "kutuonyesha rehema yake na kutupa sisi Wokovu wake "(Zaburi 85: 7). Ufahamu huu wa kiini kwamba tumaini letu linategemea huruma ya Kristo peke yake na si katika sifa yoyote yetu inapaswa kututia moyo kufuata mfano wa Kristo wa huduma ya huruma na kuonyesha huruma kwa wengine kama ilivyoonyeshwa kwetu.
English
Karama ya kiroho ya rehema ni gani?