Swali
Je! inamaanisha nini kuwa wokovu ni karama kutoka kwa Mungu?
Jibu
Neno karama ni la maana sana katika Biblia, ni vyema tuelewe fafanusi yake na Atari zake.
Katika Agano Jipya kunayo meneno mengi ya Kigiriki yalitafsiriwa "karama." Baadhi ya maneno haya yametumika katika muktadha mbali na ule wa karama ya wokovu ya Mungu, kama vile kupeana zawadi kwa wana sherehe (Ufunuo 11:10), vilitu vilivyo pokelewa kutoka kwa baba (Mathayo 7:11), matoleo kwa huduma (Wafilipi 4:17), na zawadi za mamajuzi (Mathayo 2:11).
Walakini, inapofikia maswala ya wokovu wetu, waandishi wa Agano Jipya wanatumia maneno tofauti ya Kigiriki-maneno yanayosisitiza karama ya neema nay a bure. Hapa kuna maneno mawili ambayo hutumika mara nyingi kwa karama ya wokovu:
1) Dorea, kumaanisha "karama ya bure." Neno hili linatia msisitizo katika hali ya bure ya karama- ni kitu kilichopeanwa zaidi na kupita matarajio au jinsi unavyostahili. Kila wakati linatumika hili neno linahusiana na karama za kiroho kutoka kwa Mungu. Hiki ndio kile Yesu alimpatia ule mwanamke wa Samaria kisimani (Yohana 4:10). Ni zawadi "isiyosemeka [isiyoelezeka]" katika 2 Wakorintho 9:15). Karama hii ya neema inatambulika kama Roho Mtakatifu katika Matendo 2:38; 8:20; na 11:17.
Kitenzi ambacho neno dorean lilitafsiriwa kutoka "bure" katika Mathayo 10:8; 2 Wakorintho 11:7; Ufunuo 21:6; 22:17. Katika Warumi 3:24 pindi tu baada ya tamko la Mungu la hatia yetu, tuna matumizi ya dorean: Lakini kwa zawadi ya neema ya Mungu, watu wote hukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Yesu Kristo." Karama ya wokovu ni ya bure, na nia ya karama hiyo sio kingine mbali na neema ya Anayetoa.
Kwa hiaba kubwa, linamaanisha "karama ya neema." Neno hili limetumika kufafanua wokovu katika Warumi 5:15-16. Pia, katika Warumi 6:23: "Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa Mungu ni uhai wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu." Neno lili hili limetumika kwa mkabala na karama za Kiroho baada ya wokovu (Warumi 12:6; 1 Timotheo 4:14; 2 Timotheo 1:6; 1 Petro 4:10).
Kwa wazi, ikiwa kitu ni "karama ya neema," hakiwezi kulipiewa. Kufanyia kitu kazi unakistahili, na hiyo itakuza uwajibikaji-zawadi ya deni, vile ilikuwa. Hiyo ndiyo sababu matendo huaribu neema (Warumi 4:1-5; 11:5-6).
Wakati wanawakilisha wokovu, waandishi wa Agano Jipya kwa makini walichagua maneno yanasisitiza neem ana uhuru. Kwa sababu hiyo, Biblia haingekuwa wazi zaidi- wokovu ni wa bure kabisa, karama ya kweli ya Mungu katika Kristo, na jukumu letu pekee ni kiupokea karama hiyo kwa imani ( Yohana 1:12; 3:16; Waefeso 2:8-9).
English
Je! inamaanisha nini kuwa wokovu ni karama kutoka kwa Mungu?